Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watii kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini.
Alhamisi, 30 Novemba 2017
Jumatano, 29 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sitisha Huduma ya Kidini
Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu ameamulia kabla watu wengi kumhudumia Yeye, wakiwemo watu kutoka kila nyanja ya maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake Mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni imetimia. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia Yeye. Kila mtu anayehudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na uweza wa Mungu, pamoja na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni.
Jumanne, 28 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kuzingatia Matendo Yako
Kulingana na vitendo na matendo katika maisha yenu, nyote mnahitaji kurasa za maneno ya kuwajaza na kuwajenga kila siku, kwani mko na upungufu mno, na ujuzi na maarifa yenu ya kupokea ni ya hali ya chini sana. Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilamali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa. Kila siku Ninatazama mienendo yenu na kuchunguza nia yenu na matunda yenu maovu.
Jumatatu, 27 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kutanafusi kwa Mwenyezi Mungu
Kunayo siri kubwa moyoni mwako. Huwezi kuijua hapo kwa sabubu umekuwa ukiishi katika ulimwengu usio na mwanga unaoangaza. Moyo wako na roho yako vimechukuliwa mateka na yule mwovu. Macho yako yamefunikwa na giza; huwezi kuliona jua likiangaza angani, wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yatiririkayo kutoka katika kiti cha enzi.
Ijumaa, 24 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu
![]() |
Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo.
Alhamisi, 23 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu
Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kutimiza kwa ujumla mahitaji Yangu, kwa hiyo lazima Nilenge suala moja kwa moja na kuwafafanulia moyo na akili Zangu. Tukichukulia kwamba uwezo wenu wa utambuzi na ufahamu wenu vyote ni duni sana, karibu mmekosa kabisa kujua tabia na dutu Yangu, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuhusu haya.
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maonyo Matatu
Kama muumini wa Mungu, hamfai kuwa watiifu kwa yeyote mwengane isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla mwisho wenu haujaamuliwa, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu.
Jumanne, 14 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wewe U Mwaminifu kwa Nani?
![]() |
Kila siku unayoiishi sasa ni ya maana sana na muhimu sana kwa hatima yako na majaliwa yako, kwa hivyo unapaswa kufurahia kila ulicho nacho na kila dakika inayopita. Unapaswa kutumia muda wako vizuri ili uweze kujinufaisha, ili usije kuishi maisha haya bure. Pengine unajihisi kukanganyikiwa unaojiuliza ni kwa nini Ninazungumza maneno haya. Kwa kweli, Sijapendezwa na matendo ya yeyote kati yenu.
Jumatatu, 13 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kufanya Matendo Mema ya Kutosha Ili Uandae Mwisho Wako wa Safari
![]() |
Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, ni wazi kwamba, Nimezungumza vizuri pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia.
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli
Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yalivyo, kukamilisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote walioingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote waliokuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe.
Ijumaa, 10 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Je, Wewe ni Muumini wa Kweli wa Mungu?
Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu.
Jumanne, 7 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo
Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi.
Jumatatu, 6 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa
Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati yao ni wale wanaohudumu kama makuhani, wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Ninaweka migawo hii kulingana na uaminifu alionao mwanadamu Kwangu. Wanadamu wote wakitofautishwa kulingana na aina, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu.
Jumamosi, 4 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mwanadamu Anaweza Kuokolewa Tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu
Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu.
Alhamisi, 2 Novemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini
![]() |
Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yananayomkabili maishani.
Maonyesho ya Awali ya Video za Injili | Biblia Ndiyo Bwana, ama Ni Mungu? “Bwana Wangu Ni Nani”
Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.” Moyoni mwake, Biblia ni kuu. Kwa sababu ya upendo na imani yake pofu katika Biblia, hajawahi kutafuta au kuitazama kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho.
Jumanne, 31 Oktoba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Biblia (4)
![]() |
Watu wengi wanaamini kwamba kuelewa na kuwa na uwezo wa kufasiri Biblia ni sawa na kutafuta njia ya kweli—lakini, kimsingi, je, vitu ni rahisi sana? Hakuna anayejua uhalisia wa Biblia: kwamba si kitu chochote zaidi ya rekodi ya kihistoria ya kazi ya Mungu, na agano la hatua mbili zilizopita za kazi ya Mungu, na haikupatii ufahamu wa malengo ya kazi ya Mungu. Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba inarekodi hatua mbili za kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Agano la Kale linaandika historia ya Israeli na kazi ya Yehova kuanzia wakati wa uumbaji hadi mwisho wa Enzi ya Sheria.
Jumamosi, 21 Oktoba 2017
maneno ya Mwenyezi Mungu | Tamko La Kwanza
maneno ya Mwenyezi Mungu | Tamko La Kwanza
![]() |
| Kanisa la Mwenyezi Mungu |
Je, wale wanaoshuhudia maneno Yangu huyakubali kwa kweli? Je, mnanijua kwa kweli? Mmejifunza utiifu kweli? Ninyi hutumia rasilimali kwa ajili Yangu kwa uaminifu? Mmekuwa na ushuhuda thabiti, usiokubali kushindwa Kwangu mlipokabiliwa na joka kuu jekundu? Je, moyo wenu wa ibada hulifedhehesha kweli joka kuu jekundu? Ni kupitia tu kwa jaribio la maneno Yangu ndipo Naweza kutimiza lengo Langu la kulitakasa kanisa na kuwachagua wale wanaonipenda Mimi kweli. Ni jinsi gani tena ambayo mtu yeyote angenielewa Mimi? Ni nani anaweza kuelewa uadhama Wangu, ghadhabu Yangu, na hekima Yangu kupitia kwa maneno Yangu? Nitakamilisha Nilichoanza, lakini bado ni Mimi nipimaye mioyo ya wanadamu. Kwa kweli, hakuna mwanadamu anayenielewa Mimi kwa ukamilifu, kwa hiyo Ninamwongoza kwa maneno, na kumwongoza katika mwongo mpya kwa njia hii. Mwishowe Nitakamilisha kazi Yangu yote kupitia kwa maneno Yangu, na kuwarudisha wale wanaonipenda Mimi kweli kwa ufalme Wangu, kuishi mbele ya kiti Changu cha enzi. Hali sio kama ilivyokuwa wakati fulani, na kazi Yangu imeingia katika kiwango kipya cha kuanza. Hilo likiwa hivyo, kutakuwa na njia mpya: Wale wanaolisoma neno Langu na kulikubali kama uzima wao kabisa ndio watu wa ufalme Wangu. Kwa vile wako katika ufalme Wangu, wao ni watu Wangu katika ufalme. Wanapoongoza na maneno Yangu, ingawa wanatajwa kama watu Wangu, wao kamwe hawako chini ya 'wana' Wangu. Kama watu Wangu, wote ni lazima wawe waaminifu katika ufalme Wangu na kutimiza majukumu yao, na wale wanaokosea amri Zangu za usimamizi lazima wapate adhabu Yangu. Hili ni onyo Langu kwa wote.
Ijumaa, 20 Oktoba 2017
Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)
Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)
Sauti
ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa
I
Nilitaka
kulia lakini hakuna mahali palihisi sawa.
Nilitaka
kuimba lakini hakuna wimbo ulipatikana.
Nilitaka
kuonyesha upendo wa kiumbe aliyeumbwa.
Nikitafuta
juu na chini, lakini hakuna maneno yangeweza kusema,
yangeweza
kusema jinsi hasa ninavyohisi.
Mungu
wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu.
Nainua
mikono yangu kwa sifa, ninafurahia kwamba Ulikuja katika dunia hii.
Jumapili, 24 Septemba 2017
Mwenyezi Mungu | Kuhusu Biblia (3)
Sio kila kitu katika Biblia ni rekodi ya
maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za
kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na
sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu
katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya
kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana
nyingi za kibinadamu, upendelevu wa kibinadamu, na ufasiri wa ajabu wa
kibinadamu. Ni kweli, maneno mengi ni matokeo ya kupatiwa nuru na kuangaziwa na
Roho Mtakatifu, na ni tafsiri sahihi—lakini haiwezi kusemwa kuwa ni
udhihirishaji sahahi kabisa wa ukweli. Maoni yao juu ya vitu fulani si chochote
zaidi ya maarifa uzoefu binafsi, au kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Utabiri wa
manabii ulikuwa umetolewa na Mungu mwenyewe: Unabii wa Isaya, Danieli, Ezra,
Yeremia, na Ezekieli, ulitoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu, watu hawa
walikuwa ni waonaji maono, walipokea Roho ya Unabii, wote walikuwa ni manabii
wa Agano la Kale. Wakati wa Enzi ya Sheria watu hawa, ambao walikuwa wamepokea
ufunuo wa Yehova, walizungumza unabii mwingi, ambao ulisemwa na Yehova moja kwa
moja. Na kwa nini Yehova alifanya kazi ndani yao? Kwa sababu watu wa Israeli
walikuwa ni wateule wa Mungu: Kazi ya manabii ilipaswa kufanyika miongoni mwao,
na walikuwa wamefuzu kupokea maono hayo. Kimsingi, wao wenyewe hawakuelewa
ufunuo wa Mungu kwao. Roho Mtakatifu Alizungumza maneno hayo kupitia vinywa
vyao ili watu wa baadaye waweze kuelewa mambo hayo, na kuona kwamba ni kweli
ilikuwa ni kazi ya Roho wa Mungu, ya Roho Mtakatifu, na haikutoka kwa
mwanadamu, na kuweza kuwathibitishia kazi ya Roho Mtakatifu. Wakati wa Enzi ya
Neema, Yesu Mwenyewe Alifanya kazi hii yote badala yao, na hivyo watu
hawakuzungumza tena unabii. Kwa hivyo Yesu alikuwa nabii?
Ijumaa, 22 Septemba 2017
Upendo wa Mungu | Dansi ya Bale "Kama Nisingeokolewa na Mungu"
Kama Nisingeokolewa na Mungu
Kama mimi nisingeokolewa na Mungu,
ningekuwa bado nazurura ulimwenguni humu,
nikipambana kwa bidii na maumivu katika
dhambi; kila siku huwa ya taabu isiyo na tarajio.
Kama nisingeokolewa na Mungu, bado
ningekuwa nimepondwa chini ya miguu ya shetani,
kama nimenaswa katika dhambi na starehe
zake, bila kujua maisha yangu yangekuwaje.
Kama nisingeokolewa na Mungu, nisingekuwa
na baraka zangu leo,
wala kujua kwa nini sisi tuendelee kuishi
ama maana ya maisha yetu.
Jumatano, 20 Septemba 2017
Mwenyezi Mungu | Kuhusu Biblia (2)
Biblia pia huitwa
Agano la Kale na Agano Jipya. Je, wajua “agano” linarejelea nini? “Agano”
katika “Agano Jipya” linatokana na makubaliano ya Yehova na watu wa Israeli
Alipowaua Wamisri na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Farao. Bila Shaka,
uthibitisho wa haya makubaliano ulikuwa damu ya mwanakondoo iliyopakwa kwenye
linta kupitia kwayo Mungu Alianzisha agano na mwanadamu, moja ambalo ilisemwa
kuwa wale wote waliokuwa na damu ya mwanakondoo juu na pembeni mwa viunzi vya
mlango walikuwa Waisraeli, walikuwa wateuliwa wa Mungu, na wote wangeokolewa na
Yehova (kwa kuwa Yehova wakati ule Alikuwa karibu kuwaua wazaliwa wa kwanza wa
kiume wa Misri wote na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe).
Jumapili, 17 Septemba 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Biblia (1)
Biblia inapaswa kuangaliwaje kuhusiana na imani kwa Mungu? Hili ni swali muhimu sana. Kwa nini tunawasiliana swali hili? Kwa sababu wakati ujao utaeneza injili na kupanua kazi ya Enzi ya Ufalme, na haitoshi tu kuweza kuzungumza juu ya kazi ya Mungu leo. Ili kupanua kazi Yake, ni muhimu zaidi kwamba unakuwa na uwezo wa kubadilisha dhana za watu za dini ya kale na njia za kale za imani, na kuwaacha wakiwa wameshawishika kabisa—na kufikia katika hoja hiyo Biblia inahusishwa. Kwa miaka mingi, imani ya watu ya kitamaduni (hiyo ya Ukristo, moja ya dini kuu tatu za dunia) imekuwa ni kusoma Biblia; kujitenga na Biblia sio imani kwa Bwana, kujitenga na Biblia ni madhehebu maovu, na uzushi, na hata pale watu wanaposoma vitabu vingine, msingi wa vitabu hivi ni lazima uwe ni ufafanuzi wa Biblia.
Jumamosi, 16 Septemba 2017
Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu" (Video Rasmi ya Muziki)
Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu
Mpaka siku moja,
utahisi kuwa Muumba
sio fumbo tena,
kwamba Muumba hajawahi kufichwa kutoka
kwako,
kwamba Muumba
hajawahi kuificha sura Yake kutoka kwako,
kwamba Muumba hayuko mbali na wewe hata
kidogo,
kwamba Muumba siye Yule unayemtamania
katika mawazo yako
lakini kwamba huwezi kumfikia na hisia
zako,
kwamba Anasimama kwa kweli kama mlinzi
kulia na kushoto kwako,
Akiruzuku maisha yako, na kudhibiti
majaliwa yako, kudhibiti majaliwa yako.
Hayuko katika upeo wa mbali, wala
hajajificha juu mawinguni.
Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya
kila kitu chako,
Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni
kitu pekee ulicho nacho.
Jumapili, 10 Septemba 2017
Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada "Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki"
Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki
Mungu aliipa Israeli utukufu Wake kisha
Akauhamisha mbali na pale,
na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote
Mashariki.
Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga
ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na
mwanga,
wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta
mwanga.
Mungu atawaacha wote wanaotafuta kuuona
mwanga tena
na utukufu Aliokuwa nao katika Israeli,
kuona kwamba Mungu tayari ameshuka chini
juu ya wingu jeupe miongoni mwa watu,
na kuona mawingu mengi meupe, na kuona
vishada vya matunda,
kumwona Yehova Mungu wa Israeli, Mungu wa
Israeli,
kumwona Mkuu wa Wayahudi, kumwona Masihi
Aliyengojewa,
na kuonekana kamili kwa Yeye aliyeteswa na
wafalme katika enzi zote.
Ijumaa, 1 Septemba 2017
NYENDO ZA MATESO YA KIDINI NCHINI CHINA
Tangu kilipokuja mamlakani katika China Bara mnamo mwaka wa 1949, Chama Cha Kikomunisti cha China kimekuwa hakikomi katika mateso yake kwa imani ya kidini. Kwa wayowayo kimewashika na kuwaua Wakristo, kuwafukuza na kuwadhulumu wamishonari wanaofanya kazi nchini China, wakachukua ngawira na kuchoma nakala nyingi za Biblia, wakafunga kabisa na kubomoa majengo ya kanisa, na bila mafanikio wakajaribu kukomesha makanisa yote ya nyumbani. Miaka ya hivi karibuni pia imeona sera za serikali ya CCP zikianzishwa kwa kiwango kikubwa kwa lengo la "Usimilishaji " wa Ukristo. Maelfu ya misalaba ya makanisa yamevunjwa, majengo mengi ya kanisa yambomolewa, na idadi kubwa ya Wakristo katika makanisa ya nyumbani wamekamatwa na kuteswa. Makanisa ya Kikristo nchini China hupitia mateso ya ukatili na ya umwagikaji wa damu ...
Filamu hii kwa uaminifu na bila upendeleo inanakili uzoefu halisi wa mateso waliyoyapitia Wakristo wa China katika mikono ya serikali ya CCP. Wakristo wanaoteswa katika filamu hii ni watu kutoka kwa vikundi vya kidini na madhehebu tofauti ambao walitafuta ukweli, na ambao waliisikia sauti ya Mungu na hivyo wakarudi kwa Mwenyezi Mungu. Walitembea njia sahihi ya uzima, lakini kwa wayowayo walishikwa na serikali ya CCP. Baadhi yao walifungwa, wengine wakateswa kwa namna yoyote, wengine wanaishi maisha ya wakimbizi kama wametengwa na waume au wake zao na watoto wao, na wengine hata walilemazwa au kuuawa kutokana na kutendewa vibaya. Filamu hii iliyopigwa vizuri sana inajaribu kusanifu upya kilichotokea kweli wakati huo, na hutoa tafakuri ya kina ya kuingiliwa bila haya kwa imani za kidini na haki za kibinadamu za Wakristo wa China. Ni nafasi ya kuelewa maisha ya kweli ya Wakristo wa China na familia za Kikristo, pamoja na tafakuri—inayoonekana mara chache katika miaka ya hivi karibuni—ya uzoefu na hisia za Wakristo wa China ambao wameteswa kwa sababu ya imani yao.
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.
YouTube:https://www.youtube.com/c/KanisalaMwe...Facebook:https://www.facebook.com/kingdomsalvationsw/
Twitter:https://twitter.com/CAGchurchsw
Blogger:http://nikanisalamwenyezimungu.blogs...
Instagram:https://www.instagram.com/thechurchof...
Email: contact.sw@kingdomsalvation.org
Alhamisi, 31 Agosti 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu|WANADAMU WAMEUPATA TENA UTAKATIFU WAO WALIOKUWA NAO AWALI
Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho
Facebook:https://www.facebook.com/kingdomsalvationsw/
Twitter:https://twitter.com/CAGchurchsw
Blogger:http://nikanisalamwenyezimungu.blogs...
Instagram:https://www.instagram.com/thechurchof...
Email: contact.sw@kingdomsalvation.org
Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mwisho. Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, Mungu ndiye Mpanzi, na Mvunaji (Mvunaji). Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho; Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji. Mungu Anakuwa mwili hasa kwa ajili ya kuikaribisha enzi mpya, na, kwa hakika, Anapoikaribisha enzi mpya, Atakuwa Ameikamilisha enzi ya kale wakati uo huo. Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.Ha! Ha! Ha! Ha! Kila wakati Yeye Mwenyewe Anapofanya kazi miongoni mwa mwanadamu, ni mwanzo wa mapigano mapya. Bila mwanzo wa kazi mpya, kwa kawaida hakungekuwa na kikomo kwa enzi ya kale. Na bila kikomo kwa enzi ya kale ni thibitisho kuwa vita na Shetani, vita na Shetani havijafika mwisho. (Ha!)
Ni kama tu Mungu Mwenyewe Anakuja miongoni mwa mwanadamu na kutenda kazi mpya ndipo mwanadamu atakapoweza kujitoa kutoka katika miliki ya Shetani, miliki ya Shetani, na kupata maisha mapya, maisha mapya na mwanzo mpya. Vinginevyo, mwanadamu ataishi milele katika enzi ya kale na milele kuishi katika ushawishi wa kale wa Shetani, katika ushawishi wa kale wa Shetani. Ha! Ha! Ha! Ha! Katika kila enzi inayoongozwa na Mungu, sehemu ya mwanadamu huwekwa huru, na hivyo, mwanadamu huendelea na kazi ya Mungu kuelekea enzi mpya. Ushindi wa Mungu ni ushindi kwa wale wote ambao humfuata Yeye. Ushindi wa Mungu in ushindi, ushindi kwa wale wote wanaomfuata Yeye. Katika kila enzi inayoongozwa na Mungu, sehemu ya mwanadamu huwekwa huru, na hivyo, mwanadamu huendelea na kazi ya Mungu kuelekea enzi mpya. Ushindi wa Mungu ni ushindi kwa wale wote ambao humfuata Yeye. Ushindi wa Mungu ni ushindi kwa wale wote ambao humfuata Yeye.
Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho, Mungu ndiye Mpanzi na Mvunaji.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.
YouTube:https://www.youtube.com/c/KanisalaMwe...Facebook:https://www.facebook.com/kingdomsalvationsw/
Twitter:https://twitter.com/CAGchurchsw
Blogger:http://nikanisalamwenyezimungu.blogs...
Instagram:https://www.instagram.com/thechurchof...
Email: contact.sw@kingdomsalvation.org
Jumatano, 30 Agosti 2017
Mwenyezi Mungu|Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake
Kiini cha imani ya watu wengi katika Mungu ni imani za kidini: Hawana uwezo wa kumpenda Mungu, na wanaweza kumfuata Mungu tu kama roboti, bila kuweza kumtamani Mungu, ama kumwabudu. Wanamfuata tu kimyakimya. Watu wengi wanamwamini Mungu, lakini wapo wachache sana ambao humpenda Mungu; wanamheshimu tu Mungu kwa sababu wanaogopa majanga, au hata wanamstahi Mungu kwa sababu ni Mwenye nguvu na aliye juu—lakini katika kumheshimu na kuvutiwa kwao hakuna upendo au kutamani kwa kweli.
Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kuijua Kazi ya Mungu Leo
Kuijua kazi ya Mungu katika nyakati hizi, kwa sehemu kubwa, ni kumjua Mungu katika mwili wa siku za mwisho, kile ambacho ni huduma Yake kuu, na kile ambacho Amekuja kufanya duniani. Hapo mwanzoni Nimesema katika maneno Yangu kwamba Mungu Amekuja duniani (wakati wa siku za mwisho) ili kuweka mfano kabla Hajaondoka. Ni kwa jinsi gani Mungu Ameuweka mfano huu? Kwa kuzungumza maneno, kwa kufanya kazi na kuzungumza katika nchi nzima.
Ijumaa, 25 Agosti 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu|Sitisha Huduma ya Kidini
Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu ameamulia kabla watu wengi kumhudumia Yeye, wakiwemo watu kutoka kila nyanja ya maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake Mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni imetimia. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia Yeye. Kila mtu anayehudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu.
Jumanne, 22 Agosti 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu|Waovu Lazima Waadhibiwe
Kukagua kama unatenda uhaki katika kila jambo unalotenda, na iwapo matendo yako yanachunguzwa na Mungu, ni tabia za kanuni za wale wanaomwamini Mungu. Utaitwa mwenye haki kwa sababu una uwezo wa kukidhi matakwa ya Mungu, na kwa sababu umekubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wote wanaokubali utunzaji, ulinzi na ukamilishaji Wake na wale waliopatwa Naye, ni wenye haki na hutazamwa kwa upendo sana Mungu. Zaidi ya unavyokubali neno la Mungu wakati huu, ndivyo unavyoweza kupokea na kuelewa mapenzi ya Mungu zaidi, na hivyo ndivyo unavyoweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu na kukidhi mahitaji Yake. Haya ndiyo maagizo ya Mungu kwako na kile unapaswa kufikia.
Jumatatu, 21 Agosti 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu|Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja
Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mungu alianza tu kazi Yake ya usimamizi baada ya ubinadamu kuwepo na baada ya ubinadamu kupotoshwa. Kutoka hapa kuendelea, Mungu hakupumzika tena lakini badala yake Alianza kufanya kazi miongoni mwa ubinadamu. Ilikuwa kwa sababu ya upotovu wa ubinadamu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake, na ilikuwa pia kwa sababu ya uasi wa malaika mkuu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake. Iwapo Mungu hatamshinda Shetani na kuokoa ubinadamu, ambao umepotoshwa, Mungu hatawahi tena kuweza kuingia rahani. Mungu anakosa pumziko akosavyo mwanadamu. Wakati Mungu ataingia rahani tena, mwanadamu pia ataingia rahani. Maisha ya pumziko ni yale bila vita, bila uchafu, bila udhalimu unaoendelea. Hii ni kusema kwamba hayana unyanyasaji wa Shetani (hapa “Shetani” inamaanisha nguvu za uhasama), upotovu wa Shetani, na pia uvamizi wa nguvu yoyote inayompinga Mungu. Kila kitu kinafuata aina yake na kuabudu Bwana wa uumbaji. Mbingu na dunia ni shwari kabisa. Haya ni maisha matulivu ya ubinadamu. Mungu aingiapo rahani, hakuna udhalimu wowote utaoendelea duniani, na hakutakuwa na uvamizi wowote wa nguvu za uhasama. Ubinadamu pia utaingia ulimwengu mpya; hawatakuwa tena ubinadamu uliopotoshwa na Shetani, lakini badala yake ubinadamu ambao umeokolewa baada ya kupotoshwa na Shetani. Siku ya pumziko ya ubinadamu pia ni siku ya pumziko ya Mungu. Mungu alipoteza pumziko Lake kwa sababu mwanadamu hakuweza kuingia rahani; haikuwa kwamba Hakuweza awali kupumzika. Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomwunga Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo. Mungu kuingia rahani kunamaanisha kwamba Hatafanya tena kazi Yake ya wokovu wa ubinadamu. Ubinadamu kuingia rahani kunamaanisha kwamba ubinadamu wote utaishi ndani ya mwangaza wa Mungu na chini ya baraka Zake; hakutakuwa na upotovu wowote wa Shetani, wala maovu yoyote kutokea. Ubinadamu utaishi kama kawaida duniani, na utaishi chini ya ulinzi wa Mungu. Mungu na mwanadamu waingiapo rahani pamoja, kutamaanisha kwamba ubinadamu umeokolewa na kwamba Shetani ameangamizwa, kwamba kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu imemalizika kabisa. Mungu hataendelea tena kufanya kazi miongoni mwa mwanadamu, na mwanadamu hataendelea tena kumilikiwa na Shetani. Kwa hivyo, Mungu hatakuwa shughulini tena, na mwanadamu hatakimbiakimbia tena; Mungu na mwanadamu wataingia rahani wakati huo huo. Mungu atarudia nafasi yake ya awali, na kila mtu atarudia nafasi yake husika. Hizi ndizo hatima ambazo Mungu na mwanadamu wataishi ndani kwa utaratibu huu baada ya mwisho wa usimamizi wote wa Mungu. Mungu ana hatima ya Mungu na mwanadamu ana hatima ya mwanadamu. Apumzikapo, Mungu ataendelea kuuongoza ubinadamu wote kwa maisha yao duniani. Akiwa kwa mwangaza wa Mungu, mwanadamu atamwabudu Mungu wa kweli aliye mbinguni. Mungu hataishi tena miongoni mwa ubinadamu, na mwanadamu pia hataweza kuishi na Mungu katika hitimisho la Mungu. Mungu na mwanadamu hawawezi kuishi ndani ya ulimwengu sawa; badala yake, wote wawili wana njia zao binafsi za kuishi. Mungu ndiye anayeongoza ubinadamu wote, wakati ubinadamu wote ni matokeo ya kazi ya Mungu ya usimamizi. Ni ubinadamu unaoongozwa; kuhusu kiini, ubinadamu si sawa na Mungu. Kuingia rahani kunamaanisha kurudi pahali pa awali pa mtu. Kwa hivyo, Mungu aingiapo rahani, kunamaanisha kwamba Mungu amerudi pahali Pake pa awali. Mungu hataishi tena duniani ama kushiriki kwa furaha na mateso ya ubinadamu wakati yupo miongoni mwa ubinadamu. Ubinadamu unapoingia rahani, kunamaanisha kwamba mwanadamu amekuwa kiumbe halisi; ubinadamu utamwabudu Mungu ukiwa duniani na kuwa na maisha ya kawaida ya wanadamu. Watu hawatakuwa tena wasiomtii Mungu ama kumpinga Mungu; watarudia maisha asili ya Adamu na Hawa. Haya ndiyo maisha na hatima binafsi ya Mungu na ubinadamu baada ya kuingia rahani. Kushindwa kwa Shetani ni mwelekeo usioepukika katika vita kati ya Mungu na Shetani. Kwa njia hii, kuingia kwa Mungu rahani baada ya kukamilika kwa kazi Yake ya usimamizi na wokovu kamili wa mwanadamu na kuingia rahani pia kunakuwa mielekeo isiyoepukika. Pahali pa pumziko pa mwanadamu ni duniani, na pahali pa Mungu pa pumziko ni mbinguni. Mwanadamu apumzikapo, atamwabudu Mungu na pia kutoka mbinguni kuishi duniani, na apumzikapo Mungu, ataongoza sehemu iliyobaki ya ubinadamu; Atawaongoza, sio kutoka duniani. Mungu bado atakuwa Roho, wakati mwanadamu bado atakuwa mwili. Mungu na mwanadamu wote wawili wana njia zao tofauti za kupumzika. Mungu anapopumzika, Atakuja na kujitokeza miongoni mwa mwanadamu, mwanadamu anapopumzika, ataongozwa na Mungu kutembea mbinguni na pia kufurahia maisha mbinguni. Baada ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani, Shetani hatakuweko tena, na kama Shetani, wale watu waovu pia hawatakuweko tena. Kabla ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani, wale watu waovu waliomtesa Mungu wakati mmoja duniani na adui waliokuwa hawamtii duniani watakuwa tayari wameangamizwa; watakuwa wameangamizwa na majanga makubwa ya siku za mwisho. Baada ya hao watu waovu kuangamizwa kabisa, dunia haitajua tena unyanyasaji wa Shetani. Ubinadamu utapata wokovu kamili, na hapo tu ndipo kazi ya Mungu itaisha kabisa. Haya ndiyo masharti ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani.
Kukaribia kwa mwisho wa kila kitu kunaonyesha mwisho wa kazi ya Mungu na kunaonyesha mwisho wa maendeleo ya ubinadamu. Hii inamaanisha kwamba ubinadamu kama ulivyopotoshwa na Shetani umefika mwisho wake wa maendeleo, na kwamba vizazi vya Adamu na Hawa vimeenea hadi mwisho wao binafsi, na pia inamaanisha kwamba haiwezekani kwa ubinadamu kama huo, baada ya kupotoshwa na Shetani, kuendelea kustawi. Adamu na Hawa wa mwanzoni hawakuwa wamepotoshwa, lakini Adamu na Hawa waliofukuzwa kutoka Bustani ya Edeni walivurugwa na Shetani. Wakati Mungu na mwanadamu wanaingia rahani pamoja, Adamu na Hawa—waliofukuzwa kutoka Bustani ya Edeni—na vizazi vyao hatimaye watafika mwisho; ubinadamu wa baadaye bado utakuwa na vizazi vya Adamu na Hawa, lakini hawatakuwa watu wanaomilikiwa na Shetani. Badala yake, watakuwa watu waliookolewa na kutakaswa. Huu utakuwa ubinadamu ambao umehukumiwa na kuadibiwa, na ulio takatifu. Hawa watu hawatakuwa sawa na jamii ya binadamu kama ilivyokuwa awali; mtu anaweza kusema kwamba hao ni watu wa aina tofauti kabisa na Adamu na Hawa wa awali. Hawa watu watakuwa wamechaguliwa kutoka miongoni mwa wote waliopotoshwa na Shetani, na watakuwa ndio watu ambao hatimaye wamesimama imara wakati wa hukumu na kuadibu kwa Mungu, watakuwa kundi la mwisho la watu miongoni mwa wanadamu potovu. Kundi hili la watu ndilo tu litaweza kuingia katika raha ya mwisho pamoja na Mungu. Wanaoweza kusimama imara wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu siku za mwisho—yaani, wakati wa kazi ya mwisho ya utakaso—watakuwa wale watakaoingia katika raha ya mwisho na Mungu; kwa hivyo, wanaoingia rahani wote watakuwa wametoka katika ushawishi wa shetani na kupokewa na Mungu baada tu ya kupitia kazi Yake ya mwisho ya utakaso. Hawa watu ambao hatimaye wamepokewa na Mungu wataingia katika raha ya mwisho. Kiini cha kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu ni kutakasa ubinadamu, na ni ya siku ya raha ya mwisho. Vinginevyo, ubinadamu wote hautaweza kufuata aina yao ama kuingia katika raha. Hii kazi ni njia ya pekee ya ubinadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa ubinadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa ubinadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaobaki watatakaswa na kufurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani waingiapo ulimwengu wa juu wa ubinadamu; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya ubinadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Ubinadamu wa baadaye hautakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni mashabaha ya adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki. Walikuwa wamekombolewa wakati mmoja, na pia walikuwa wamehukumiwa na kuadibiwa; walikuwa pia wamemhudumia Mungu wakati mmoja, lakini siku ya mwisho itakapofika, bado wataondolewa na kuangamizwa kwa sababu ya uovu wao na kwa sababu ya kutotii na kutokombolewa kwao. Hawatakuwa tena katika ulimwengu wa baadaye, na hawatakuweko tena miongoni mwa jamii ya binadamu ya baadaye. Watenda maovu wote na yeyote na wote ambao hawajaokolewa wataangamizwa wakati watakatifu miongoni mwa ubinadamu wataingia rahani, bila kujali kama wao ni roho za wafu ama wale wanaoishi bado katika mwili. Bila kujali enzi ya hizi roho zitendazo maovu na watu watenda maovu, ama roho za watu wenye haki na watu wanaofanya haki wako, mtenda maovu yeyote ataangamizwa, na yeyote mwenye haki ataishi. Iwapo mtu ama roho inapokea wokovu haiamuliwi kabisa kulingana na kazi ya enzi ya mwisho, lakini inaamuliwa kulingana na iwapo wamempinga ama kutomtii Mungu. Kama watu wa enzi ya awali walifanya maovu na hawangeweza kuokolewa, bila shaka wangekuwa mashabaha ya adhabu. Kama watu wa enzi hii wanafanya maovu na hawawezi kuokolewa, hakika wao pia ni mashabaha ya adhabu. Watu wanatengwa kwa msingi wa mema na mabaya, sio kwa msingi wa enzi. Baada ya kutengwa kwa msingi wa mema na mabaya, watu hawaadhibiwi ama kutuzwa mara moja; badala yake, Mungu atafanya tu kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wema baada ya kufanya kazi Yake ya ushindi katika siku za mwisho. Kwa kweli, Amekuwa akitumia mema na mabaya kutenga ubinadamu tangu Afanye kazi Yake miongoni mwa ubinadamu. Atawatuza tu wenye haki na kuwaadhibu waovu baada ya kukamilika kwa kazi Yake, badala ya kuwatenga waovu na wenye haki baada ya kukamilika kwa kazi Yake mwishowe na kisha kufanya kazi Yake ya kuwaadhibu waovu na kuwatuza wazuri mara moja. Kazi Yake ya mwisho ya kuadhibu waovu na kuwatuza wazuri inafanywa kabisa ili kutakasa kabisa ubinadamu wote, ili Aweze kuleta ubinadamu mtakatifu mno katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi. Kama Mungu hangewaangamiza waovu lakini badala yake kuwaacha wabakie, basi ubinadamu wote bado haungeweza kuingia rahani, na Mungu hangeweza kuleta ubinadamu katika ulimwengu bora. Kazi ya aina hii haingekuwa imekamilika kabisa. Atakapomaliza kazi Yake, ubinadamu wote utakuwa mtakatifu kabisa. Mungu anaweza kuishi kwa amani rahani kwa namna hii pekee.
Watu leo hawawezi kutengana na mambo ya mwili; hawawezi kuacha starehe za mwili, wala hawawezi kuiacha dunia, pesa, ama tabia yao potovu. Watu wengi wanaendelea na shughuli zao kwa hali ya uzembe. Kwa kweli, hawa watu hawana Mungu mioyoni mwao hata kidogo; zaidi ya hayo, hawamchi Mungu. Hawana Mungu mioyoni mwao, na hivyo hawawezi kutambua yote anayofanya Mungu, na hawawezi kabisa kuamini maneno Azungumzayo kwa mdomo Wake. Watu hawa ni wa mwili sana, wamepotoshwa sana na hawana ukweli wowote, zaidi ya hayo, hawaamini kwamba Mungu anaweza kuwa mwili. Yeyote asiyemwamini Mungu wa mwili—yaani, yeyote asiyeamini kazi na hotuba ya Mungu anayeonekana na haamini Mungu anayeonekana lakini badala yake anaabudu Mungu asiyeonekana mbinguni—hana Mungu katika moyo wake. Ni watu wasiomtii na wanaompinga Mungu. Watu hawa hawana ubinadamu na fahamu, kusema chochote kuhusu ukweli. Kwa watu hawa Mungu anayeonekana na kushikika hawezi kuaminika zaidi, lakini Mungu asiyeonekana wala kushikika ni Mungu wa kuaminika na pia Anayefurahisha nyoyo zao. Wanachotafuta si ukweli wa uhalisi, wala si kiini cha kweli cha uhai, wala nia za Mungu; badala yake, wanatafuta msisimko. Mambo yoyote yanayoweza kuwaruhusu kufikia tamaa zao ni, bila shaka, imani na shughuli zao. Wamwamini Mungu tu ili kuridhisha tamaa zao, si kutafuta ukweli. Hawa watu si watenda maovu? Wanajiamini sana, na hawaaamini kwamba Mungu aliye mbinguni atawaangamiza, hawa “watu wazuri.” Badala yake, wanaamini kwamba Mungu atawaruhusu kubaki na, zaidi ya hayo, Atawatuza vizuri sana, kwani wamemfanyia Mungu mambo mengi na kuonyesho kiwango kikubwa cha “uaminifu” Kwake. Kama wangemtafuta Mungu anayeonekana, wangelipiza kisasi mara moja dhidi ya Mungu na kukasirika wakati hawatapata tamaa zao. Hawa ni watu waovu wanaotaka kuridhisha tamaa zao; si watu wa uadilifu wanaosaka ukweli. Watu kama hao ni wale wanaojulikana kama waovu wanaomfuata Kristo. Wale watu wasioutafuta ukweli hawawezi kuamini ukweli. Hawawezi kabisa kutambua matokeo ya baadaye ya ubinadamu, kwani hawaamini kazi ama hotuba yoyote ya Mungu anayeonekana, na hawawezi kuamini hitimisho la baadaye la ubinadamu. Hivyo, hata wakimfuata Mungu anayeonekana, bado wanatenda maovu na hawatafuti ukweli, wala hawatendi ukweli Ninaohitaji. Wale watu wasioamini kwamba wataangamizwa kinyume ni kwamba ni wale watu watakaoangamizwa. Wote wanajiamini kuwa wajanja sana, na wanaamini kwamba wao wenyewe ndio wanaotenda ukweli. Wanafikiria mwenendo wao mbovu kuwa ukweli na hivyo wanauthamini. Hawa watu waovu wanajiamini sana; wanachukua ukweli kuwa mafundisho ya dini, na kuchukua vitendo vyao vibovu kuwa ukweli, na mwishowe watavuna tu walichopanda. Watu wanapojiamini zaidi na wanapokuwa na kiburi zaidi, ndipo hawawezi zaidi kupata ukweli; watu wanapomwamini Mungu wa mbinguni zaidi, ndipo wanampinga Mungu zaidi. Hawa ndio watu watakaoadhibiwa. Kabla ya ubinadamu kuingia rahani, iwapo kila aina ya mtu ataadhibiwa ama kutuzwa kutaamuliwa kulingana na iwapo wanatafuta ukweli, iwapo wanamjua Mungu, iwapo wanaweza kumtii Mungu anayeonekana. Waliomhudumia Mungu anayeonekana lakini bado hawamjui wala kumtii hawana ukweli. Watu hawa ni watenda maovu, na watenda maovu bila shaka wataadhibiwa; zaidi ya hapo, wataadhibiwa kulingana na mienendo yao mibovu. Mungu anaaminiwa na mwanadamu, na pia Anastahili utii wa mwanadamu. Wale wanaomwamini tu Mungu asiye yakini na asiyeonekana ni wale wasiomwamini Mungu; zaidi ya hapo, hawawezi kumtii Mungu. Kama hawa watu bado hawawezi kumwamini Mungu anayeonekana wakati kazi Yake ya ushindi inakamilika, na pia wanaendelea kutomtii na kumpinga Mungu anayeonekana katika mwili, hawa “wanaoamini isiyo yakini” bila shaka, wataangamizwa. Ni kama ilivyo na wale miongoni mwenu—yeyote anayemtambua Mungu Aliyepata mwili kwa maneno lakini bado hatendi ukweli wa utii kwa Mungu Aliyepata mwili hatimaye ataondolewa na kuangamizwa, na yeyote anayemtambua Mungu anayeonekana na pia kula na kunywa ukweli ulioonyeshwa na Mungu anayeonekana lakini bado anamtafuta Mungu asiye yakini na asiyeonekana pia yeye ataangamizwa baadaye. Hakuna hata mmoja wa watu hawa anayeweza kubaki hadi wakati wa pumziko baada ya kazi ya Mungu kukamilika; hakuwezi kuwa yeyote kama watu hawa atakayebakia hadi wakati wa pumziko. Watu wenye pepo ni wale wasiotenda ukweli; asili yao ni ile inayompinga na kutomtii Mungu, na hawana nia hata kidogo za kumtii Mungu. Watu wote kama hao wataangamizwa. Iwapo una ukweli na iwapo unampinga Mungu hayo yanaamuliwa kulingana na asili yako, si kulingana na sura yako ama hotuba na mwenendo wako wa mara kwa mara. Asili ya kila mtu inaamua iwapo ataangamizwa; hii inaamuliwa kulingana na asili iliyofichuliwa na mienendo yao na kutafuta kwao ukweli. Miongoni mwa watu wanaofanya kazi sawa na pia kufanya kiasi sawa cha kazi, wale ambao asili yao ni nzuri na wanaomiliki ukweli ni watu wanaoweza kubaki, lakini wale ambao asili yao ya ubinadamu ni mbovu na wasiomtii Mungu anayeonekana ni wale watakaoangamizwa. Kazi ama maneno yoyote ya Mungu yanayoelekezwa kwa hatima ya ubinadamu yanahusiana na ubinadamu ipasavyo kulingana na asili ya kila mtu; hakutakuwa na ajali yoyote, na hakika hakutakuwa na kosa hata kidogo. Mtu anapofanya kazi tu ndipo hisia za binadamu ama maana itachanganywa ndani. Kazi anayofanya Mungu ndiyo inayofaa zaidi; hakika Hataleta madai ya uongo dhidi ya kiumbe yeyote. Sasa kuna watu wengi wasioweza kutambua hatima ya baadaye ya ubinadamu na ambao pia hawaamini maneno Nisemayo; wote wasioamini, pamoja na wasiotenda ukweli, ni mapepo! Wanaotafuta na wasiotafuta sasa ni aina mbili tofauti ya watu, na wao ni aina mbili ya watu na hatima mbili tofauti. Wanaotafuta maarifa ya ukweli na kutenda ukweli ni watu ambao Mungu ataokoa. Wale wasiojua njia ya ukweli ni mapepo na adui; ni vizazi vya malaika mkuu na wataangamizwa. Hata wacha Mungu wanaomwamini Mungu asiye yakini—je, si mapepo pia? Watu wanaomiliki dhamiri nzuri lakini hawakubali njia ya ukweli ni mapepo; asili yao ni ile inayompinga Mungu. Wale wasiokubali njia ya ukweli ni wale wanaompinga Mungu, na hata kama watu hawa wanavumilia taabu nyingi, bado wataangamizwa. Wasio tayari kuiwacha dunia, wasioweza kuvumilia kutengana na wazazi wao, wasioweza kuvumilia kujiondolea raha zao za mwili, wote hawamtii Mungu na wote wataangamizwa. Yeyote asiyemwamini Mungu aliyepata mwili ni pepo; zaidi ya hayo, wataangamizwa. Wanaoamini lakini hawatendi ukweli, wasiomwamini Mungu aliyepata mwili, na wale ambao hawaamini kabisa kuwepo kwa Mungu wataangamizwa. Yeyote anayeweza kubaki ni mtu ambaye amepitia uchungu wa usafishaji na kusimama imara; huyu ni mtu ambaye kweli amepitia majaribio. Yeyote asiyemtambua Mungu ni adui; yaani, yeyote aliye ndani ama nje ya mkondo huu ambaye hamtambui Mungu aliyepata mwili ni adui wa Kristo! Shetani ni nani, mapepo ni nani, na nani ni maadui wa Mungu kama si wapinzani wasiomwamini Mungu? Wao si watu wasiomtii Mungu? Wao si watu wanaodai kwa maneno kuamini lakini hawana ukweli? Wao si wale watu wanaofuata tu kupata kwa baraka lakini hawawezi kumshuhudia Mungu? Bado unaweza kushiriki na wale mapepo leo na kusisitiza dhamiri na mapenzi na hawa mapepo; je, hii haichukuliwi kuwa kueneza nia nzuri kwa Shetani? Haichukuliwi kuwa kushiriki na mapepo? Kama watu bado hawawezi kutofautisha kati ya mazuri na maovu leo, na bado wanasisitiza kwa upofu mapenzi na huruma bila kwa njia yoyote kutamani kutafuta matakwa ya Mungu, na hawawezi kwa njia yoyote kuwa na moyo wa Mungu kama wao, mwisho wao utakuwa dhalili zaidi. Yeyote asiyemwamini Mungu wa mwili ni adui wa Mungu. Kama unaweza kusisitiza dhamiri na mapenzi kwa adui, je, hujakosa hisia ya haki? Kama unalingana na wale Ninaowachukia na kutokubaliana nao, na bado unasisitiza mapenzi na hisia za binafsi nao, basi wewe si asiyetii? Humpingi Mungu kimakusudi? Je, mtu kama huyu anamiliki ukweli? Ikiwa watu wanasisitiza dhamiri kwa adui, kusisitiza upendo kwa mapepo na kusisitiza huruma kwa Shetani, hawakatizi kazi ya Mungu kimakusudi? Wale watu wanaomwamini Yesu tu na hawamwamini Mungu aliyepata mwili wakati wa siku za mwisho na wale wanaodai kwa maneno kumwamini Mungu aliyepata mwili lakini wanafanya maovu wote ni adui wa Kristo, sembuse wale watu wasiomwamini Mungu. Hawa watu wote wataangamizwa. Kiwango ambacho mwanadamu anamhukumu mwanadamu kinatokana na tabia zake; aliye na mwenendo mzuri ni mtu mwenye haki, na aliye na mwenendo wa kuchukiza ni mwovu. Kiwango ambacho Mungu anamhukumu mwanadamu kinatokana na iwapo asili ya mtu inamtii Yeye; anayemtii Mungu ni mtu mwenye haki, na asiyemtii Mungu ni adui na mtu mwovu, bila kujali iwapo tabia ya mtu huyu ni nzuri ama mbaya, na bila kujali iwapo hotuba ya mtu huyu ni sahihi ama si sahihi. Watu wengine wanatamani kutumia matendo mazuri kupata hatima nzuri ya baadaye, na watu wengine wanataka kutumia hotuba nzuri kununua hatima nzuri. Watu wanaamini kimakosa kwamba Mungu anaamua matokeo ya mwanadamu kulingana na tabia ama hotuba yake, na kwa hivyo watu wengi watataka kutumia haya kupata fadhila ya muda mfupi kupitia udanyanyifu. Watu ambao baadaye watasalimika kupitia pumziko wote watakuwa wamevumilia siku ya dhiki na pia kumshuhudia Mungu; wote watakuwa watu ambao wamefanya jukumu lao na wana nia ya kumtii Mungu. Wanaotaka tu kutumia fursa ya kuhudumu ili kuepuka kutenda ukweli hawataweza kubaki. Mungu ana viwango sahihi vya mipangilio ya matokeo ya kila mtu; Hafanyi tu maamuzi haya kulingana na maneno na mwenendo wa mtu, wala Hayafanyi kulingana na tabia zao wakati wa kipindi kimoja cha muda. Hakika Hatakuwa na huruma na mwenendo wowote mbaya wa mtu kwa sababu ya huduma ya mtu ya zamani kwa Mungu, wala Hatamnusuru mtu kutokana na kifo kwa sababu ya gharama kwa Mungu ya mara moja. Hakuna anayeweza kuepuka adhabu ya uovu wake, na hakuna anayeweza kuficha tabia zake mbovu na hivyo kuepuka adhabu ya uangamizi. Kama mtu anaweza kweli kufanya jukumu lake, basi inamaanisha kwamba ni mwaminifu milele kwa Mungu na hatafuti tuzo, bila kujali iwapo anapokea baraka ama bahati mbaya. Kama watu wana uaminifu kwa Mungu waonapo baraka lakini wanapoteza uaminifu wao wasipoweza kuona baraka na mwishowe bado wasiweze kumshuhudia Mungu na bado wasiweze kufanya jukumu yao kama wapasavyo, hawa watu waliomhudumia Mungu wakati mmoja kwa uaminifu bado wataangamizwa. Kwa ufupi, watu waovu hawawezi kuishi milele, wala hawawezi kuingia rahani; watu wenye haki tu ndio mabwana wa pumziko. Baada ya ubinadamu kuingia katika njia sawa, watu watakuwa na maisha ya kawaida ya binadamu. Wote watafanya jukumu lao husika na kuwa waaminifu kabisa kwa Mungu. Watatoa kabisa kutotii kwao na tabia yao iliyopotoshwa, na wataishi kwa ajili ya Mungu na kwa sababu ya Mungu. Watakosa utotii na upinzani. Wataweza kabisa kumtii Mungu. Haya ndiyo maisha ya Mungu na mwanadamu na maisha ya ufalme, na ni maisha ya pumziko.
Wanaopeleka watoto na jamaa zao wasioamini kabisa kanisani ni wachoyo sana na wanaonyesha ukarimu wao. Watu hawa wanasisitiza tu upendo, bila kujali iwapo wanaamini ama iwapo ni matakwa ya Mungu. Wengine wanaleta wake zao mbele ya Mungu, ama kuleta wazazi wao mbele ya Mungu, na bila kujali iwapo Roho Mtakatifu anakubali ama anafanya kazi Yake, kwa upofu “wanawachukua watu wenye vipaji” kwa ajili ya Mungu. Kuna faida gani inayoweza kupatikana kutokana na kueneza ukarimu huu kwa watu hawa wasioamini? Hata kama hawa wasioamini wasio na uwepo wa Roho Mtakatifu wanapambana kumfuata Mungu, bado hawawezi kuokolewa kama mtu anavyodhani wanaweza. Wanaopokea wokovu kwa kweli si rahisi hivyo kuwapata. Wale ambao hawajapitia kazi ya Roho Mtakatifu na majaribio na hawajakamilishwa na Mungu aliyepata mwili hawawezi kukamilika kabisa. Kwa hivyo, watu hawa hawana uwepo wa Roho Mtakatifu kutoka wakati wanaanza kumfuata Mungu kwa jina. Kulingana na hali yao halisi, hawawezi tu kufanywa kamili. Hivyo, Roho Mtakatifu Haamui kutumia nguvu nyingi kwao, wala Hawapatii nuru yoyote ama kuwaongoza kwa njia yoyote; Anawaruhusu tu kufuata na hatimaye kufichua matokeo yao—haya yametosha. Shauku na nia za mwanadamu zinatoka kwa Shetani, na hakuna vile zinaweza kukamilisha kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali mtu ni mtu wa aina gani, mtu lazima awe na kazi ya Roho Mtakatifu—je, mtu anaweza kumkamilisha mtu? Mbona mume anampenda mke wake? Na mbona mke anampenda mume wake? Mbona watoto ni watiifu kwa wazazi wao? Na mbona wazazi wanawapenda sana watoto wao? Watu kweli wana nia za aina gani? Je, si kuweza kukidhi mipango na tamaa zao za ubinafsi? Kweli ni ya mpango wa usimamizi wa Mungu? Ni ya kazi ya Mungu? Ni ya kutimiza wajibu wa kiumbe? Waliomwamini Mungu kwanza na hawangepata uwepo wa Roho Mtakatifu hawawezi kupata kazi ya Roho Mtakatifu; imeamuliwa kwamba watu hawa wataangamizwa. Bila kujali kiasi cha upendo ambao mtu anao kwao, hauwezi kuchukua nafasi ya kazi ya Roho Mtakatifu. Shauku na upendo wa mwanadamu unawakilisha nia za mwanadamu, lakini haviwezi kuwakilisha nia za Mungu na haviwezi kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu. Hata mtu akieneza kiasi kikubwa zaidi cha upendo ama huruma kwa hao watu wanaomwamini Mungu kwa jina na kujifanya kumfuata Yeye lakini hawajui ni nini maana ya kumwamini Mungu, bado hawatapata huruma ya Mungu ama kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Hata kama watu wanaomfuata Mungu kwa dhati ni wenye akili ndogo na hawawezi kuelewa kweli nyingi, bado wanaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu mara kwa mara, lakini wale walio wa akili nzuri kidogo, lakini hawaamini kwa dhati hawawezi kabisa kupata uwepo wa Roho Mtakatifu. Hakuna kabisa uwezekano wowote wa wokovu na watu hawa. Hata wakisoma na kusikiza ujumbe mara kwa mara ama kuimba sifa kwa Mungu, mwishowe hawataweza kubaki mpaka wakati wa pumziko. Iwapo mtu anatafuta kwa dhati hakuamuliwi na jinsi wengine wanamhukumu ama jinsi wengine karibu wanamwona, lakini kunaamuliwa na iwapo Roho Mtakatifu anamfanyia kazi na iwapo ana uwepo wa Roho Mtakatifu, na kunaamuliwa zaidi na iwapo tabia yake inabadilika na iwapo ana maarifa ya Mungu baada ya kupitia kazi ya Roho Mtakatifu kwa muda fulani; ikiwa Roho Mtakatifu anamfanyia mtu kazi, tabia ya mtu huyu itabadilika polepole, na mtazamo wake wa kumwamini Mungu utakua safi polepole. Bila kujali muda gani mtu anamfuata Mungu, kama wamebadilika, hii inamaanisha kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kwake. Kama hawajabadilika, inamaanisha kwamba Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwake. Hata kama hawa watu wanatoa huduma fulani, wanachochewa na nia zao za kupata bahati nzuri. Huduma ya mara kwa mara haiwezi kuchukua nafasi ya mabadiliko katika tabia yao. Hatimaye, bado wataangamizwa, kwani hakuna haja ya wale wanaotoa Huduma ndani ya ufalme, wala hakuna haja ya yeyote ambaye tabia yake haijabadilika kuwahudumia wale watu ambao wamekamilishwa na walio waaminifu kwa Mungu. Hayo maneno kutoka zamani, “Wakati mtu anamwamini Bwana, bahati inatabasamu kwa familia yake nzima,” yanafaa kwa Enzi ya Neema lakini hayana uhusiano na hatima ya mwanadamu. Yalifaa tu kwa hatua ya wakati wa Enzi ya Neema. Maana iliyokusudiwa ya maneno haya inaelekezwa kwa amani na baraka yakinifu ambazo watu wanafurahia; hayamaanishi kwamba familia nzima ya anayemwamini Bwana itaokolewa, wala hayamaanishi kwamba wakati mtu anapata bahati nzuri, familia yake nzima pia itaingia rahani. Iwapo mtu anapokea baraka ama kupata bahati mbaya inaamuliwa kulingana na kiini cha mtu, na haiamuliwi kulingana na asili ya kawaida ambayo mtu anashiriki na wengine. Ufalme hauna kabisa usemi kama huu ama kanuni kama hii. Kama mtu anaweza kusalimika hatimaye, ni kwa sababu amefikia mahitaji ya Mungu, na kama mtu hawezi hatimaye kubaki mpaka kipindi cha pumziko, ni kwa sababu mtu huyu hamtii Mungu na hajakidhi mahitaji ya Mungu. Kila mtu ana hatima inayofaa. Hatima hizi zinaamuliwa kulingana na asili ya kila mtu na hazihusiani kabisa. Mwenendo ovu wa mtoto hauwezi kuhamishwa kwa wazazi wake, na haki ya mtoto hauwezi kushirikishwa wazazi wake. Mwenendo ovu wa mzazi huwezi kuhamishwa kwa watoto wake, na haki ya mzazi hiwezi kushirikishwa watoto wake. Kila mtu anabeba dhambi zake husika, na kila mtu anafurahia bahati yake husika. Hakuna anayeweza kuchukua ya mwengine. Hii ni haki. Kwa mtazamo wa mwanadamu, iwapo wazazi wanapata bahati nzuri, watoto wao pia wanaweza, na watoto wakifanya maovu, wazazi wao lazima walipie dhambi zao. Huu ni mtazamo wa mwanadamu na njia ya mwanadamu ya kufanya vitu. Si mtazamo wa Mungu. Matokeo ya kila mtu yanaamuliwa kulingana na asili inayotoka kwa mwenendo wao, na daima yanaamuliwa inavyofaa. Hakuna awezaye kubeba dhambi za mwengine; hata zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kupokea adhabu badala ya mwengine. Hii ni thabiti. Malezi ya upendo ya mzazi kwa watoto wake hayamaanishi kwamba anaweza kufanya matendo ya haki badala ya watoto wake, wala upendo wenye utiifu wa mtoto kwa wazazi wake haumaanishi kwamba anaweza kufanya matendo ya haki badala ya wazazi wake. Hiyo ndiyo maana ya kweli ya maneno haya, “Basi kutakuwa na watu wawili kondeni; mmoja wao atatwaliwa, na mmoja ataachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga katika kisiagi; mmoja atatwaliwa, na mmoja ataachwa.” Hakuna anayeweza kuwaingiza watoto wake watenda maovu rahani kwa msingi wa upendo wao wa kina kwa watoto wao, wala hakuna anayeweza kumwingiza mke wake (ama mume) rahani kwa sababu ya mwenendo wao wa haki. Hii ni kanuni ya utawala; hakuwezi kuwa na ubaguzi kwa mtu yeyote. Wanaotenda haki ni wanaotenda haki, na watenda maovu ni watenda maovu. Watenda haki watasalimika, na watenda maovu wataangamizwa. Watakatifu ni watakatifu; wao si wachafu. Wachafu ni wachafu, na hawana sehemu yoyote takatifu. Watu wote waovu wataangamizwa, na watu wote wa haki watasalimika, hata kama watoto wa watenda maovu wanafanya matendo ya haki, na hata kama wazazi wa mtu wa haki wanafanya matendo ya haki. Hakuna uhusiano kati ya mume anayeamini na mke asiyeamini, na hakuna uhusiano kati ya watoto wanaoamini na wazazi wasioamini. Ni aina mbili zisisolingana. Kabla ya kuingia rahani, mtu ana jamaa wa kimwili, lakini baada ya mtu kuingia rahani, mtu hana jamaa wa kimwili tena wa kuzungumzia. Wanaofanya wajibu wao na wasiofanya ni adui, wanaompenda Mungu na wanaomchukia Mungu ni wapinzani. Wanaoingia rahani na wale ambao wameangamizwa ni aina mbili ya viumbe visivyolingana. Viumbe wanaotimiza wajibu wao watasalimika, na viumbe wasiotimiza wajibu wao wataangamizwa; zaidi ya hayo, hii itadumu milele. Je, unampenda mume wako ili kutimiza wajibu wako kama kiumbe? Je, unampenda mke wako ili kutimiza wajibu wako kama kiumbe? Je, wewe ni mtiifu kwa wazazi wako wasioamini ili kutimiza wajibu wako kama kiumbe? Mtazamo wa mwanadamu wa kumwamini Mungu ni sahihi ama la? Mbona unamwamini Mungu? Unataka kupata nini? Unampenda Mungu jinsi gani? Wasioweza kutimiza wajibu wao kama viumbe na hawawezi kufanya juhudi nzima wataangamizwa. Watu leo wana mahusiano ya kimwili miongoni mwao, na pia ushirikiano wa damu, lakini baadaye hii yote itavunjwa. Waumini na wasioamini hawalingani ila wanapingana. Walio rahani wanaamini kwamba kuna Mungu na wanamtii Mungu. Wasiomtii Mungu wote watakuwa wameangamizwa. Familia hazitakuwa tena duniani; kunawezaje kuwa na wazazi na watoto ama mahusiano kati ya waume na wake? Kutoambatana kati ya imani na kutoamini kutakuwa kumevunja haya mahusiano ya kimwili!
Awali hakukuwa na familia miongoni mwa ubinadamu, ila mwanamume na mwanamke tu, watu wa aina mbili. Hakukuwa na nchi, sembuse familia, lakini kwa sababu ya upotovu wa mwanadamu, watu wa aina yote walijipanga katika koo binafsi, baadaye kukua kwa nchi na mataifa. Nchi na mataifa haya yalikuwa na familia ndogo binafsi, na kwa namna hii watu wa aina yote walisambazwa miongoni mwa jamii mbalimbali kulingana na tofauti ya lugha na mipaka igawayo. Kwa kweli, bila kujali idadi ya jamii zilizo duniani, ubinadamu una babu mmoja pekee. Mwanzoni, kulikuwa na watu wa aina mbili tu, na aina hizi mbili zilikuwa mwanamume na mwanamke. Hata hivyo, kwa sababu ya maendeleo ya kazi ya Mungu, kupita kwa historia na mabadiliko ya kijiografia, kwa viwango mbalimbali aina hizi mbili za watu ziliendelezwa kuwa watu wa aina nyingine zaidi. Mwishowe, bila kujali idadi ya jamii zilizo katika ubinadamu, ubinadamu wote bado ni viumbe wa Mungu. Bila kujali ambayo watu wako ndani, wote ni viumbe Wake; wote ni vizazi vya Adamu na Hawa. Hata kama hawajatengenezwa na mikono ya Mungu, ni vizazi vya Adamu na Hawa, ambao Mungu Mwenyewe aliumba. Bila kujali aina ambayo watu wako ndani, wote ni viumbe Wake; kwa sababu ni wa ubinadamu, ambao uliumbwa na Mungu, hatima yao ni hiyo ambayo ubinadamu unapaswa kuwa nayo, na wamegawanywa kulingana na kanuni zinazopanga ubinadamu. Hiyo ni kusema kwamba, watenda maovu na wenye haki, hata hivyo, ni viumbe. Viumbe wafanyao maovu wataangamizwa hatimaye, na viumbe wafanyao matendo ya haki watasalimika. Huu ni mpangilio unaofaa sana wa viumbe wa aina hizi mbili. Watenda maovu hawawezi, kwa sababu ya kutotii kwao, kukataa kwamba ni viumbe wa Mungu lakini wameporwa na Shetani na hivyo hawawezi kuokolewa. Viumbe wa mwenendo wa haki hawawezi kutegemea ukweli kwamba watasalimika kukataa kwamba wameumbwa na Mungu na bado wamepokea wokovu baada ya kupotoshwa na Shetani. Watenda maovu ni viumbe wasiomtii Mungu; ni viumbe ambao hawawezi kuokolewa na tayari wameporwa na Shetani. Watu wanaotenda maovu ni watu pia; ni watu waliopotoshwa mno na watu wasioweza kuokolewa. Jinsi walivyo viumbe pia, watu wa mwenendo wa haki pia wamepotoshwa, lakini ni watu walio tayari kuacha tabia yao potovu na wanaweza kumtii Mungu. Watu wa mwenendo wa haki hawajajaa haki; badala yake, wamepokea wokovu na kuacha tabia yao potovu kumtii Mungu; watashikilia msimamo huo mwishowe, lakini hii si kusema kwamba hawajapotoshwa na Shetani. Baada ya kazi ya Mungu kuisha, miongoni mwa viumbe Wake wote, kutakuwa na wale watakaoangamizwa na wale watakaosalimika. Huu ni mwelekeo usioepukika wa kazi Yake ya usimamizi. Hakuna anayeweza kuyakataa haya. Watenda maovu hawawezi kusalimika; wanaomtii na kumfuata Mungu hadi mwishowe hakika watasalimika. Kwa sababu kazi hii ni ya usimamizi wa ubinadamu, kutakuwa na wale watakaobaki na wale watakaoondolewa. Haya ni matokeo tofauti ya watu wa aina tofauti, na hii ndiyo mipango inayofaa zaidi ya viumbe Wake. Mpango wa mwisho wa Mungu kwa mwanadamu ni kugawa kwa kuzivunja familia, kuyavunja mataifa na kuivunja mipaka ya kitaifa. Ni moja isiyo na familia na mipaka ya kitaifa, kwani mwanadanu, hata hivyo, ni wa babu mmoja na ni kiumbe wa Mungu. Kwa ufupi, viumbe wafanyao maovu wataangamizwa, na viumbe wanaomtii Mungu watasalimika. Kwa njia hii, hakutakuwa na familia, hakutakuwa na nchi na hasa hakutakuwa na mataifa katika pumziko la baadaye; ubinadamu wa aina hii ni aina takatifu kabisa ya ubinadamu. Adamu na Hawa waliumbwa awali ili mwanadamu aweze kutunza mambo yote duniani; mwanadamu awali alikuwa bwana wa vitu vyote. Nia ya Yehova ya kumuumba mwanadamu ilikuwa kumruhusu mwanadamu kuwa duniani na pia kutunza vitu vyote duniani, kwani mwanadamu awali hakuwa amepotoshwa na pia hakuweza kutenda maovu. Hata hivyo, baada ya mwanadamu kupotoshwa, hakuwa mtunzaji wa vitu vyote tena, na madhumuni ya wokovu wa Mungu ni kurejesha kazi hii ya mwanadamu, kurejesha ufahamu wa awali wa mwanadamu na utii wake wa awali; ubinadamu rahani utakuwa picha halisi ya matokeo ambayo kazi ya Mungu ya wokovu inatarajia kufikia. Ingawa hayatakuwa tena maisha kama yale ya bustani ya Edeni, kiini chake kitakuwa sawa; ubinadamu hautakuwa tu nafsi yake ya awali isiyo potovu, lakini badala yake ubinadamu uliopotoshwa na kisha kupata wokovu. Watu hawa waliopata wokovu hatimaye (yaani, baada ya kazi Yake kuisha) wataingia rahani. Vivyo hivyo, matokeo ya wale walioadhibiwa pia yote yatafichuliwa mwishowe, na wataangamizwa tu baada ya kazi Yake kuisha. Hii ni kusema kwamba baada ya kazi Yake kuisha, watendao maovu na wale waliookolewa wote watafichuliwa, kwani kazi ya kufichua watu wa aina zote (bila kujali iwapo ni watenda maovu ama waliookolewa) itatekelezwa kwa watu wote wakati huo huo. Watenda maovu wataondolewa, na wale wanaoweza kubaki watafichuliwa wakati huo huo. Kwa hivyo, matokeo ya watu wa aina zote yatafichuliwa wakati huo huo. Hataliruhusu kwanza kundi la watu waliookolewa kuingia rahani kabla ya kuweka kando watenda maovu na kuwahukumu au kuwaadhibu kidogo kidogo; ukweli kwa kweli si hivyo. Wakati watenda maovu wanaangamizwa na waliosalimika wanaingia rahani, kazi Yake katika ulimwengu mzima itakuwa imemalizika. Hakutakuwa na utaratibu wa kipaumbele miongoni mwa wale wanaopata baraka na wale wanaopata taabu; wanaopokea baraka wataishi milele, na wanaopata taabu wataangamia milele. Hizi hatua mbili za kazi zitakamilika wakati huo huo. Ni hasa kwa sababu kuna watu wasiotii ndiyo maana haki ya watu wanaotii itafichuliwa, na ni hasa kwa sababu kuna wale waliopokea baraka ndiyo maana taabu ya wale wanaotenda maovu kwa sababu ya mwenendo wao mbovu itafichuliwa. Kama Mungu hakufichua watenda maovu, hao watu wanaomtii Mungu kwa dhati hawangeona jua; kama Mungu hangewapelekea wanaomtii katika hatima inayofaa, wasiomtii Mungu hawangeweza kupata adhabu wanayostahili. Huu ndio mwendo wa kazi Yake. Kama hangefanya kazi hii ya kuadhibu maovu na kutuza mazuri, viumbe Wake hawangeweza kuingia hatima zao husika. Mwanadamu aingiapo rahani, watenda maovu wataangamizwa, ubinadamu wote utaingia katika njia sahihi, na watu wa kila aina watakuwa na aina yao kulingana na kazi wanayopaswa kufanya. Hii tu ndiyo itakuwa siku ya ubinadamu kupumzika na mwenendo usioepukika wa maendeleo ya ubinadamu, na wakati tu ubinadamu utaingia rahani ndipo utimilifu mkubwa na wa mwisho wa Mungu utamalizika; hii itakuwa tamati ya kazi Yake. Hii kazi itamaliza maisha ya uharibifu ya kimwili ya ubinadamu, na itamaliza maisha ya ubinadamu potovu. Kutoka hapa ubinadamu utaingia katika ulimwengu mpya. Ingawa mwanadamu anaishi kimwili, kuna tofauti kubwa kati ya kiini cha maisha yake na kiini cha maisha ya ubinadamu potovu. Maana ya kuwepo kwake na maana ya kuwepo kwa ubinadamu potovu pia ni tofauti. Ingawa haya si maisha ya mtu wa aina mpya, inaweza kusemwa kuwa maisha ya ubinadamu ambao umepata wokovu na maisha yenye ubinadamu na busara kurejeshwa. Hawa ni watu ambao hawakumtii Mungu wakati mmoja, na ambao walishindwa na Mungu wakati mmoja na baadaye kuokolewa na Yeye; hawa ni watu waliomwaibisha Mungu na baadaye wakamshuhudia. Uwepo wao, baada ya kupitia na kuendelea kuishi baada ya jaribio Lake, ni uwepo wa maana kubwa zaidi; ni watu waliomshuhudia Mungu mbele ya Shetani; ni watu wanaofaa kuishi. Watakaoangamizwa ni watu wasioweza kumshuhudia Mungu na hawafai kuishi. Uangamizi wao utakuwa kwa sababu ya mwenendo wao mwovu, na uangamizi ni hatima yao bora zaidi. Mwanadamu aingiapo baadaye katika ulimwengu mzuri, hakutakuwa na mahusiano kati ya mume na mke, kati ya baba na binti ama kati ya mama na mwana wa kiume ambayo mwanadamu anafikiria atapata. Wakati huo, mwanadamu atafuata aina yake, na familia itakuwa tayari imevunjwa. Baada ya kushindwa kabisa, Shetani hatausumbua ubinadamu tena, na mwanadamu hatakuwa tena na tabia potovu ya kishetani. Wale watu wasiotii watakuwa wameangamizwa tayari, na wale watu wanaotii pekee ndio wataishi. Na basi familia chache sana zitasalimika bila kuharibika; mahusiano ya kimwili yatawezaje kuweko? Maisha ya kimwili ya zamani ya mwanadamu yatapigwa marufuku kabisa; mahusiano ya kimwili yatawezaje kuweko kati ya watu? Bila tabia potovu ya kishetani, maisha ya watu hayatakuwa tena maisha ya zamani ya siku zilizopita, lakini badala yake maisha mapya. Wazazi watapoteza watoto, na watoto watapoteza wazazi. Waume watapoteza wake, na wake watapoteza waume. Watu sasa wana mahusiano ya kimwili miongoni mwao. Wakati wote watakuwa wameingia rahani hakutakuwa na mahusiano ya kimwili tena. Ubinadamu kama huo tu ndio utakuwa wa haki na mtakatifu, ubinadamu kama huo tu ndio utamwabudu Mungu.
Mungu aliumba ubinadamu, Akawaweka duniani na kuwaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa ubinadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa ubinadamu. Mwishowe lazima bado ashinde ubinadamu, aokoe ubinadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali. Ataanzisha ufalme Wake na kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu, kumaanisha kwamba Atarejesha mamlaka Yake duniani na kurejesha mamlaka Yake miongoni mwa viumbe vyote, Mwanadamu alipoteza moyo wake wa kumcha Mungu baada ya kupotoshwa na Shetani na kupoteza kazi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kuwa nayo, kuwa adui asiyemtii Mungu. Mwanadamu alimilikiwa na Shetani na kufuata amri za Shetani; hivyo Mungu hakuwa na njia ya kufanya kazi miongoni mwa viumbe Wake, na hakuweza zaidi kuwafanya viumbe Wake kumcha. Mwanadamu aliumbwa na Mungu, na anapaswa kumwabudu Mungu, lakini mwanadamu kwa kweli alimpuuza Mungu na kumwabudu Shetani. Shetani alikuwa sanamu katika moyo wa mwanadamu. Hivyo Mungu alipoteza nafasi yake katika moyo wa mwanadamu, kusema kwamba Alipoteza maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu, na ili kurejesha maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu lazima arejeshe mfano wa awali wa mwanadamu na kumtoa mwanadamu tabia yake potovu. Ili kumrejesha mwanadamu kutoka kwa Shetani, lazima Amwokoe mwanadamu kutoka kwa dhambi. Kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu polepole na kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, na mwishowe kurejesha ufalme Wake. Uangamizi wa mwisho wa wale wana wa kutotii pia utafanywa ili kumruhusu mwanadamu kumwabudu Mungu vizuri zaidi na kuishi duniani vizuri zaidi. Kwa sababu Mungu alimuumba mwanadamu, Atamfanya mwanadamu amwabudu; kwa sababu Anataka kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, Atairejesha kabisa, na bila ughushi wowote. Kurudisha mamlaka Yake kunamaanisha kumfanya mwanadamu amwabudu na kumfanya mwanadamu amtii; kunamaanisha kwamba Atamfanya mwanadamu aishi kwa sababu Yake na kufanya adui zake waangamie kwa sababu ya mamlaka Yake; kunamaanisha kwamba Atafanya kila sehemu Yake kuendelea miongoni mwa ubinadamu na bila upinzani wowote wa mwanadamu. Ufalme Anaotaka kuanzisha ni ufalme Wake Mwenyewe. Ubinadamu Anaotaka ni ule unaomwabudu, ule unaomtii kabisa na una utukufu Wake. Asipookoa ubinadamu potovu, maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu hautakuwa chochote; Hatakuwa na mamlaka yoyote miongoni mwa mwanadamu, na ufalme Wake hautaweza kuweko tena duniani. Asipoangamiza wale adui wasiomtii, Hataweza kupata utukufu Wake wote, wala Hataweza kuanzisha ufalme Wake duniani. Hizi ndizo ishara za ukamilishaji wa kazi Yake na ishara za ukamilishaji wa utimilifu Wake mkubwa; kuangamiza kabisa wale miongoni mwa ubinadamu wasiomtii, na kuwaleta wale waliokamilika rahani. Wakati ubinadamu umerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati ubinadamu unaweza kutimiza kazi yake husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea ubinadamu utaingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani utatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.
Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu ndiye ujio wa pili wa Bwana Yesu. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi usome maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana! Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli kuja hapa na kutazama.
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu
Kwa nini unamwamini Mungu ? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa...
-
Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mw...
-
Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ...
-
Biblia pia huitwa Agano la Kale na Agano Jipya. Je, wajua “agano” linarejelea nini? “Agano” katika “Agano Jipya” linatokana na makubalia...























