Biblia pia huitwa
Agano la Kale na Agano Jipya. Je, wajua “agano” linarejelea nini? “Agano”
katika “Agano Jipya” linatokana na makubaliano ya Yehova na watu wa Israeli
Alipowaua Wamisri na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Farao. Bila Shaka,
uthibitisho wa haya makubaliano ulikuwa damu ya mwanakondoo iliyopakwa kwenye
linta kupitia kwayo Mungu Alianzisha agano na mwanadamu, moja ambalo ilisemwa
kuwa wale wote waliokuwa na damu ya mwanakondoo juu na pembeni mwa viunzi vya
mlango walikuwa Waisraeli, walikuwa wateuliwa wa Mungu, na wote wangeokolewa na
Yehova (kwa kuwa Yehova wakati ule Alikuwa karibu kuwaua wazaliwa wa kwanza wa
kiume wa Misri wote na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe).
Agano hili lina viwango viwili vya maana. Hakuna mmoja wa watu au wanyama wa Misri angeokolewa naYehova; Angewaua wazaliwa wa kwanza wa kiume na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe wao wote. Kwa hivyo, katika vitabu vingi vya unabii kulitabiriwa kwamba Wamisri wangeadibiwa vikali kutokana na agano la Yehova. Hiki ndicho kiwango cha kwanza cha maana. Yehova Aliwaua wazaliwa wa kwanza wa kiume wa Misri na wazaliwa wa kwanza wa mifugo wao wote, na kuwaacha Waisraeli wote, jambo lililomaanisha kuwa wale wote waliokuwa wa nchi ya Israeli walipendwa na Yehova na wote wangeokolewa; Alidhamiria kufanya kazi ya muda mrefu ndani yao, na Alianzisha agano nao kwa kutumia damu ya mwanakondoo. Tangu wakati ule kuendelea, Yehova Asingewaua Waisraeli na Alisema kuwa daima wangekuwa wateuliwa Wake. Angeianza kazi Yake ya Enzi Nzima ya Sheria Miongoni mwa makabila kumi na mawili ya Israeli, Angeziweka wazi sheria Zake zote kwa Waisraeli, na kuchagua manabii na waamuzi kutoka kati yao, na wangekuwa katikati ya kazi Yake. Alifanya Agano nao: Angefanya kazi tu miongoni mwa wateuliwa isipokuwa enzi ibadilike. Agano la Yehova lilikuwa lisilobadilika kwani lilitengenezwa kwa damu, na lilianzishwa na wateuliwa Wake. La muhimu zaidi, Alikuwa Ameteua mawanda na malengo yafaayo ya kazi Yake katika enzi nzima, na kwa hivyo watu waliliona agano kuwa la umuhimu sana. Hiki ndicho kiwango cha pili cha maana ya agano. Isipokuwa kitabu cha Mwanzo, ambacho kilikuwepo kabla ya kuanzishwa kwa agano, vitabu vingine vyote vya Agano la Kale vinaeleza kuhusu kazi miongoni mwa Waisraeli baada ya kuanzishwa kwa agano hili. Bila shaka, yapo maelezo ya hapa na pale ya Watu wa Mataifa, ila kwa ujumla, Agano la Kale linaeleza kuhusu kazi ya Mungu nchini Israeli. Kwa sababu ya Agano kati ya Yehova na Waisraeli, vitabu vilivyoandikwa katika Enzi ya Sheria vinaitwa “Agano la Kale.” Vimepatiwa jina hili kutokana na agano la Yehova na Waisraeli.

Agano Jipya
lilipatiwa jina hilo kutokana na damu iliyomwagwa na Yesu msalabani na agano
Lake na wale wote waliomwamini. Agano la Yesu lilikuwa hili: Watu hawakuwa na
budi kumwamini ili dhambi zao zisamehewe kwa kumwagika kwa damu Yake, na kwa
njia hiyo wangeokolewa na kuzaliwa upya kupitia Kwake, na kamwe wasingeendelea
kuwa wenye dhambi; watu walipaswa kumwamini ili wapokee neema Yake, na
hawangeteseka jehanamu baada ya kufa. Vitabu vyote vilivyoandkwa wakati wa Enzi
ya Neema vilizuka baada ya hili agano, na vyote vinaeleza kuhusu kazi na
matamshi yaliyomo. Havielezi zaidi ya wokovu wa kusulubishwa kwa Bwana Yesu au
hili agano; vyote ni vitabu vilivyoandikwa na wapendwa katika Bwana waliokuwa
na tajriba. Kwa hivyo hivi vitabu vilevile vimepatiwa jina kutokana na agano:
Vinaitwa “Agano Jipya.” Haya “Maagano” mawili yanajumuisha tu Enzi ya Neema na
Enzi ya Sheria na hayana uhusiano na enzi ya mwisho. Hivyo basi, Biblia haina
msaada mkubwa kwa watu wa leo wa siku za mwisho. Zaidi, hutumika kama marejeleo
ya muda mfupi, ila kimsingi haina matumizi ya thamani kubwa. Ila watu wa dini
bado wanaienzi kuliko kitu kingine chochote. Hawaijui Biblia; wanajua tu jinsi
ya kuieleza Biblia na kimsingi hawajui asili yake. Mtazamo wao kuhusu Biblia
ni: Kila kitu katika Biblia ni sahihi, haina upungufu au makosa. Baada ya hapo
wao huanza kuichunguza. Kwa sababu kwanza wameshakubali kwamba Biblia iko
sahihi, bila makosa, wanaichunguza na kuitathimini kwa shauku kubwa. Hatua ya
leo ya kazi haikutabiriwa kwa Biblia. Hakukutajwa kazi ya ushindi katika sehemu
za giza zaidi, kwani hii ni kazi mpya zaidi. Kwa sababu enzi ya kazi ni
tofauti, hata Yesu Mwenyewe hakufahamu kuwa hatua hii ya kazi ingefanywa katika
siku za mwisho—basi, watu wa siku za mwisho wangetathimini vipi kuigundua hii
hatua ya kazi?
Wengi wa wale
wanaoeleza Biblia wanatumia mitazamo ya kimantiki na hawana usuli wa uhalisia.
Wanatumia mantiki tu kivielewa vitu vingi. Kwa miaka na miaka, hakuna
aliyethubutu kuichanganua Biblia, au kusema “hapana” kwa Biblia, kwa sababu
kitabu hiki ni “kitabu kitakatifu,” na watu wanakiabudu kama Mungu. Hili
limeendelea kwa maelfu kadhaa ya miaka. Mungu hajashughulishwa na hakuna
aliyegundua maelezo wa ndani kuhusu Biblia. Tunasema kwamba kuithamini sana
Biblia ni kuabudu miungu, na bado hakuna kati ya hawa waumini anayethubutu
kuyaona mambo kwa njia hii, na watakwambia: “Ndugu! Usiseme hivyo, ni vibaya!
Wawezaje kumkufuru Mungu?” Baadaye watakuwa na hisia za uchungu: “Lo, Yesu wa
huruma, Bwana wa wokovu, nakuomba umsamehe dhambi zake kwa kuwa Wewe ni Bwana
Ampendaye mwanadamu, nasi sote tumekosa, tafadhali tuonee huruma kubwa, amina.”
Umeona jinsi walivyo wacha Mungu; ingekuwaje rahisi kwa wao kuukubali ukweli?
Msomo wako ambao utawaogopesha kipumbavu. Hakuna ambaye angethubutu kufikiri
kuwa Biblia ingeweza kupakwa doa na mawazo ya binadamu na dhana za binadamu, na
hakuna awezaye kuiona hii dosari. Baadhi ya mambo katika Biblia ni uzoefu na
ufahamu wa wanadamu, baadhi ni kupatiwa nuru ya Roho Mtakatifu, na pia kuna
unajisi wa akili na fikra za wanadamu. Mungu hajawahi kuingilia mambo haya lakini
kuna kikomo: Hayawezi kuzidi fikra ya kawaida ya watu, na yakipita, yatakuwa
yakiingilia na kuitatiza kazi ya Mungu. Kile kinachozidi fikra za kawaida za
watu ni kazi ya Shetani, kwa kuwa kinatoa watu wajibu wao, ni kazi ya Shetani,
na kuelekezwa na Shetani, na katika kipindi hiki Roho Mtakatifu Hatakuruhusu
kutenda mambo kwa njia hiyo. Wakati mwingine ndugu na dada huuliza: “Ni sawa
nikitenda mambo kwa namna hii na ile?” Mimi hutazama kimo chao na kusema:
“Sawa!” Vilevile kunao watu ambao husema: “Nikitenda namna hii na ile, je, hali
yangu ni ya kawaida?” Nami hujibu: “Ndiyo, ni ya kawaida, kawaida haswa!”
Wengine husema: “Je, ni sawa nikifanya hivi?” Nami husema: “Hapana!” Wao
husema: “Ni kwa nini ni sawa kwake na si sawa kwangu?” Nami husema: “Kwa sababu
unachokifanya kinatoka kwa Shetani, kinasumbua, na chanzo cha motisha yako ni
uasi.” Huwepo pia wakati ambapo kazi haijasonga kadiri inavyotakiwa na ndugu na
dada hawatambui. Wengine huniuliza kama ni sawa kufanya kazi namna ile, na
Nionapo kuwa matendo yao hayatatatiza kazi ya siku za usoni, Mimi husema: “Ni
sawa.” Kazi ya Roho Mtakatifu huwapa watu upeo; watu hawalazimiki kufuata
mapenzi ya Roho Mtakatifu hadi nukta ya mwisho, kwani watu wana fikra ya
kawaida na udhaifu, na wana mahitaji ya kimwili, wana matatizo halisi, na
katika bongo zao kuna mawazo ambayo kimsingi hawana njia za kuyadhibiti. Kila
Ninachohitaji kutoka kwa wanadamu kina mipaka. Wengine huamini kuwa maneno
Yangu yana utata, kwamba Nawaambia kutenda mambo kwa njia yoyote ile—hii ni kwa
sababu hamfahamu kuwa kuna upeo ufaao katika mahitaji Yangu. Ingekuwa
mnavyodhani—Ningekuwa na mahitaji sawa kwa kila mtu bila kighairi, na
kuwahitaji wafikie kimo sawa—basi hili lisingefanyika. Huku ni kuuliza
lisilowezekana, na ni kanuni ya kazi ya mwanadamu, si kanuni ya kazi ya Mungu.
Kazi ya Mungu huendeshwa kulingana na hali halisi ya wanadamu, na imekitwa
katika ubora wao asilia. Hii vilevile ni kanuni ya kueneza injili: Ni lazima
uifanye taratibu, na kuruhusu hali asilia kuchukua mkondo wake hadi wakati
utakapomwambia mtu ukweli wazi wazi. Ni hapo ndipo watakapoelewa, na ni wakati
huo tu ndipo wataweza kuiweka kando Biblia. Ikiwa Mungu Asingefanya hatua hii
ya kazi, ni nani angeweza kuyavunja desturi? Ni nani angeweza kuifanya kazi
mpya? Ni nani angeweza kutafuta njia mpya nje ya Biblia? Kwa sababu dhana za
jadi ya watu na maadili ya kijamii ni maudhi, hawana uwezo wa kuviacha hivi
vitu wao wenyewe, wala hawana ujasiri wa kufanya hivyo. Hapo ni bila kutaja
namna watu wa leo wametekwa na maneno machache yaliyokufa katika Biblia, maneno
ambayo yameimiliki mioyo yao. Watakuwaje radhi kuiacha Biblia? Watawezaje
kukubali kwa urahisi njia iliyo nje ya Biblia? Hilo haliwezekani pasipo na wewe
kuzungumza wazi kuhusu simulizi ya ndani ya Biblia na kanuni za kazi ya Roho
Mtakatifu, ili watu wote washawishiwe kabisa—ambalo ni la haja kubwa. Hii ni
kwa sababu kila aliye ndani ya dini anaiheshimu Biblia na kuiabudu kama Mungu,
vilevile wanajaribu kumfunga Mungu katika mipaka ya Biblia, na ndivyo hutimiza
madhumuni yao punde tu wanapomuangika Mungu msalabani kwa mara nyingine.
Umeme waMashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na
kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho.
Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku
za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa
kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa
hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu
husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa
Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni