Sio kila kitu katika Biblia ni rekodi ya
maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za
kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na
sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu
katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya
kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana
nyingi za kibinadamu, upendelevu wa kibinadamu, na ufasiri wa ajabu wa
kibinadamu. Ni kweli, maneno mengi ni matokeo ya kupatiwa nuru na kuangaziwa na
Roho Mtakatifu, na ni tafsiri sahihi—lakini haiwezi kusemwa kuwa ni
udhihirishaji sahahi kabisa wa ukweli. Maoni yao juu ya vitu fulani si chochote
zaidi ya maarifa uzoefu binafsi, au kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Utabiri wa
manabii ulikuwa umetolewa na Mungu mwenyewe: Unabii wa Isaya, Danieli, Ezra,
Yeremia, na Ezekieli, ulitoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu, watu hawa
walikuwa ni waonaji maono, walipokea Roho ya Unabii, wote walikuwa ni manabii
wa Agano la Kale. Wakati wa Enzi ya Sheria watu hawa, ambao walikuwa wamepokea
ufunuo wa Yehova, walizungumza unabii mwingi, ambao ulisemwa na Yehova moja kwa
moja. Na kwa nini Yehova alifanya kazi ndani yao? Kwa sababu watu wa Israeli
walikuwa ni wateule wa Mungu: Kazi ya manabii ilipaswa kufanyika miongoni mwao,
na walikuwa wamefuzu kupokea maono hayo. Kimsingi, wao wenyewe hawakuelewa
ufunuo wa Mungu kwao. Roho Mtakatifu Alizungumza maneno hayo kupitia vinywa
vyao ili watu wa baadaye waweze kuelewa mambo hayo, na kuona kwamba ni kweli
ilikuwa ni kazi ya Roho wa Mungu, ya Roho Mtakatifu, na haikutoka kwa
mwanadamu, na kuweza kuwathibitishia kazi ya Roho Mtakatifu. Wakati wa Enzi ya
Neema, Yesu Mwenyewe Alifanya kazi hii yote badala yao, na hivyo watu
hawakuzungumza tena unabii. Kwa hivyo Yesu alikuwa nabii?
Yesu, kimsingi
alikuwa ni nabii, lakini pia Alikuwa na uwezo wa kufanya kazi ya mitume:
Aliweza kusema unabii na kuhubiri na kufundisha watu katika nchi yote. Bado
kazi Aliyoifanya na utambulisho Aliouwakilisha haukuwa unafanana. Alikuja
kuwakomboa binadamu wote, kumkomboa mwanadamu kutoka dhambini; Alikuwa nabii,
na mtume, lakini zaidi ya hapo Alikuwa Kristo. Nabii Anaweza kuzungumza unabii,
lakini haiwezi kusemwa kwamba yeye ni Kristo. Wakati huo, Yesu alizungumza
unabii mwingi, na hivyo inaweza kusemwa kwamba Alikuwa nabiii, lakni haiwezi
kusemwa kwamba Alikuwa nabii na hivyo sio Kristo. Hiyo ni kwa sababu
Alimwakilisha Mungu Mwenyewe katika kutekeleza hatua ya kazi, na utambulisho
Wake ulikuwa tofauti na ule wa Isaya: Alikuja kukamilisha kazi ya ukombozi, na
hivyo Alitoa maisha ya mwanadamu, na Roho wa Mungu Alikuja Kwake moja kwa moja.
Katika kazi Aliyoifanya, hakukuwa na uvuvio wa kutoka kwa Roho wa Mungu au
maelekezo kutoka kwa Yehova. Badala yake, Roho alikuja kufanya kazi moja kwa
moja, kitu ambacho kinatosha kuthibitisha kwamba Yesu Hakuwa sawa na nabii.
Kazi Aliyoifanya ilikuwa ni kazi ya ukombozi, kaziliyoifuatia ilikuwa ni
kuzungumza unabii. Alikuwa ni nabii, mtume, na zaidi ya hapo Alikuwa ni
Mkombozi. Wakati huo, watabiri, wangeweza tu kuzungumza unabii, na walikuwa
hawana uwezo wa kumwakilisha Roho wa Mungu katika kufanya kazi nyingine yoyote.
Kwa sababu Yesu alifanya kazi kubwa ambayo haijawahi kufanywa na binadamu, na
Alifanya kazi ya kumkomboa mwanadamu, kwa hiyo Alikuwa tofauti na manabii
wengine kama Isaya. Kwamba watu wengine hawakubali mkondo wa leo ni kwa sababu
hii imetengeneza kizuizi kwao. Wanasema: "Katika Agano Jipya manabii wengi
pia walisema maneno mengi—sasa, kwa nini hawakuwa Mungu katika mwili? Mungu wa
leo Anazungumza maneno—je, hii inatosha kuthibitisha kuwa Yeye ni Mungu mwenye
mwili? Huipatii Biblia umuhimu mkubwa, wala huichunguzi, sasa una msingi gani
wa kusema kwamba Yeye ni Mungu aliyepata mwili? Unasema kwamba wameongozwa na
Roho Mtakatifu, na unaamini kwamba hatua hii ya kazi ni kazi ambayo imefanywa
na Mungu Mwenyewe- lakini msingi wako kwa hili ni nini? Umetilia mkazo katika
maneno ya Mungu leo, inaonekana kana kwamba umeikana Biblia, na kuiweka katika
upande mmoja, na hivyo wanasema kwamba unaamini uzushi, kwamba wewe ni sehemu
ya kikundi cha kishetani.
Ikiwa unatamani kuwa na ushuhuda kwa kazi
ya Mungu wakati wa siku za mwisho, basi unapaswa kuelewa kisa cha ndani cha
Biblia, muundo wa Biblia, na hulka ya Biblia. Leo, watu wanaamini kwamba Biblia
ni Mungu, na kwamba Mungu ni Biblia. Na hivyo pia, wanaamini kwamba maneno yote
ya Biblia ni maneno pekee ambayo Mungu alizungumza, na kwamba yote
yalizungumzwa na Mungu. Wale wanaomwamini Mungu hata wanafikia hatua ya
kufikiri kwamba ingawa vitabu vyote sitini na sita vya Agano la Kale na Agano
Jipya viliandikwa na watu, vyote viliandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na vilikuwa
ni rekodi ya matamshi ya Roho Mtakatifu. Hii ni tafsiri ya watu yenye makosa,
na haiafikiani kabisa na kweli. Kimsingi, mbali na vitabu vya unabii, sehemu
kubwa ya Agano la Kale ni rekodi ya kihistoria. Baadhi ya nyaraka za Agano
Jipya zinatokana na uzoefu wa watu, na baadhi zinatokana na kupatiwa nuru na
Roho Mtakatifu; nyaraka za Paulo, kwa mfano, zilitokana na kazi ya mwanadamu,
zote zilitokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, na ziliandikwa kwa ajili ya
makanisa, yalikuwa ni maneno ya kushawishi na kutia moyo kwa kaka na dada wa
makanisa. Hayakuwa maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu—Paulo asingeweza
kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu, na wala hakuwa nabii, achilia mbali
kuona maono. Nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya makanisa ya Efeso,
Filadefia, Galatia, na makanisa mengineyo. Na hivyo, nyaraka za Paulo za Agano
Jipya ni nyaraka ambazo Paulo aliandika kwa ajili ya makanisa, na sio uvuvio wa
Roho Mtakatifu, wala sio matamshi ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu. Ni maneno
tu ya kushawishi, faraja, na kutia moyo ambayo aliyaandika kwa ajili ya
makanisa wakati wa kazi yake. Na hivyo pia, ni rekodi zaidi ya kazi na muda ya
Paulo. Ziliandikwa kwa ajili ya kaka na dada wote katika Bwana, na zilikuwa ni
kwa ajili ya kuwafanya kaka na dada wa makani yote ya wakati huo kufuata
ushauri wake na kudumu siku zote katika njia zote za Bwana Yesu. Kwa namna
yoyote ile Paulo hakusema kuwa, iwe ni kwa makanisa ya wakati huo au makanisa
ya wakati ujao, yote yanapaswa kula na kunywa vitu vyake, wala hakusema kwamba
maneno yake yote yalitoka kwa Mungu. Kulingana na mazingira ya kanisa wakati
huo, aliwasiliana tu na kaka na dada, na aliwashawishi, na akawaimarisha imani
kwao; na aliwahubiria na kuwakumbusha watu na kuwashawishi. Maneno yake
yalijikita katika mzigo wake mwenyewe, na aliwasadia watu kupitia maneno haya.
Alifanya kazi ya mitume wa kanisa wa wakati huo, alikuwa mfanyakazi ambaye
alitumiwa na Bwana Yesu, na hivyo alipewa jukumu la makanisa, alipewa jukumu la
kufanya kazi ya makanisa, alipaswa kujifunza mazingira ya kaka na dada, na kwa
sababu hii, aliandika nyaraka kwa kaka na dada wote katika Bwana. Yote
aliyoyasema yale yaliyokuwa ni ya kuadilisha na mazuri kwa watu yalikuwa
sahihi, lakini hayakuwa yanawakilisha matamshi ya Roho Mtakatifu, na hakuwa
anamwakilisha Mungu. Ni uelewa mbaya kupita kiasi, na makufuru makubwa sana kwa
watu kuchukulia rekodi za uzoefu wa mwanadamu na nyaraka za mwanadamu kama
maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu kwa makanisa! Hiyo ni kweli kabisa
tunapokuja katika nyaraka ambazo Paulo aliziandika kwa ajili ya makanisa, maana
nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya kaka na dada kulingana na mazingira na
hali ya kila kanisa kwa wakati huo, na yalikuwa ni kwa ajili ya kuwashawishi
kaka na dada katika Bwana, ili waweze kupokea neema ya Bwana Yesu. Nyaraka zake
zilikuwa ni kwa ajili ya kuwaamsha kaka na dada wa wakati huo. Inaweza kusemwa
kuwa huu ulikuwa ni mzigo wake mwenyewe, na pia ulikuwa ni mzigo aliopewa na
Roho Mtakatifu; hata hivyo, alikuwa ni mtume aliyeyaongoza makanisa ya wakati
huo, ambaye aliandika nyaraka kwa ajili ya makanisa na kuwashawishi, huo
ulikuwa wajibu wake. Utambulisho wake ulikuwa tu ni mtume anayefanya kazi, na
alikuwa ni mtume tu aliyetumwa na Mungu; hakuwa mtabiri, wala mtoa unabii. Kwa
hivyo kwake, kazi yake mwenyewe na maisha ya kaka na dada yalikuwa na umuhimu
mkubwa sana. Hivyo, asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu. Maneno
yake hayakuwa maneno ya Roho Mtakatifu, wala yasingesemwa kuwa ni maneno ya
Mungu, maana Paulo hakuwa chochote zaidi ya kiumbe wa Mungu, na hakika hakuwa
Mungu aliyepata mwili. Utambulisho wake haukuwa sawa na ule wa Yesu. Maneno ya
Yesu yalikuwa ni maneno ya Roho Mtakatifu, yalikuwa ni maneno ya Mungu, maana
utambulisho wake ulikuwa ule wa Kristo—Mwana wa Mungu. Inawezekanaje Awe sawa
na Paulo? Ikiwa watu wanaona nyaraka au maneno kama ya Paulo kama maatamshi ya
Roho Mtakatifu, na kuwaabudu kama Mungu, basi inaweza kusemwa tu kuwa ni watu
wasiochagua kwa busara. Tukisema kwa ukali zaidi, haya sio makufuru?
Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na inawezekenaje watu
wapigie magoti rekodi za nyaraka zake na maneno aliyoyazungumza kana kwamba
yalikuwa ni "kitabu kitakatifu," au "kitabu cha mbinguni"?
Je, inawezekana maneno ya Mungu kutamkwa kwa kawaida na mwanadamu?
Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na hivyo,
unasemaje—kwamba nyaraka alizoandika kwa ajili ya makanisa haziwezi kutiwa doa
na mawazo yake mwenyewe? Inawezekanaje zisitiwe doa na mawazo ya kibinadamu?
Aliandika nyaraka kwa ajili ya makanisa kulingana na uzoefu wake binafsi, na
kiwango cha maisha yake binafsi. Kwa mfano, Paulo aliandika waraka kwa kanisa
la Wagalatia ambao ulikuwa na maoni fulani, na Petro aliandika waraka mwingine,
ambao ulikuwa na mtazamo mwingine. Ni upi kati ya hizo ulitoka kwa Roho
Mtakatifu? Hakuna anayeweza kutoa jibu, hakika. Hivyo inaweza kusemwa tu kwamba
wote wanawiwa na mzigo kwa makanisa, lakini barua zao zinawakilisha kimo chao,
zinawakilisha vile wanavyowapatia na kuwasaidia kaka na dada, na vile
wanavyowiwa na makanisa, na zinawakilisha tu kazi ya binadamu; hayakuwa ya Roho
Mtakatifu kabisa. Ikiwa unasema kwamba nyaraka zake ni maneno ya Roho Mtakatifu,
basi wewe ni mpumbavu, na unafanya makufuru! Nyaraka za Paulo na nyaraka
nyingine za Agano Jipya ni sawa na kumbukumbu za viongozi mashuhuri wa kiroho
wa hivi karibuni. Zipo sawa na vitabu vya Watchman Nee au uzoefu wa Lawrence,
na kadhalika. Ni vile tu vitabu vya viongozi mashuhuri wa kiroho wa hivi
karibuni havijajumuishwa katika Agano Jipya, lakini hulka ya watu hawa ni sawa:
Kulikuwa na watu ambao walitumiwa na Roho Mtakatifu wakati fulani, na
hawakuweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja.
Injili ya Mathayo ya Agano Jipya inaandika
ukoo wa Yesu. Mwanzoni, inasema kwamba Yesu alikuwa mzao wa Abrahamu, mwana wa
Daudi, na mwana wa Yusufu; sehemu inayofuata inasema kwamba Yesu alizaliwa kwa
njia ya Roho Mtakatifu, na kuzaliwa na bikira—kitu kinachomaanisha kwamba
Hakuwa mwana wa Yusufu au mzao wa Abrahamu, kwamba Hakuwa mwana wa Daudi. Hata
hivyo, orodha ya ukoo inasisitiza kumhusisha Yesu na Yusufu. Sehemu inayofuata,
orodha ya ukoo inaanza kurekodi mchakato ambao kwa huo Yesu alizaliwa. Inasema
mimba ya Yesu ilitungwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, kwamba Alizaliwa na bikira,
na sio mwana wa Yusufu. Lakini katika orodha ya ukoo imeandikwa waziwazi kwamba
Yesu alikuwa mwana wa Yusufu, na kwa kuwa orodha ya ukoo iliandikwa kwa ajili
ya Yesu, inaandika vizazi arobaini na mbili. Inapokwenda katika ukoo wa Yusufu,
inasema kwa haraka kwamba Yusufu alikuwa mume wa Mariamu, haya ni maneno kwa
ajili ya kuthibitisha kwamba Yesu alikuwa mzao wa Abrahamu. Je, huu si
mkanganyiko? Orodha hii ya ukoo inaonyesha waziwazi chimbuko la Yusufu, ni wazi
kwamba hii ni orodha ya ukoo wa Yusufu, lakini Mathayo anasisitiza kwamba ni
orodha ya ukoo wa Yesu. Je, hii haipingi ukweli kwamba Yesu alizaliwa kwa njia
ya Roho Mtakatifu? Hivyo, orodha ya ukoo iliyoandikwa na Mathayo sio mawazo ya
kibinadamu? Hii ni dhihaka! Kwa namna hii, unaweza kujua kwamba kitabu hiki sio
chote kimetoka kwa Roho Mtakatifu. Pengine, kuna baadhi ya watu wanaodhani
kwamba Mungu lazima atakuwa na orodha ya ukoo duniani, na matokeo yake ni
kwamba wanampachika Yesu kama kizazi cha arobaini na viwili cha Abrahamu. Hii
ni dhihaka kabisa! Baada ya kuja duniani, Mungu angewezaje kuwa na orodha ya
ukoo? Ikiwa unasema kwamba Mungu ana ukoo, je, humweki katika madaraja sawa
miongoni mwa viumbe wa Mungu? Maana Mungu si wa ulimwengu, Yeye ni Bwana wa
uumbaji, na ingawa yeye ni wa mwili, hana asili sawa na mwanadamu. Unawezaje
kumweka Mungu katika daraja sawa na viumbe wa Mungu? Abrahamu hawezi
kumwakilisha Mungu; alikuwa ni mhusika wa kazi ya Yehova wakati huo, alikuwa ni
mtumishi mwaminifu tu aliyethibitishwa na Yehova, na alikuwa mmoja wa watu wa
Israeli. Inawezekanaje awe babu wa Yesu?
Ni nani aliandika orodha ya ukoo wa Yesu?
Ni Yesu Mwenyewe ndiye aliyeandika? Je, ni Yesu Mwenyewe ndiye Alisema,
"Andika orodha Yangu ya ukoo"? Iliandikwa na Mathayo baada ya Yesu
kuangikwa msalabani. Wakati huo, Yesu alikuwa amefanya kazi kubwa ambayo
ilikuwa haifahamiki kwa mitume, na Hakutoa maelezo yoyote. Baada ya Yeye
kuondoka, mitume walianza kuhubiri na kufanya kazi kila mahali, na kwa ajili ya
hatua hiyo ya kazi, walianza kuandika nyaraka na vitabu vya injili. Vitabu vya
injili ya Agano Jipya vilirekodiwa miaka ishirini hadi thelathini baada ya Yesu
kusulubiwa msalabani. Kabla ya hapo, watu wa Israeli walisoma tu Agano la Kale.
Hiyo ni sawa na kusema, katika Enzi ya Neema watu walisoma Agano la Kale. Agano
Jipya lilionekana tu wakati wa Enzi ya Neema. Agano Jipya halikuwepo wakati wa
kazi ya Yesu; watu waliandika kazi Yake baada ya kuwa amefufuka na kupaa
mbinguni. Baada ya hapo kulikuwa na Injili Nne, katika nyongeza hiyo pia
kulikuwa na nyaraka za Paulo na Petro, na vile vile kitabu cha Ufunuo. Zaidi ya
miaka mia moja tu baada ya Yesu kupaa mbinguni, ambapo vizazi vilivyofuata
vilipangilia rekodi zao, na kuzaliwa Agano Jipya. Ni baada tu ya kazi hii
kukamilika ndipo kukapatikana Agano Jipya; halikuwepo hapo kabla. Mungu alikuwa
amefanya kazi yote hiyo, mtume Paulo alifanya kazi yote hiyo, na baadaye
nyaraka za Paulo na Petro ziliunganishwa, na njozi kuu zaidi iliyorekodiwa na Yohana
katika kisiwa cha Patmo iliwekwa mwishoni, maana ilikuwa inatoa unabii wa kazi
ya siku za mwisho. Hii yote ilikuwa ni mipango ya vizazi vilivyofuata na ni
tofuati na matamshi ya leo. Kile kilichorekodiwa leo ni kulingana na hatua za
kazi ya Mungu; kile ambacho watu wanashughulika nacho leo ni kazi ambayo
imefanywa na Mungu Mwenyewe, na maneno yaliyotamkwa na Mungu Mwenyewe. Hupaswi
kuingilia—maneno, ambayo yanatoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu,
yameliyopangwa hatua kwa hatua, na ni tofauti na mpangilio wa rekodi za
wanadamu. Inaweza kusemwa kuwa, kile walichorekodi kilikuwa ni kulingana na
kiwango chao cha elimu na tabia. Kile walichokirekodi kilikuwa ni uzoefu wa
wanadamu, na kila mmoja alikuwa na namna yake ya kurekodi na kuelewa, na kila
rekodi ilikuwa tofauti. Hivyo, ikiwa unaiabudu Biblia kama Mungu wewe ni mjinga
na mpumbavu wa kutupwa! Kwa nini usitafute kazi ya Mungu wa leo? Ni kazi ya
Mungu tu ndiyo inayoweza kumwokoa mwanadamu. Biblia haiwezi kumwokoa mwanadamu,
haijabadilika kabisa kwa maelfu ya miaka, na kama unaiabudu Biblia hutaweza
kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Hatua mbili za kazi ya Mungu katika Israeli zote
zimerekodiwa katika Biblia, na hivyo unaona miongoni mwa rekodi hizi majina
yote ni ya Israeli, na matukio yote ni ya Israeli; na hata jina “Yesu” ni jina
la Kiisraeli. Ikiwa unaendelea kusoma Biblia leo, huoni unafungamanishwa kwa
maagano? Yale yaliyorekodiwa katika Agano Jipya la Biblia ni masuala ya Yudea.
Matini ya awali yalikuwa katika Kiyunani na Kiebrania, na maneno ya Yesu, na
jina ambalo kwalo Aliitwa wakati huoambapo yote yalikuwa katika lugha ya
mwanadamu. Aliposulubiwa msalabani, Yesu Alisema: “Eloi, Eloi, lama sabakthani”
Je, hiki sio Kiebrania? Hii tu ni kwa sababu Yesu alipata mwili Yudea, lakini
haithibitishi kwamba Mungu ni Myahudi. Leo, Mungu amefanyika mwili China, na
hivyo kila kitu Anachokisema bila shaka ni katika lugha ya Kichina. Lakini
hakiwezi kulinganishwa na Kichina kilichotafsiriwa kutoka katika Biblia, maana
chanzo cha maneno haya ni tofauti. Moja inatoka kwa Kiebrania kilichorekodiwa
na watu, na moja inatoka katika matamshi ya moja kwa moja ya Roho.
Umeme wa Mashariki, Kanisa la MwenyeziMungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa
pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao
wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa
na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe
na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni
ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno
ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni