Jumamosi, 21 Oktoba 2017

maneno ya Mwenyezi Mungu | Tamko La Kwanza

maneno ya  Mwenyezi Mungu | Tamko La Kwanza

Kanisa la Mwenyezi Mungu

Je, wale wanaoshuhudia maneno Yangu huyakubali kwa kweli? Je, mnanijua kwa kweli? Mmejifunza utiifu kweli? Ninyi hutumia rasilimali kwa ajili Yangu kwa uaminifu? Mmekuwa na ushuhuda thabiti, usiokubali kushindwa Kwangu mlipokabiliwa na joka kuu jekundu? Je, moyo wenu wa ibada hulifedhehesha kweli joka kuu jekundu? Ni kupitia tu kwa jaribio la maneno Yangu ndipo Naweza kutimiza lengo Langu la kulitakasa kanisa na kuwachagua wale wanaonipenda Mimi kweli. Ni jinsi gani tena ambayo mtu yeyote angenielewa Mimi? Ni nani anaweza kuelewa uadhama Wangu, ghadhabu Yangu, na hekima Yangu kupitia kwa maneno Yangu? Nitakamilisha Nilichoanza, lakini bado ni Mimi nipimaye mioyo ya wanadamu. Kwa kweli, hakuna mwanadamu anayenielewa Mimi kwa ukamilifu, kwa hiyo Ninamwongoza kwa maneno, na kumwongoza katika mwongo mpya kwa njia hii. Mwishowe Nitakamilisha kazi Yangu yote kupitia kwa maneno Yangu, na kuwarudisha wale wanaonipenda Mimi kweli kwa ufalme Wangu, kuishi mbele ya kiti Changu cha enzi. Hali sio kama ilivyokuwa wakati fulani, na kazi Yangu imeingia katika kiwango kipya cha kuanza. Hilo likiwa hivyo, kutakuwa na njia mpya: Wale wanaolisoma neno Langu na kulikubali kama uzima wao kabisa ndio watu wa ufalme Wangu. Kwa vile wako katika ufalme Wangu, wao ni watu Wangu katika ufalme. Wanapoongoza na maneno Yangu, ingawa wanatajwa kama watu Wangu, wao kamwe hawako chini ya 'wana' Wangu. Kama watu Wangu, wote ni lazima wawe waaminifu katika ufalme Wangu na kutimiza majukumu yao, na wale wanaokosea amri Zangu za usimamizi lazima wapate adhabu Yangu. Hili ni onyo Langu kwa wote.

Ijumaa, 20 Oktoba 2017

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)



Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa
I
Nilitaka kulia lakini hakuna mahali palihisi sawa.
Nilitaka kuimba lakini hakuna wimbo ulipatikana.
Nilitaka kuonyesha upendo wa kiumbe aliyeumbwa.
Nikitafuta juu na chini, lakini hakuna maneno yangeweza kusema,
yangeweza kusema jinsi hasa ninavyohisi.
Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu.
Nainua mikono yangu kwa sifa, ninafurahia kwamba Ulikuja katika dunia hii.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Kwa nini unamwamini Mungu ? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa...