Mpango wa Mungu wa miaka elfu sita ya usimamizi unaelekea kikomo, na lango la ufalme limefunguliwa kwa wale ambao wanatafuta kuonekana kwa Mungu. Ndugu wapendwa, mnasubiri nini? Mnatafuta nini? Mnausubiri kuonekana kwa Mungu? Mnazitafuta nyayo za Mungu? Kuonekana kwa Mungu kunatamaniwa sana! Ni vigumu, kiasi gani kupata nyayo za Mungu! Katika enzi kama hii, katika dunia kama hii, lazima tufanye nini ili tushuhudie kuonekana kwa Mungu? Sharti tufanye nini ili tufuate nyayo za Mungu? Wale wote wanaosubiri kuonekana kwa Mungu wanakumbana na maswali kama haya. Nyinyi nyote mmewahi kuyafikiria zaidi ya mara moja—ila matokeo ni gani? Mungu hujidhihirisha wapi? Nyayo za Mungu zipo wapi? Umepata majibu?
Jumamosi, 12 Agosti 2017
Mwenyezi Mungu|Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu ilianza tu baada ya mwanadamu kupotoshwa, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu pia ilianza tu punde mwanadamu alipopotoshwa. Kwa maneno mengine, usimamizi wa Mungu wa mwanadamu ulianza kutokana na kazi ya kumwokoa mwanadamu, na wala haukutokana na kazi ya kuiumba dunia. Hakungekuwa na kazi ya kumsimamia mwanadamu pasipo kuwepo na tabia potovu ya mwanadamu, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu ina sehemu tatu, badala ya hatua nne, au enzi nne. Hii tu ndio njia sahihi ya kutaja kazi ya Mungu ya usimamizi wa mwanadamu. Enzi ya mwisho itakapofikia kikomo, kazi ya kusimamia mwanadamu itakuwa imekamilika. Hitimisho la kazi ya usimamizi lina maana kuwa kazi ya kuwaokoa wanadamu wote imemalizika kabisa, na kwamba mwanadamu amefika mwisho wa safari yake. Pasipo kazi ya kuwaokoa wanadamu wote, kazi ya usimamizi wa wanadamu haingekuwapo, wala hakungekuwa na hatua tatu za kazi. Ilikuwa ni hasa kwa ajili ya upotovu wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu alihitaji wokovu kwa dharura, ndipo Yehova alikamilisha uumbaji wa dunia na kuanza kazi ya Enzi ya Sheria. Hapo tu ndipo kazi ya kumsimamia mwanadamu ilipoanza, kumaanisha kwamba hapo tu ndipo kazi ya kumwokoa mwanadamu ilipoanza. “Kumsimamia mwanadamu” haimaanishi kuongoza maisha ya mwanadamu aliyeumbwa upya duniani (ambapo ni kusema, mwanadamu ambaye bado hakuwa amepotoshwa). Badala yake, ni wokovu wa ubinadamu ambao umepotoshwa na Shetani, ambapo ni kusema kwamba, ni kubadilishwa kwa mwanadamu aliyepotoshwa. Hii ndiyo maana ya kumsimamia mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu haihusishi kazi ya kuiumba dunia, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu haijumuishi kazi ya kuumba ulimwengu, na inahusisha tu hatua tatu za kazi zilizo tofauti na uumbaji wa ulimwengu. Ili kuelewa kazi ya kumsimamia mwanadamu, ni muhimu kuwa na ufahamu wa historia ya hatua tatu za kazi—hili ndilo kila mtu anapaswa kulifahamu ili kuokolewa. Kama viumbe wa Mungu, mnapaswa kutambua kuwa mwanadamu aliumbwa na Mungu, na kufahamu chanzo cha upotovu wa mwanadamu, na, vilevile, kufahamu mchakato wa wokovu wa mwanadamu. Iwapo mnafahamu tu jinsi ya kutenda kulingana na mafundisho ili kupata neema ya Mungu, lakini hamna fununu jinsi Mungu anavyomwokoa mwanadamu, au ya chanzo cha upotovu wa mwanadamu, basi hili ndilo mnalokosa kama viumbe wa Mungu. Hupaswi kutoshelezwa tu na kuelewa kwa ukweli unaoweza kuwekwa katika vitendo, huku ukibakia kutojua upeo mpana wa kazi ya usimamizi ya Mungu—kama hivi ndivyo ilivyo, basi wewe ni mwenye kulazimisha kauli sana. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo hadithi ya ndani ya usimamizi wa Mungu wa mwanadamu, ujio wa injili ya dunia nzima, fumbo kubwa zaidi kati ya wanadamu, na pia ni msingi wa kueneza injili. Ukizingatia tu kuelewa ukweli sahili unaohusiana na maisha yako, na usijue lolote kuhusu hili, maajabu makuu zaidi na maono, basi maisha yako si ni sawa na bidhaa yenye kasoro, yasio na maana isipokuwa kuangaliwa?
Ikiwa mwanadamu huzingatia tu matendo, na kuona kazi ya Mungu na hekima ya mwanadamu kama za upili, basi si ni sawa na kuwa mwerevu kwa kiasi kidogo cha pesa na mjinga kwa kiasi kikubwa cha pesa? Lile ambalo sharti ulijue, lazima ulijue, na kile unachostahili kuonyesha kwa vitendo, lazima ukionyeshe kwa vitendo. Ni hapo tu ndipo utakapokuwa mtu anayejua kufuata ukweli. Siku yako ya kueneza injili itakapowadia, ikiwa utaweza kusema tu kuwa Mungu ni Mkuu na Mwenye haki, kuwa ni Mungu Mkuu, Mungu ambaye hapana mwanadamu yeyote mkuu anayeweza kujilinganisha naye, na kuwa hakuna aliye juu zaidi wa kumpiku..., kama waweza tu kusema maneno haya yasiyofaa na ovyo, na kabisa huwezi kunena maneno yenye umuhimu zaidi, na yaliyo na kiini, kama huna lolote la kusema kuhusu kumjua Mungu, ama kazi ya Mungu, na zaidi ya hapo, huwezi kuelezea ukweli, au kutoa kile ambacho kinakosekana kwa mwanadamu, basi mtu kama wewe hana uwezo wa kutekeleza wajibu wake vyema. Kumshuhudia Mungu na kueneza injili ya ufalme si jambo rahisi. Lazima kwanza uwe na ukweli, na maono yatakayoeleweka. Unapokuwa na uwazi wa maono na ukweli wa masuala tofauti tofauti ya kazi ya Mungu, moyoni mwako unapata kujua kazi ya Mungu, na bila kujali anayoyafanya Mungu—iwe ni hukumu ya haki ama kusafishwa kwa mwanadamu—unamiliki maono makuu kama msingi wako, na unamiliki ukweli sahihi wa kuonyesha kwa matendo, basi utaweza kumfuata Mungu hadi mwisho. Lazima ujue kuwa bila kujali kazi ambayo Yeye anatenda, lengo la kazi ya Mungu halibadiliki, kiini cha kazi Yake hakibadiliki, na mapenzi Yake kwa mwanadamu hayabadiliki. Bila kujali maneno Yake ni makali namna gani, haijalishi mazingira ni mabaya kiasi gani, kanuni za kazi Yake, na nia Yake ya kumwokoa mwanadamu hayatabadilika. Mradi tu si ufunuo wa mwisho wa mwadhamu au hatima ya mwanadamu, na si kazi ya awamu ya mwisho, au kazi ya kutamatisha mpango wote wa usimamizi, na mradi tu ni wakati Anapomfinyanga mwanadamu, basi kiini cha kazi Yake hakitabadilika: Daima kitakuwa wokovu wa mwanadamu. Hili linapaswa kuwa msingi wa imani yenu katika Mungu. Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu. Punde unapofahamu lengo la hatua hizi tatu za kazi, basi utafahamu jinsi ya kuthamini umuhimu wa kila hatua ya kazi, na utatambua jinsi ya kutenda ili kutosheleza shauku ya Mungu. Iwapo utaweza kufikia hatua hii, basi hili, ono kubwa kuliko yote, litakuwa msingi wako. Unapaswa kufuata sio tu njia rahisi za matendo, ama ukweli wenye undani, lakini unapaswa kuunganisha maono na matendo, ili kwamba kuwe na ukweli unaoweza kuwekwa kwenye vitendo, na maarifa yaliyo na msingi wa maono. Ni hapo tu ndipo utakapokuwa mtu anayefuatilia ukweli.
Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani ya hatua kuna maelezo ya tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu. Wale wasiofahamu hatua tatu za kazi watakosa kuelewa njia mbalimbali na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu; wale wanaoshikilia tu imara mafundisho ya dini yanayosalia kutoka katika hatua moja ya kazi ni watu wanaomwekea Mungu mipaka kwa mafundisho ya dini, na wale ambao imani yao kwa Mungu haina udhahiri na uhakika . Watu kama hao kamwe hawawezi kupokea wokovu wa Mungu. Ni hatua tatu tu za Mungu zinazoweza kuonyesha kabisa ukamilifu wa tabia ya Mungu, na kuonyesha kabisa nia ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu wote, na mchakato mzima wa wokovu wa mwanadamu. Hili ni dhibitisho kuwa Yeye amemshinda Shetani na kumpata mwanadamu, ni dhibitisho la ushindi wa Mungu, na ni maonyesho ya tabia kamili ya Mungu. Wale wanaoelewa hatua moja tu kati ya hatua tatu za kazi ya Mungu wanajua tu sehemu ya tabia ya Mungu. Katika dhana ya mwanadamu, ni rahisi kwa hatua hii moja kuwa mafundisho ya kidini, panakuwa na uwezekano zaidi wa mwanadamu kuweka amri kumhusu Mungu, na mwanadamu anatumia hii sehemu moja ya tabia ya Mungu kama dhihirisho la tabia nzima ya Mungu. Zaidi ya hayo, mawazo mengi ya mwanadamu yanachanganywa ndani yake, hivi kwamba anaweka vikwazo imara kwa tabia, nafsi, na hekima ya Mungu, na pia kanuni za kazi ya Mungu ndani ya vigezo vyenye mipaka, akiamini kwamba ikiwa Mungu alikuwa hivi wakati mmoja, basi Yeye atasalia kuwa vile daima, na kamwe hatabadilika. Ni wale tu wanaojua na kuthamini hatua tatu za kazi ndio wanaoweza kumjua Mungu kabisa na kwa usahihi. Angalau, hawatamfafanua Mungu kama Mungu wa Waisraeli, ama Wayahudi, na hawatamwona kama Mungu atakayesulubiwa msalabani milele kwa ajili ya mwanadamu. Kama unapata kumjua Mungu kutokana na hatua moja ya kazi Yake tu, basi maarifa yako ni kidogo, kidogo sana. Maarifa yako ni sawa na tone moja katika bahari. Kama si hivyo, kwa nini wengi wa walinzi wa kidini wa kale walimtundika Mungu msalabani akiwa hai? Je, si kwa ajili mwanadamu humwekea Mungu mipaka kwenye vigezo fulani? Je, si watu wengi humpinga Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofautitofauti ya Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye majivuno na wadekezi katika asili yao, na wanatazama kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza masomo ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo zee “kudhibitisha” kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele ya Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wadogo wasioona mbali, wanaojaribu kuonyesha tu jinsi walivyo werevu? Kwa maarifa haba ya Biblia, wanajaribu kupotosha “wasomi” wa dunia, kwa mafundisho duni ya dini ili kuwafunza watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya ihusu mchakato wao wanavyofikiria, na kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kuona kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Je, watu hawa wana mantiki yoyote ya kuzungumzia? Kwa kweli, maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo wanavyokuwa wagumu wa kuhukumu kazi Yake. Zaidi ya hayo, wanazungumzia tu machache kuhusu maarifa yao ya kazi ya Mungu leo, lakini si wepesi wa kuhukumu. Kadri watu wanavyojua machache kumhusu Mungu, ndivyo wanavyozidi kuwa wenye majivuno na wenye kujiamini sana, na ndivyo wanavyozidi kutangaza nafsi ya Mungu kwa utundu—ilhali wanazungumzia tu nadharia, na wala hawapeani ushahidi wowote halisi. Watu kama hawa hawana thamani yoyote kabisa. Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wanaopayuka, ni wepesi wa kuhukumu wanaoruhusu silika yao ya kiasili kukana haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na pia kuitusi na kuikufuru —je, watu hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, zaidi ya hayo, wale wasiojua, wenye majivuno ya asili na wasioweza kutawalwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Hawadharau tu wale wanaofanya kazi ya Mungu, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa jasiri pasi na hadhari hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele! Watu kama hawa wasio na heshima, wenye kujifurahisha, wanajifanya kuwa wanamwamini Mungu, na kadiri wanavyozidi kufanya vile, ndivyo wanavyozidi kukosea amri za utawala wa Mungu. Je, si hao mafidhuli ambao kiasili hawazuiliki, na hawajawahi kumtii yeyote, wote hupitia njia hii? Je, si wao humpinga Mungu siku baada ya siku, Yeye ambaye daima huwa mpya na wala hazeeki? Leo, mnapaswa kuelewa umuhimu wenu wa kujua hatua tatu za kazi ya Mungu. Maneno Ninayosema yana manufaa kwenu, wala si mazungumzo ya bure. Mkikimbiza mambo, je, si bidii Yangu yote itakuwa kazi bure? Kila mmoja wenu anapaswa kujua asili yake. Watu wengi wamebobea katika mabishano, majibu ya maswali ya nadharia yanatoka kinywani mwenu, lakini hamna la kusema kwa maswali kuhusu dutu. Hadi leo, bado mnashiriki mazungumzo duni, na hamuwezi kubadilisha asili yenu ya zamani, na wengi wenu hawana nia ya kubadilisha jinsi mnavyofuatilia ili kupata ukweli wa juu, mnaishi tu maisha yenu shingo upande. Je, watu kama hawa wataweza kumfuata Mungu hadi tamati vipi? Hata ikiwa mtafika mwishoni mwa safari, itakuwa na faida gani kwenu? Ni bora mbadili mawazo yenu kabla hamjachelewa, kufuatilia kwa kweli, au kufa moyo mapema. Muda unapokatika utakuwa kimelea doezi—je, mko radhi kutekeleza jukumu kama hili la hali ya chini na lenye aibu?
Hatua tatu za kazi ni rekodi ya kazi nzima ya Mungu, ni rekodi ya wokovu wa Mungu wa mwanadamu, na si porojo tu. Kama kweli mnataka kutafuta kujua tabia nzima ya Mungu, basi sharti mfahamu hatua tatu za kazi inayofanywa na Mungu, na, zaidi, sharti msiache hatua yoyote. Hiki ndicho kiwango cha chini kinachopaswa kufikiwa na wale wanaotafuta kumjua Mungu. Mwanadamu mwenyewe hawezi kuvumbua maarifa ya Mungu. Si kitu ambacho mwanadamu mwenyewe anaweza kufikiria, wala si matokeo ya fadhila za Roho Mtakatifu kwa mtu mmoja. Badala yake, ni maarifa yanayotokea mwanadamu anapopitia kazi ya Mungu, na ni maarifa ya Mungu yanayotokana tu na mwanadamu kupitia ukweli wa kazi ya Mungu. Maarifa kama haya hayawezi kutimizwa kwa ghafla, wala si jambo linaloweza kufundishwa. Inahusiana kabisa na uzoefu wa kibinafsi. Wokovu wa Mungu wa mwanadamu ndiyo kiini cha hatua hizi tatu za kazi, ilhali katika kazi ya wokovu kumejumuishwa mbinu kadhaa za kufanya kazi na namna ambazo tabia ya Mungu imeonyeshwa. Hili ndilo jambo gumu sana kwa mwanadamu kutambua na kwa mwanadamu kuelewa. Mgawanyiko wa enzi, mabadiliko ya kazi ya Mungu, mabadiliko katika eneo la kazi, mabadiliko ya wanaopokea kazi na kadhalika—haya yote yamejumuishwa katika hatua tatu za kazi. Hususan, tofauti katika njia ya utendakazi wa Roho Mtakatifu, na vilevile mabadiliko katika tabia ya Mungu, picha, jina, utambulisho, au mabadiliko mengine, yote ni sehemu ya hatua tatu za kazi. Sehemu moja ya kazi inaweza tu kuwakilisha sehemu moja, na imewekewa mipaka ndani ya wigo fulani. Haihusiani na mgawanyiko wa enzi, ama mabadiliko ya kazi ya Mungu, wala masuala mengine. Huu ni ukweli ulio waziwazi. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo ukamilifu wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu lazima ajue kazi ya Mungu, tabia ya Mungu katika kazi ya wokovu, na bila ukweli huu, maarifa yako kumhusu Mungu yatakuwa tu maneno matupu, ni mahubiri ya starehe tu. Maarifa kama haya hayawezi kumshawishi au kumshinda mtu, maarifa kama haya yako nje ya uhalisi, na si ukweli. Yanaweza kuwa mengi, na mazuri kwa masikio, lakini kama hayaambatani na tabia ya asili ya Mungu, basi Mungu hatakusamehe. Hatakosa kuyasifu maarifa yako tu, bali pia atakuadhibu kwa kuwa mwenye dhambi aliyemkufuru. Maneno ya kumjua Mungu hayazungumzwi kwa mzaha. Ingawa unaweza kuwa na ulimi laini wenye maneno matamu, na maneno yako yaweza kuwafufua wafu, na kuwaua walio hai, bado huna elimu ya kuzungumza kuhusu maarifa ya Mungu. Mungu si mtu ambaye unaweza kuhukumu kwa urahisi, ama kusifu bila mpango, ama kupaka tope bila kujali. Unamsifu mtu yeyote na watu wowote, ilhali unajitahidi kupata maneno sahihi ya kuelezea ukuu wa wema na neema za Mungu—hili ndilo mshindwa yeyote hujifunza. Ingawa kuna wataalam wengi wa lugha wanaoweza kumwelezea Mungu, usahihi wa kile wanachoelezea ni asilimia moja ya ukweli unaozungumzwa na watu wa Mungu na wana misamiati michache tu, ilhali wanamiliki tajriba yenye uzito. Basi inaweza kuonekana kuwa maarifa ya Mungu yapo katika usahihi na uhalisi, na wala si utumiaji mzuri wa maneno au misamiati mingi. Maarifa ya mwanadamu na maarifa ya Mungu kabisa hayahusiani. Somo la kumjua Mungu liko juu zaidi kuliko sayansi za asili za mwanadamu. Ni somo linaloweza kutimizwa tu na idadi ndogo sana ya watu wanaotafuta kumjua Mungu, na haliwezi kutimizwa na mtu yeyote tu mwenye kipaji. Na kwa hivyo lazima msione kumjua Mungu na kufuatilia ukweli kama kwamba kunaweza kupatikana na mtoto mdogo tu. Pengine umekuwa na mafanikio makuu katika maisha yako ya kifamilia, ama kazi yako, ama katika ndoa yako, lakini inapofika kwenye ukweli, na somo la kumjua Mungu, huna lolote la kujivunia, hujatimiza malengo yoyote. Kutia ukweli kwenye vitendo, inaweza kusemwa, ni jambo gumu kwenu, na kumjua Mungu ni tatizo kuu hata zaidi. Hili ni tatizo lenu, na pia ni tatizo linalokabiliwa na wanadamu wote. Kati ya wale wenye mafanikio katika kumjua Mungu, karibu wote hawajafikia kiwango. Mwanadamu hajui maana ya kumjua Mungu, ama kwa nini ni muhimu kumjua Mungu, ama kiasi gani kinahesabiwa kama kumjua Mungu. Hili ndilo linalomshangaza mwanadamu, na ni kitendawili kikubwa zaidi kinachokabiliwa na mwanadamu—na hakuna awezaye kujibu swali hili, ama aliye na hiari kujibu hili swali, kwa sababu, hadi leo, hamna katika wanadamu aliyefanikiwa katika kusomea kazi hii. Pengine, kitendawili cha hatua tatu za kazi kitakapotambulishwa kwa mwanadamu, kutakuwepo katika mfululizo kundi la watu wenye vipaji wanaomjua Mungu. Bila shaka, Natumaini kuwa hivyo ndivyo ilivyo, na, hata zaidi, Niko katika harakati ya kutekeleza kazi hii, na Ninatumaini kuona kujitokeza kwa vipaji zaidi kama hivi katika siku za hivi karibuni. Watakuwa wale wanaoshuhudia ukweli wa hatua hizi tatu za kazi, na, bila shaka, watakuwa pia wa kwanza kushuhudia hizi hatua tatu za kazi. Kama kutakuwa na aliye na vipaji hivi, siku ambayo kazi ya Mungu itafikia kikomo, ama kuwe na wawili ama watatu, na kibinafsi wamekubali kufanywa wakamilifu na Mungu mwenye mwili, basi hakuna jambo la kuhuzunisha na kujutia kama hili—ingawa ni katika hali mbaya zaidi tu. Kwa vyovyote vile, Ninatumai kuwa wale wote wanaotafuta kwa kweli wanaweza kupata baraka hii. Tangu mwanzo wa wakati, hakujawahi kuwa na kazi kama hii, hapo awali hakujawahi kuwa na kazi kama hii katika historia ya ukuaji wa mwanadamu. Kama kweli unaweza kuwa mmoja wa wale wa kwanza wanaomjua Mungu, je, si hii itakuwa heshima ya juu kuliko viumbe wote? Je, kuna kiumbe mwingine kati ya wanadamu anayeweza kusifiwa na Mungu zaidi? Kazi kama hii ni ngumu kutekeleza, lakini mwishowe bado itapokea malipo. Bila kujali jinsia yao ama uraia wao, wale wote wenye uwezo wa kufikia maarifa ya Mungu, mwishowe, watapokea heshima kuu ya Mungu, na watakuwa tu wenye kumiliki mamlaka ya Mungu. Hii ndiyo kazi ya leo, na pia ndiyo kazi ya siku za usoni; ni ya mwisho na ya juu zaidi kuwahi kutekelezwa katika miaka 6000 ya kazi, na ni njia ya kufanya kazi inayodhihirisha kila kundi la mwanadamu. Kupitia kazi ya kumfanya wanadamu kumjua Mungu, daraja tofauti za mwanadamu zinadhihirishwa: Wale wanaomjua Mungu wamehitimu kupokea baraka za Mungu na kukubali ahadi zake, wakati wale wasiomjua Mungu hawajahitimu kupokea baraka za Mungu wala kupokea ahadi zake. Wale wanaomjua Mungu ni wandani wa Mungu, na wale wasiomjua Mungu hawawezi kuitwa wandani wa Mungu; wandani wa Mungu wanaweza kupokea baraka zozote za Mungu, lakini wale wasio wandani wa Mungu hawastahili kazi yoyote Yake. Iwe ni dhiki, usafishaji, ama hukumu, yote ni kwa ajili ya kumfanya mwanadamu hatimaye kufikia maarifa ya Mungu na ili kwamba mwanadamu amtii Mungu. Hii ndiyo athari pekee itakayofikiwa hatimaye. Hakuna lolote katika hatua tatu za kazi lililofichwa, na hii ni faida kwa maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu, na humsaidia mwanadamu kupata maarifa kamili na mengi ya Mungu. Kazi hii yote ni ya kumfaidi mwanadamu.
Kazi ya Mungu Mwenyewe ni maono ambayo mwanadamu lazima afahamu, kwa kuwa kazi ya Mungu haiwezi kutekelezwa na mwanadamu, wala haimilikiwi na mwanadamu. Hatua tatu za kazi ndizo ukamilifu wa usimamizi wa Mungu, na hakuna ono kuu kuliko hili linalopaswa kufahamika kwa mwanadamu. Kama mwanadamu hafahamu maono haya makuu, basi si rahisi kumjua Mungu, na si rahisi kujua mapenzi ya Mungu, na, zaidi ya hayo, njia ambayo mwanadamu anapitia inazidi kuwa ngumu. Bila maono, mwanadamu hangeweza kufika umbali huu. Ni maono ambayo yamemlinda mwanadamu hadi leo, na ambayo yamempa mwanadamu ulinzi mkuu. Katika siku za usoni, maarifa yenu lazima yawe ya kina, na sharti mfahamu mapenzi Yake yote na umuhimu wa kazi Yake yenye busara katika hatua tatu za kazi. Hiki tu ndicho kimo chenu cha kipekee. Hatua ya kazi ya mwisho haisimami peke yake, ila ni sehemu ya yote iliyounganishwa pamoja na hatua mbili za awali, ambayo ni kusema kwamba haiwezekani kukamilisha kazi nzima ya wokovu kwa kufanya kazi ya hatua moja pekee. Ingawa hatua ya mwisho ya kazi inaweza kumwokoa mwanadamu kabisa, hii haimaanishi kwamba ni muhimu tu kutekeleza hatua hii pekee, na kwamba hatua mbili za hapo awali hazihitajiki kumwokoa mwanadamu kutokana na ushawishi wa Shetani. Hakuna hatua moja kati ya zote tatu inayoweza kuwekwa kama maono ya kipekee ambayo lazima yajulishwe mwanadamu, kwa kuwa ukamilifu wa kazi ya wokovu ni hatua tatu za kazi, wala si hatua moja kati ya tatu. Ilimradi kazi ya wokovu bado haijakamilishwa, usimamizi wa Mungu utashindwa kufikia kikomo. Nafsi ya Mungu, tabia, na hekima zimeonyeshwa katika ukamilifu wa kazi ya wokovu, wala hazikufichuliwa kwa mwanadamu hapo mwanzo, lakini zimeonyeshwa hatua kwa hatua katika kazi ya wokovu. Kila hatua ya kazi ya wokovu huonyesha sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya nafsi Yake: si kila hatua ya kazi inayoweza moja kwa moja kuonyesha kabisa na kwa ukamilifu nafsi ya Mungu. Kwa hivyo, kazi ya wokovu inaweza tu kuhitimishwa hatua tatu za kazi zitakapokamilika, na kwa hivyo, maarifa ya mwanadamu ya ukamilifu wa Mungu hayawezi kutenganishwa na hatua tatu za kazi ya Mungu. Kile ambacho mwanadamu hupokea kutoka kwa hatua moja ya kazi ni tabia ya Mungu inayoonyeshwa katika sehemu moja ya kazi yake tu. Haiwezi kuwakilisha tabia na nafsi inayoonyeshwa katika hatua ya awali na ijayo. Hii ni kwa sababu kazi ya kumwokoa mwanadamu haiwezi kumalizika mara moja katika kipindi kimoja, ama katika eneo moja, lakini hukuwa kwa kina hatua kwa hatua kulingana na kiwango cha kukua kwa mwanadamu katika wakati na maeneo tofauti. Ni kazi inayofanywa hatua kwa hatua, na haikamilishwi katika hatua moja. Na kwa hiyo, hekima yote ya Mungu imejumuishwa katika hatua tatu, badala ya hatua moja. Nafsi yake yote na hekima yake yote zimewekwa wazi katika hatua hizi tatu, na kila hatua ina nafsi Yake, na ni rekodi ya hekima ya kazi Yake. Mwanadamu anapasa kujua tabia yote ya Mungu iliyoonyeshwa katika hatua hizi tatu. Nafsi hii ya Mungu ndiyo ina maana zaidi kwa wanadamu wote, na ikiwa watu hawana maarifa haya wanapomwabudu Mungu, basi hawana tofauti na wale wanaoabudu Budha. Kazi ya Mungu kati ya wanadamu haijafichiwa mwanadamu, na inapaswa kujulikana na wale wote wanaomwabudu Mungu. Kwa sababu Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi ya wokovu kati ya wanadamu, mwanadamu anapaswa kujua maonyesho ya kile ambacho anacho na alicho wakati wa hatua hizi tatu za kazi. Hili ndilo ambalo ni lazima lifanywe na mwanadamu. Kile ambacho Mungu anamfichia mwanadamu ni kile ambacho mwanadamu hawezi kutimiza, na kile ambacho mwanadamu hapaswi kujua, ilhali yale Mungu anayomfunulia mwanadamu ni yale ambayo mwanadamu anapaswa kujua na yale ambayo mwanadamu anapaswa kumiliki. Kila moja ya hatua tatu za kazi huendelea juu ya msingi wa hatua iliyopita; haitekelezwi peke yake, tofauti na kazi ya wokovu. Ingawa kuna tofauti kubwa katika enzi na aina ya kazi ambayo inafanywa, katika kiini chake bado ni wokovu wa mwanadamu, na kila hatua ya kazi ya wokovu ina kina kuliko iliyopita. Kila hatua inaendelea kutoka kwa msingi wa hatua ya mwisho ambayo haiondolewi. Kwa njia hii, katika kazi Yake ambayo daima huwa mpya na kamwe si kuukuu, Mungu mara kwa mara anaonyesha kipengele cha tabia yake ambayo hayajawahi kuonyeshwa kwa mwanadamu hapo awali, na daima anamfichulia mwanadamu kazi Yake mpya, na nafsi Yake mpya, na hata ikiwa wazoefu wakongwe wa kidini hufanya juu chini kukinzana na hili, na kulipinga waziwazi, Mungu daima hufanya kazi mpya ambayo anakusudia kufanya. Kazi Yake daima hubadilika, na kwa sababu hili, daima inakabiliwa na upinzani wa mwanadamu. Na hivyo, pia, tabia Yake inabadilika daima, na vilevile enzi na wanaopokea kazi Yake. Zaidi ya hayo, kila mara Yeye hufanya kazi ambayo haijawahi kufanywa tena, hata kufanya kazi ambayo huonekana kwa mwanadamu kuhitilafiana na kazi iliyofanywa awali, kuwa kinyume nayo. Mwanadamu anaweza kukubali tu aina moja ya kazi, ama njia moja ya matendo. Ni vigumu kwa wanadamu kukubali kazi ama njia za matendo, ambayo yanakinzana nao, ama yaliyo juu kuwaliko —lakini Roho Mtakatifu daima anafanya kazi mpya, na kwa hivyo kunakuwepo kikundi baada ya kikundi cha wataalamu wa kidini wanaoipinga kazi mpya ya Mungu. Watu hawa wamekuwa “wataalamu” hasa kwa sababu mwanadamu hana maarifa ya jinsi Mungu huwa mpya wala hazeeki, na zaidi ya hayo, hana maarifa ya kanuni za kazi ya Mungu, na hata zaidi hawana maarifa ya njia nyingi ambazo Mungu humwokoa mwanadamu. Kwa hivyo, mwanadamu kabisa anashindwa kueleza kama ni kazi inayotoka kwa Roho Mtakatifu, au ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Watu wengi hushikilia mtazamo ambao, kama inalingana na maneno yanayokuja kabla, basi wanaweza kuikubali, na kama kuna tofauti na kazi ya awali, basi wanaipinga na kuikataa. Leo, je, nyote hamjafuata katika kanuni hizi? Hatua tatu za kazi ya wokovu hazijakuwa na athari kubwa kwenu, na kuna wale wanaoamini kuwa hatua mbili zilizopita za kazi ni mzigo usiohitaji kufahamika. Wanafikiria kuwa hatua hizi hazifai kutangazwa kwa umati na zinafaa kufutwa haraka iwezekanavyo, ili watu wasihisi kwamba wamezidiwa na hatua mbili za awali za zile hatua tatu za kazi. Wengi wanaamini kuwa kupeana ufahamu kuhusu hatua mbili zilizopita ni hatua ya mbali sana, wala haina faida katika kumjua Mungu—hivyo ndivyo mnavyofikiria. Leo, nyote mnaamini kuwa ni haki kutenda vile, lakini siku itawadia ambapo mtagundua umuhimu wa kazi Yangu: Mjue kuwa Sifanyi kazi yoyote ambayo haina umuhimu. Kwa sababu Ninawatangazia hatua tatu za kazi, kwa hivyo lazima ziwe na faida kwenu; kwa sababu hatua hizi tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, kwa hivyo lazima ziwe lengo la kila mmoja duniani. Siku moja, nyote mtagundua umuhimu wa kazi hii. Fahamuni kuwa mnapinga kazi ya Mungu, ama mnatumia dhana zenu kupima kazi ya leo, kwa sababu hamjui kanuni za kazi ya Mungu, na kwa sababu hamchukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa makini kutosha. Upinzani wenu kwa Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kumetokana na dhana zenu na upumbavu wenu wa kiasili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sawa, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kiasili ya kutotii. Baada ya kupata imani yao katika Mungu, watu wengine hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, ilhali wanathubutu kuzungumza hadharani wakitathmini haki na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na pia wanawakemea mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; utu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote. Je, si siku itawadia ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumwagiza Mungu jinsi atakavyofanya kazi. Je, ni kwa namna gani watu hawa wasio na busara watamjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati anapomtafuta na anapokuwa na uzoefu naye; si katika kumkosoa kwa ghafla ndipo anapokuja kumjua Mungu kwa kupitia kutiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kadri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, Ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, asili yako ya zamani, na utu wako, tabia na maadili ndiyo “mtaji” ambao unampingia Mungu, na kadri unavyokuwa mpotevu, ama ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale waliomilikiwa na dhana kali na wenye tabia ya unafiki wamo hata zaidi katika uadui wa Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo. Ikiwa dhana zako hazitarekebishwa, basi daima zitakuwa kinyume na Mungu; daima hutalingana na Mungu, na daima utakuwa mbali na Yeye.
Ni katika kuweka dhana zako za kale kando tu ndipo utakapoweza kupata maarifa mapya, ilhali maarifa ya zamani si lazima yawe dhana za zamani. “Dhana” inamaanisha vitu vinavyodhaniwa na mwanadamu ambavyo viko mbali na uhalisi. Kama maarifa ya zamani yalikuwa yamepitwa na wakati katika enzi ya kale, na yalimzuia mwanadamu kuingia katika kazi mpya, basi maarifa kama yale pia ni dhana. Ikiwa mwanadamu ataweza kuchukua mwelekeo mzuri kwa maarifa kama yale, na anaweza pata kumjua Mungu kutoka kwa vipengele tofauti, kuunganisha ya zamani na mapya, basi maarifa ya kale yatamsaidia mwanadamu, na yatakuwa msingi wa mwanadamu kuingia katika enzi mpya. Funzo la kumjua Mungu linahitaji kwamba uwe stadi wa kanuni nyingi: jinsi ya kuingia kwenye njia ya kumjua Mungu, ukweli gani unapasa kuelewa ili kumjua Mungu, na jinsi ya kufanya dhana zako na asili yako ya asili kutii mipango yote ya kazi mpya ya Mungu. Ukitumia kanuni hizi kama msingi wa kuingia kwenye somo la kumjua Mungu, basi maarifa yako yatakuwa na kina zaidi na zaidi. Kama una maarifa wazi ya hatua tatu za kazi —ambapo ni kusema kwamba, ya mpango mzima wa usimamizi wa Mungu —na ikiwa utaweza kupatanisha hatua mbili za awali na hatua ya sasa, na unaweza kuona kwamba ni kazi iliyofanywa na Mungu Mmoja, basi utakuwa na msingi imara zaidi. Hatua tatu za kazi zilifanywa na Mungu mmoja; haya ndiyo maono makubwa zaidi, na ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Hatua tatu za kazi zingefanywa tu na Mungu Mwenyewe, na hapana mwanadamu yeyote ambaye angeweza kufanya kazi kama hii kwa niaba Yake—ambayo ni kusema kuwa ni Mungu Mwenyewe pekee ambaye angeifanya kazi Yake toka mwanzo hadi leo. Ingawa hatua tatu za kazi ya Mungu zimefanywa katika enzi tofauti na maeneo tofauti, na ingawa kazi ya kila moja ni tofauti, yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kati ya maono yote, hili ndilo kuu zaidi ambalo mwanadamu anapaswa kulijua, na ikiwa litaeleweka kabisa na mwanadamu, basi ataweza kusimama imara. Leo, tatizo kuu linaloyakumba madhehebu yote na vikundi vya dini ni kwamba hayajui kazi ya Roho Mtakatifu, na hayana uwezo wa kutofautisha kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi isiyo ya Roho Mtakatifu—na kwa hivyo hawawezi kueleza kama hatua hii ya kazi, kama hatua mbili za awali, pia zimefanywa na Yehova Mungu. Ingawa watu wanamfuata Mungu, wengi hawawezi kueleza kama ni njia sahihi. Mwanadamu anahofia ikiwa hii ndiyo njia inayoongozwa na Mungu Mwenyewe , na kama Mungu kupata mwili ni jambo la hakika, na watu wengi bado hawana dokezo jinsi ya kupambanua ikifikia maneno kama haya. Wale wanaomfuata Mungu hawawezi kujua njia, na kwa hivyo habari zinazozungumzwa zinaathiri sehemu ndogo tu kati ya watu hawa na hayana uwezo wa kufaa kikamilifu, na kwa hivyo, hili basi linaathiri maisha ya watu kama hawa. Ikiwa mwanadamu anaweza kuona katika hatua tatu za kazi kuwa zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe wakati tofauti, katika maeneo tofauti, na kwa watu tofauti, basi mwanadamu ataona kuwa,[a] ingawa kazi ni tofauti, yote imefanywa na Mungu mmoja. Kwa kuwa ni kazi ambayo imefanywa na Mungu mmoja, basi lazima iwe sawa, na bila dosari, na ingawa halingani na dhana za mwanadamu, hakuna kupinga kuwa ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Ikiwa mwanadamu anaweza kusema kwa hakika kuwa ni kazi ya Mungu mmoja, basi dhana zake zitakuwa duni, na ambazo hazifai kutajwa. Kwa sababu maono ya mwanadamu hayako wazi, na mwanadamu anamjua Mungu tu kama Yehova, na Yesu kama Bwana, na ana mitazamo miwili kumhusu Mungu mwenye mwili wa leo, watu wengi wamejitoa kwa ajili ya kazi ya Yehova na Yesu, na wamezingirwa na dhana kuhusu kazi ya leo, watu wengi daima huwa na shaka na hawachukulii kazi ya leo kwa makini. Mwanadamu hana uelewa kuhusu hatua mbili za mwisho, ambazo hazikuonekana. Hili ni kwa sababu mwanadamu haelewi uhalisi wa hatua mbili za mwisho kazi, na wala hakuzishuhudia binafsi. Ni kwa sababu haziwezi kuonekana ndiyo mwanadamu anawaza jinsi anavyopenda; bila kujali atakayodhania, hakuna ukweli wa kudhibitisha, na yeyote wa kurekebisha. Mwanadamu anaruhusu silika yake ya asili itawale, huku akikosa kujali na kuachilia mawazo yake yaende popote, kwa kuwa hakuna ukweli wa kudhibitisha, na kwa hivyo dhana za mwanadamu zinakuwa “ukweli,” bila kujali kama zina dhibitisho. Kwa hivyo mwanadamu anaamini Mungu wake aliyemuwazia akilini mwake, na hamtafuti Mungu wa uhalisi. Ikiwa mtu mmoja ana aina moja ya imani, basi kati ya watu mia moja kuna aina mia moja za imani. Mwanadamu ana imani kama hizi kwa maana hajaona uhalisi wa kazi ya Mungu, kwa sababu amesikia tu kwa masikio yake na hajaona kwa macho yake. Mwanadamu amesikia hekaya na hadithi —lakini amesikia kwa nadra kuhusu maarifa ya ukweli ya kazi ya Mungu. Ni katika dhana zao ndivyo watu ambao wamekuwa waumini kwa mwaka mmoja tu wanaamini Mungu, na hilo ni kweli pia kwa wale ambao wamemwamini Mungu katika maisha yao yote. Wale ambao hawawezi kuona ukweli daima hawawezi kuepuka imani ambayo wana dhana kwazo kumhusu Mungu. Mwanadamu anaamini kuwa amejiweka huru kutokana na vifungo vya dhana zake za kale, na ameingia eneo jipya. Je, mwanadamu hajui kuwa maarifa ya wale wasioweza kuona uso wa kweli wa Mungu kuwa ni dhana na tetesi? Mwanadamu anafikiria kuwa dhana zake ni sawa, na wala hayana kasoro, na hufikiri kuwa hizi dhana zimetoka kwa Mungu. Leo, mwanadamu anaposhuhudia kazi ya Mungu, anaachilia dhana zilizokuwa zimeongezeka kwa miaka mingi. Mawazo na dhana za awali zinakuwa vizuizi vya kazi ya hatua hii, na inakuwa vigumu kwa mwanadamu kuachana na dhana kama hizo na kupinga mawazo kama yale. Dhana kuhusu kazi hii ya hatua kwa hatua ya wengi wa wale wanaomfuata Mungu hadi leo zimekuwa ya kuhuzunisha na watu hawa wamefanya uadui wa kikaidi na Mungu mwenye mwili hatua kwa hatua, na chanzo cha chuki ni mawazo na dhana za mwanadamu. Ni hasa kwa sababu ukweli haumruhusu mwanadamu kuwa na uhuru wa hiari ya mawazo yake, na, zaidi ya hayo, hauwezi kupingwa na mwanadamu kwa urahisi, na mawazo na dhana za mwanadamu hazistahimili uwepo wa ukweli, na hata zaidi ya hayo, kwa sababu mwanadamu hawezi kufikiria kuhusu usahihi na unyofu wa ukweli, na kwa nia moja tu huachilia mawazo yake, na hutumia dhana yake, kwamba dhana na mawazo ya mwanadamu zimekuwa adui wa kazi ya leo, kazi ambayo haiambatani na dhana za mwanadamu. Hili linaweza kusemwa kuwa kasoro ya dhana za mwanadamu, na wala si dosari ya kazi ya Mungu. Mwanadamu anaweza kufikiria lolote atakalo, lakini hawezi teta kwa ajili ya hatua yoyote ya kazi ya Mungu au hata sehemu yoyote; ukweli wa kazi ya Mungu hauwezi kukiukwa na mwanadamu. Unaweza kuruhusu mawazo yako yatawale, na unaweza pia kujumuisha hadithi nzuri kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, lakini kamwe huwezi kupinga ukweli wa kila hatua ya kazi ya Yehova na Yesu; hii ni kanuni, na pia ni amri ya utawala, na mnapaswa kuelewa umuhimu wa masuala haya. Mwanadamu anaamini kuwa hatua hii ya kazi hailingani na dhana za mwanadamu, na hivi sivyo katika hatua mbili zilizopita za kazi. Katika mawazo yake, mwanadamu anaamini kuwa kazi ya hatua mbili zilizopita kwa hakika si sawa na kazi ya leo —lakini je, umewahi kufikiria kuwa kanuni zote za kazi ya Mungu ni sawa, na kuwa kazi Yake huwa vitendo daima, na kuwa, bila kujali enzi, daima kutakuwa na halaiki ya watu wanaokataa na kuupinga ukweli wa kazi Yake? Wale wote ambao leo wanakataa na kuipinga hatua hii ya kazi bila shaka wangempinga Mungu wakati uliopita, kwa kuwa watu kama hawa daima watakuwa adui za Mungu. Watu wanaoujua ukweli wa kazi ya Mungu wataona hatua tatu za kazi kama kazi ya Mungu mmoja, na watatupilia mbali dhana zao. Hawa ni watu wanaomjua Mungu, na watu kama hawa ndio kwa kweli humfuata Mungu. Wakati ambapo usimamizi mzima wa Mungu utakaribia kufika mwisho, Mungu ataweka vitu vyote kulingana na aina. Mwanadamu aliumbwa kwa mikono ya Muumba, na mwishowe lazima kabisa amrudishe mwanadamu chini ya utawala Wake; huu ndio mwisho wa hatua tatu za kazi. Hatua ya kazi ya siku za mwisho, na hatua mbili zilizopitwa katika Israeli na Yudea, ni mpango wa Mungu wa usimamizi katika dunia nzima. Hakuna anayeweza kupinga hili, na ni ukweli wa kazi ya Mungu. Ingawa watu hawajapata uzoefu ama kushuhudia kazi zake nyingi, ukweli unabaki kuwa ukweli, na hauwezi kukanwa na mwanadamu yeyote. Watu wanaomwamini Mungu katika nchi zote duniani watakubali hatua tatu za kazi. Kama wajua tu hatua moja ya kazi, na huelewi hatua nyingine mbili za kazi, na huelewi kazi ya Mungu katika wakati uliopita, basi huwezi kuongea ukweli wa mpango mzima wa usimamizi wa Mungu, na maarifa yako ya Mungu yameegemea upande mmoja, kwa kuwa katika imani yako katika Mungu humfahamu, ama kumwelewa, na kwa hivyo hustahili kutoa ushuhuda wa Mungu. Bila kujali kama maarifa yako ya sasa ya mambo haya yana kina kirefu ama cha juujuu tu, mwishowe, lazima muwe na maarifa, na ushawishike kabisa, na watu wote wataona uzima wa kazi ya Mungu na kunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Mwishoni mwa kazi hii, madhehebu yote yatakuwa moja, viumbe wote watarejea chini ya utawala wa Muumba, viumbe wote watamwabudu Mungu mmoja wa kweli, na madhehebu yote yatakuwa bure, na hayataonekana tena.
Mbona mfululizo huu wa marejeo yanayohusu hatua tatu za kazi? Kupita kwa enzi, maendeleo ya kijamii, na uso wa asili unaobadilika yote hufuata mabadiliko katika hatua tatu za kazi. Mwanadamu hubadilika kwa wakati na kazi ya Mungu, na wala hakui peke yake mwenyewe. Kutajwa kwa hatua tatu za kazi ya Mungu ni kwa ajili ya kuleta viumbe wote, na watu kutoka dini zote, chini ya utawala wa Mungu mmoja. Bila kujali wewe ni wa dini gani, mwishowe nyote mtanyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu anayeweza kufanya kazi hii; haiwezi kufanywa na kiongozi yeyote wa kidini. Kuna dini kadhaa kuu duniani, na kila moja ina kichwa, ama kiongozi, na wafuasi wameenea katika nchi tofauti tofauti na maeneo yote duniani; kila nchi, iwe ndogo au kubwa, ina dini tofauti tofauti ndani yake. Hata hivyo, bila kujali ni dini ngapi zilizo duniani, watu wote wanaoishi duniani mwishowe wanaishi katika uongozi wa Mungu mmoja, na uwepo wao hauongozwi na viongozi wa kidini au vichwa. Ambayo ni kusema kwamba wanadamu hawaongozwi na kiongozi yeyote wa kidini ama kiongozi; badala yake wanadamu wote wanaongozwa na Muumba, aliyeziumba mbingu na nchi, na vitu vyote, na ambaye aliwaumba wanadamu —na huu ni ukweli. Hata ingawa dunia ina dini kadhaa kuu, bila kujali jinsi zilivyo kuu, zote zipo chini ya utawala wa Muumba, na hakuna inayoweza kuzidi wigo wa mamlaka hii. Maendeleo ya wanadamu, maendeleo ya kijamii, maendeleo ya sayansi ya asili — kila moja haitengani na mipango ya Muumba, na kazi hii sio kitu kinachoweza kufanywa na uongozi fulani wa dini. Viongozi wa dini ni viongozi tu wa dini fulani, na hawawezi kuwakilisha Mungu, ama Yule aliyeziumba mbingu na nchi na vitu vyote. Viongozi wa kidini wanaweza kuongoza wale wote walio katika dini yote, lakini hawawezi kuamrisha viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu – huu ni ukweli uliokubalika ulimwenguni. Viongozi wa dini ni viongozi tu, na hawawezi kuwa sawa na Mungu (Muumba). Vitu vyote vi mikononi mwa Muumba, na mwishowe vyote vitarejea mikononi mwa Muumba. Mwanadamu kiasili aliumbwa na Mungu, na haijalishi dini, kila mtu atarejea katika utawala wa Mungu— hili haliwezi kuepukika. Ni Mungu tu Aliye Juu Zaidi kati ya vitu vyote, na mtawala mkuu kati ya viumbe wote lazima pia warejee chini ya utawala Wake. Bila kujali mwanadamu ana hadhi ya juu kiasi gani, hawezi kumfikishwa mwanadamu kwenye hatima inayomfaa, wala hakuna anayeweza kuainisha kila kitu kulingana na aina. Yehova mwenyewe alimuumba mwanadamu na kumwainisha kila mmoja kulingana na aina na siku ya mwisho itakapowadia bado Atafanya kazi Yake Mwenyewe, kuanisha kila kitu kulingana na aina—hili haliwezi kufanywa na mwingine isipokuwa Mungu. Hatua tatu za kazi ambazo zilifanywa tangu mwanzo hadi leo zote zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe, na zilitekelezwa na Mungu mmoja. Ukweli wa hatua tatu za kazi ni ukweli wa uongozi wa Mungu kwa wanadamu wote, ukweli ambao hakuna anayeweza kuupinga. Mwishoni mwa hatua tatu za kazi, vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina na kurejea chini ya utawala wa Mungu, kwa kuwa duniani kote kuna Mungu mmoja tu, na hakuna dini nyingine. Yule asiyeweza kuiumba dunia hataweza kuiangamiza, ilhali Yule aliyeumba dunia hakika ataiangamiza, na kwa hivyo, kama mtu hana uwezo wa kutamatisha enzi na ni wa kumsaidia mwanadamu kukuza akili zake tu, basi hakika hatakuwa Mungu, na hakika hatakuwa Bwana wa mwanadamu. Hataweza kufanya kazi kuu kama hii; kuna mmoja tu anayeweza kufanya kazi kama hii, na wote wasioweza kufanya hii kazi hakika ni adui wala si Mungu. Kama ni madhehebu, basi hawalingani na Mungu, na kama hawaligani na Mungu basi wao ni adui za Mungu. Kazi yote inafanywa na huyu Mungu mmoja wa kweli, na ulimwengu mzima unatawaliwa na huyu Mungu mmoja. Bila kujali kama anafanya kazi Uchina ama Israeli, bila kujali kama kazi inafanywa na Roho ama mwili, yote hufanywa na Mungu Mwenyewe, na haiwezi kufanywa na mwingine yeyote. Ni kabisa kwa sababu Yeye ni Mungu wa wanadamu wote ndiyo kwamba Yeye hufanya kazi kwa njia ya uhuru, pasipo kuwekewa masharti yoyote—na haya ndiyo maono makuu zaidi. Kama kiumbe wa Mungu, kama ungependa kutekeleza jukumu la kiumbe wa Mungu na kuelewa mapenzi ya Mungu, lazima uelewe kazi ya Mungu, lazima uelewe mapenzi ya Mungu kwa viumbe, lazima uelewe mpango wake wa usimamizi, na lazima uelewe umuhimu wote wa kazi Anayofanya. Wale wasioelewa hivi hawajahitimu kuwa viumbe wa Mungu! Kama kiumbe wa Mungu, kama huelewi ulikotoka, huelewi historia ya mwanadamu na kazi yote iliyofanywa na Mungu, na, hata zaidi, huelewi jinsi mwanadamu ameendelea hadi leo, na huelewi ni nani anayeamuru wanadamu wote, basi huna uwezo wa kutekeleza wajibu wako. Mungu amemwongoza mwanadamu hadi leo, na tangu alipomuumba mwanadamu duniani hajawahi kumwacha. Roho Mtakatifu daima haachi kufanya kazi, hajawahi kuacha kumwongoza mwanadamu, na hajawahi kumwacha. Lakini mwanadamu hatambui kuwa kuna Mungu, pia hamjui Mungu, na je, kuna jambo la kufedhehesha zaidi kuliko hili kwa viumbe wote wa Mungu? Mungu binafsi humwongoza mwanadamu, lakini mwanadamu haelewi kazi ya Mungu. Wewe ni kiumbe wa Mungu, ilhali huelewi historia yako mwenyewe, na wala hujui ni nani aliyekuongoza katika safari yako, hutambui kazi iliyofanywa na Mungu, na kwa hivyo huwezi kumjua Mungu. Ikiwa hujui sasa, basi hutawahi kuhitimu kutoa ushuhuda kwa Mungu. Leo, Muumba binafsi huwaongoza watu wote kwa mara nyingine, na kuwafanya watu wote kuona hekima yake, uweza, wokovu, na kustaajabisha kwake. Ilhali bado hujatambua au kuelewa—na kwa hivyo, je, si wewe ndiwe utakayekosa kupokea wokovu? Wale walio wa Shetani hawaelewi maneno ya Mungu, na wale walio wa Mungu wanaweza kusikia sauti ya Mungu. Wale wote wanaotambua na kuelewa maneno Ninayozungumza ni wale watakaookolewa, na kumshuhudia Mungu; wote wasioelewa maneno Ninayoyazungumza hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu, na ni wale watakaoondolewa. Wale wasioyaelewa mapenzi ya Mungu na hawaitambui kazi ya Mungu hawawezi kupata maarifa ya Mungu, na watu kama hawa hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu. Kama ungependa kumshuhudia Mungu, basi lazima umjue Mungu, na maarifa ya Mungu yanapatikana kwa kupitia kazi ya Mungu. Kwa ufupi, kama ungependa kumjua Mungu, basi lazima ujue kazi ya Mungu: Kufahamu kazi ya Mungu ndilo jambo la umuhimu kabisa. Hatua tatu za kazi zitakapofikia tamati, patafanyika kundi la watu wanaomshuhudia Mungu, kundi la wale wanaomjua Mungu. Watu hawa wote watamjua Mungu na wataweza kuonyesha ukweli kwa matendo. Watakuwa na utu na hisia, na wote watajua hatua tatu za kazi ya wokovu ya Mungu. Hii ndiyo kazi ambayo itatekelezwa mwishowe, na watu hawa ndio dhihirisho la kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi, na ndio ushuhuda wenye nguvu zaidi kwa kushindwa kwa Shetani. Wale wanaoweza kumshuhudia Mungu wataweza kupokea ahadi na baraka za Mungu, na litakuwa ndilo kundi litakalosalia pale mwisho kabisa, lile linalomiliki mamlaka ya Mungu na lililo na ushuhuda wa Mungu. Pengine wale kati yenu wanaweza wote kuwa sehemu ya kundi hili, ama pengine nusu tu, ama wachache tu —inategemea radhi yenu na ufuatiliaji wenu.
Alhamisi, 10 Agosti 2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli
Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yalivyo, kukamilisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote walioingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote waliokuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Anayotamani kufanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuuliza kuhusu maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu Atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, kwa hivyo wote wanaokubali kazi ya mwisho ya Mungu ni wale watakaotakaswa na Mungu. Kwa hali nyingine, wale wote wanaoikubali kazi ya mwisho ya Mungu ni wale watakaohukumiwa na Mungu.
Kama ilivyozungumziwa awali, hukumu ingeanza na nyumba ya Mungu. “Hukumu” hii inarejelea hukumu ambayo Mungu hutoa leo hii kwa wale wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi siku za mwisho. Pengine kuna wale wanaoamini katika mawazo ya kimiujiza kama yale ya kuwa siku za mwisho zitakapowadia, Mungu Ataandaa meza kubwa mbinguni, ambako kitambaa cheupe kitatandikwa, kisha Mungu Ataketi kwenye kiti kikuu cha enzi na wanadamu wote watapiga magoti ardhini. Kisha Mungu Atafunua dhambi zote zilizowekwa dhidi ya kila mwanadamu kubainisha iwapo atapaa juu mbinguni ama atatupwa chini kwenye ziwa la moto wa jehanamu. Haijalishi mawazo ya mwanadamu yalivyo, kiini cha kazi ya Mungu hakiwezi kubadilishwa. Mawazo ya mwanadamu ni miundo ya fikra za mwanadamu tu na zinatoka kwenye ubongo wa mwanadamu, na zimetungwa na kuunganishwa kutokana na mambo aliyoyaona na kuyasikia. Kwa hivyo Ninasema, kwa vyovyote vile picha zilizowazwa ziwe za hali ya juu kiasi gani, hizo ni kama mchoro tu na haziwezi kubadilishwa na mpango wa kazi ya Mungu. Isitoshe, mwanadamu mzima amepotoshwa na Shetani, sasa atawezaje kuyaelewa mawazo ya Mungu? Mwanadamu huiona kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya ajabu mno. Mwanadamu anaamini kwamba kwa sababu ni Mungu Mwenyewe Anayefanya kazi ya kuhukumu, basi lazima ni ya kiwango cha juu zaidi na isiyoeleweka kwa wanadamu wenye mwili wa kufa; lazima inasikika katika mbingu yote na kutetemesha dunia, vinginevyo, itakuwaje kazi ya hukumu ya Mungu? Mwanadamu anaamini kuwa kwa maana hii ni kazi ya hukumu, basi lazima Mungu ni wa kuvutia na wa adhimu Anapofanya kazi, na wale wanaohukumiwa wanalia kwa sauti wakitoa machozi wakiwa kwenye magoti wakiomba msamaha. Onyesho hili lazima ni la kuvutia na la kusisimua mno…Kila mwanadamu huona kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya ajabu. Je, unajua kwamba muda mrefu baada ya Mungu kuanza kazi ya kuhukumu miongoni mwa wanadamu, wewe bado umestarehe usingizini? Je, unajua kwamba, wakati ambao unadhani kuwa kazi ya hukumu ya Mungu imeanza rasmi, utakuwa tayari umewadia wakati ambapo Mungu Anazibadili mbingu na nchi? Wakati huo, pengine utakuwa tu umeelewa maana ya maisha, lakini kazi ya adhabu ya Mungu isiyo na huruma itakuleta kuzimu, ukiwa bado usingizini. Hapo ndipo kwa ghafla utafahamu kuwa kazi ya hukumu ya Mungu itakuwa imeshakamilika.
Tusipoteze muda wa thamani tukizungumzia mada hizi za kuchukiza. Badala yake, tuzungumzie kinachofanyiza hukumu. Ikifika kwa neno “hukumu,” utawaza juu ya maneno yote ambayo Yehova Alizungumza juu ya kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu Aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno haya ni yale ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, kumaanisha, mandhari tofauti, na ni tofauti kabisa na yale maneno Anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo Anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufunua kiini cha mwanadamu, na kuchunguza maneno na matendo ya mwanadamu. Maneno haya yanajumuisha kweli mbali mbali, kama vile jukumu la mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida kikamilifu, na pia hekima na asili ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yanalenga nafsi na asili potovu ya mwanadamu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu anavyomkataa Mungu kwa dharau, yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu za adui dhidi ya Mungu. Mungu Anapofanya kazi ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu, bali Anatoa ufunuo, na kushughulika naye na kumpogoa kwa muda mrefu. Namna hii ya ufunuo, kushughulika na kupogoa haiwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Kazi kama hii pekee ndiyo huchukuliwa kama hukumu; na kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kushawishiwa, na kugeuzwa mawazo na kujisalimisha kwa Mungu, na kufaidi ufahamu kamili wa Mungu. Kazi ya hukumu humletea mwanadamu kuelewa kwa uso wa kweli wa Mungu na pia ukweli kuhusu uasi wa mwanadamu. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, ufahamu wa makusudi ya kazi ya Mungu, na pia ufahamu wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na mizizi ya upotovu huo, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu. Usipouchukulia ukweli huu kama muhimu na kila mara kufikiri kuuepuka au kutafuta njia nyingine isipokuwa ukweli, basi Ninasema kuwa wewe ni mtenda dhambi mkubwa. Iwapo una imani kwa Mungu, lakini hutafuti ukweli au mapenzi ya Mungu, wala hupendi njia inayokuleta karibu na Mungu, basi Nakwambia kuwa wewe ni mmoja anayejaribu kuepuka hukumu. Wewe ni kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti kikuu cheupe cha enzi, na Mungu Hatawasamehe waasi wowote wanaotoroka kutoka machoni Pake. Wanadamu wa aina hii watapokea adhabu kali zaidi. Wale wanaokuja mbele za Mungu ili wahukumiwe, na wametakaswa wataishi milele katika ufalme wa Mungu. Bila shaka, hii ni katika siku za usoni.
Kazi ya hukumu ni kazi Yake Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe cha nyama Anayepaswa kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu. Wengi wana ladha ya shubiri mdomoni kuhusu nafsi ya pili ya Mungu, kwa maana mwanadamu huona vigumu kuamini ya kwamba Mungu atafanya kazi ya hukumu akiwa na mwili. Lakini lazima Nikueleze kwamba mara nyingi kazi ya Mungu huzidi matarajio ya mwanadamu na ni vigumu kwa mawazo yao kukubali. Kwa maana wanadamu ni mabuu kwenye ardhi, ilhali Mungu ni mkuu Anayejaza ulimwengu mzima; mawazo ya mwanadamu ni kama shimo la maji machafu ambayo yanazalisha mabuu peke yake, ilhali kila hatua ya kazi inayoelekezwa na mawazo ya Mungu ni matunda ya hekima ya Mungu. Mwanadamu hutaka kila wakati kushindana na Mungu; kwa hivyo Nasema ni wazi kuwa ni nani yuko katika nafasi ya kupoteza mwishowe. Kwa hivyo Nawasihi nyote msijichukue kuwa wa maana zaidi kushinda dhahabu. Ikiwa wengine wanaweza kukubali hukumu ya Mungu, ni kwa nini wewe usiikubali? Unasimama kiwango kipi juu ya wengine? Iwapo wengine wanaweza kuinamisha vichwa vyao mbele ya ukweli, ni kwa nini usifanye vile pia? Mwelekeo mkuu wa kazi ya Mungu hauwezi kukomeshwa. Hatarudia kazi ya hukumu tena kwa sababu ya “kustahili” kwako, na utajuta kwa uchungu kupoteza nafasi nzuri kama hiyo. Usipoyaamini maneno Yangu, basi kingoje kiti cheupe kikuu cha enzi kilicho angani “kipitishe hukumu” juu yako! Lazima ujue kwamba Waisraeli wote walimkataa kwa dharau na kumkana Yesu, ilhali uhakika wa ukombozi wa Yesu kwa wanadamu ulizidi kusambaa mpaka mwisho wa ulimwengu. Je, hili silo jambo ambalo Mungu tayari Amelitimiza? Iwapo bado unangoja Yesu Aje Akupeleke mbinguni, basi Nasema kuwa wewe ni mti mkavu.[a] Yesu Hatamkubali mfuasi bandia kama wewe asiye mwaminifu kwa ukweli na anayetafuta baraka pekee. Badala yake, Hataonyesha huruma Anapokutupa kwenye ziwa la moto uungue kwa makumi ya maelfu ya miaka.
Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kupendwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi inayodumu milele. Mungu Hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidai uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao wataona adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi na mwili. Je, hii haiweki wazi haki ya hali halisi ya Mungu? Je, hii siyo sababu kamili ya hukumu ya Mungu na ufunuo wa mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu Atawaweka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali roho wa uovu huishi ili miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao itatoa harufu ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, wafuasi wanafiki, na wafanyakazi bandia, kisha wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu ili miili yao inajisiwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawakuwa waaminifu mpaka mwisho watahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio. Mwishowe, Mungu Atawaangamiza. Mungu Huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, na zaidi ya hayo hawatapata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimika kuhusiana na Mungu watahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio watapona, na wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu Ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vile vile waliopangiwa na Mungu kuwa makuhani. Haya ndiyo matunda Anayopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa makafiri. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yenu itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu haimsubiri yeyote asiyeweza kuwa katika hatua moja na Mungu, na asili ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma.
Jumatano, 9 Agosti 2017
Mwenyezi Mungu|Ngurumo Saba Zatoa Sauti - Zikitabiri Kuwa Injili Ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni
Mimi hueneza kazi Yangu katika mataifa. Katika ulimwengu mzima unang’aa utukufu Wangu; mapenzi Yangu yamo katika mtawanyiko wa wanadamu, wote wakiongozwa kwa mkono Wangu na kufanya kazi Ninayosambaza. Kuanzia sasa, Ninaingia enzi mpya na kuleta watu wote katika ulimwengu mwingine. Ninaporudi katika "nchi Yangu," Ninaanza sehemu nyingine ya kazi katika mpango Wangu wa awali ili mwanadamu aje kujua zaidi kunihusu. Nauchukua ulimwengu katika ukamilifu wake na kuona kwamba[a] ni wakati muafaka wa kazi Yangu, hivyo Mimi Nasafiri huku na kule kufanya kazi Yangu mpya ndani ya mwanadamu. Ni enzi mpya, licha ya yote, na Ninaleta kazi mpya ili niwachukue watu wapya zaidi katika enzi mpya na kuwatupa kando zaidi ya wale Nitakaowaondoa. Katika taifa la joka kubwa jekundu, Ninatekeleza hatua ya kazi isiyoweza kueleweka na mwanadamu na kuwafanya kutingika katika upepo, ambapo baadaye wengi kwa kimya watabebwa na upepo unaovuma. Huu ni "uwanja wa kupura" Ninaotaka kuusafisha; ni kile Ninachotamani na pia ni mpango Wangu. Kwa maana wengi waovu kwa kimya wameingia ndani wakati wa kazi Yangu, lakini Sina haraka ya kuwafukuza. Badala yake, Nitawatawanya wakati utakapofika. Ni baada ya hapo tu ndipo Nitakapokuwa chemchemi ya uzima, ili wale wanaonipenda watapata kutoka Kwangu matunda ya mtini na harufu ya maua. Katika nchi ambako Shetani huishi, nchi ya vumbi, hakuna dhahabu safi, ila ni mchanga tu. Kwa sababu ya kukabiliwa na hili, Ninafanya hatua hiyo ya kazi. Lazima ujue kwamba Ninachopata ni safi, dhahabu safi, wala si mchanga. Ni jinsi gani waovu wanaweza kubaki katika nyumba Yangu? Ninawezaje kuruhusu Mbweha kuwa vimelea katika Paradiso Yangu? Ninatumia kila mbinu linaloweza kuwazwa kuwafukuza. Kabla ya mapenzi Yangu kufichuliwa, hakuna anayefahamu Ninachotaka kufanya. Kuchukua fursa hii, Ninawafukuza wale waovu, na wao wanalazimika kuondoka Kwangu. Hili ndilo Mimi huwawafanyia waovu, lakini bado kuna siku ya wao kufanya huduma Kwangu. Hamu ya watu kupata baraka ni nyingi mno; Kwa hivyo Ninageuza mwili Wangu na kuonyesha uso Wangu wa utukufu kwa mataifa ili watu wote waishi katika dunia yao wenyewe na kujihukumu, Ninaposema maneno ambayo ni lazima Niyaseme na kuwasambazia binadamu wanachohitaji. Wakati wanadamu wanapopata fahamu, Nitakuwa kwa muda mrefu Nimeeneza kazi Yangu. Kisha Nitawaeleza wanadamu mapenzi Yangu, na kuanza sehemu ya pili ya Kazi Yangu juu ya wanadamu, kuwaruhusu watu wote wanifuate kwa karibu ili washirikiane na Kazi Yangu, na kuwaruhusu watu kufanya yote katika uwezo wao kufanya Nami kazi Ninayopaswa kufanya.
Hakuna aliye na imani kwamba atauona utukufu Wangu, na Mimi Siwalazimishi. Mimi Nauondoa utukufu Wangu kutoka miongoni mwa watu hao na kuchukua kwa ulimwengu mwingine. Wakati watu wanatubu tena, basi Mimi Nitaonyesha utukufu Wangu kwa zaidi ya wale wanaoamini. Hii ni kanuni ambayo Mimi hufuata katika kazi Yangu. Kwa maana kuna wakati ambapo utukufu Wangu unaondoka Kanaani, na pia kuna wakati ambapo utukufu Wangu unawaacha waliochaguliwa. Aidha, kuna wakati ambapo utukufu Wangu unaiacha dunia nzima, kiasi kwamba itakuwa hafifu na kutumbukia katika giza. Hata nchi ya Kanaani haitaona mwanga wa jua; watu wote watapoteza imani yao, lakini hakuna hata mmoja anayeweza kuiacha harufu nzuri ya nchi ya Kanaani. Nitakapopita katika mbingu mpya na nchi tu ndipo Nitakapofichua sehemu nyingine ya utukufu Wangu kwanza katika nchi ya Kanaani, kuruhusu mwanga kuangazia dunia nzima ikiwa giza kama usiku, ili kwamba dunia nzima iujie mwanga huo. Wacha watu wote duniani kote waje kuteka nguvu za mwanga, kuruhusu utukufu Wangu uongezeke na kuonekana upya kwa mataifa yote. Wacha watu wote watambue kwamba muda mrefu uliopita Nilikuja duniani na muda mrefu uliopita Nilileta utukufu Wangu kutoka Israeli hadi Mashariki; kwa maana utukufu Wangu unang'aa kutoka Mashariki, ambako uliletwa kutoka Enzi ya Neema hadi leo. Lakini Nilitokea Israeli na kutoka huko Nikawasili Mashariki. Wakati mwanga wa Mashariki unapong’aa polepole tu ndipo giza kote duniani linaanza kugeuka na kuwa mwanga, na hapo tu ndipo mwanadamu atatambua kwamba nilishatoka Israeli na Nimeanza kuchomoza upya katika Mashariki. Niliwahi shuka katika Israel na baadaye Niliondoka. Kwa sababu hii, [b] Siwezi tena kuzaliwa huko kwa mara nyingine, kwa ajili kazi Yangu inaongoza ulimwengu mzima na umeme unaangaza kutoka Mashariki kwenda Magharibi. Hii ndiyo sababu Mimi Nimeshuka katika Mashariki na kuwaletea Kanaani watu wa Mashariki. Ningependa kuleta watu kutoka dunia nzima katika nchi ya Kanaani, hivyo Mimi Naendelea kutoa sauti Yangu katika nchi ya Kanaani ili kuudhibiti ulimwengu mzima. Kwa wakati huu, hakuna mwanga katika dunia nzima isipokuwa katika Kanaani, na watu wote wamehatarishwa na njaa na baridi. Niliipa Israeli utukufu Wangu kisha Nikauhamisha mbali na pale, na kuwaleta Waisraeli Mashariki, na kuwaleta watu wote Mashariki. Nimewaelekeza wote kwenye mwanga ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga, wasilazimike kuutafuta tena. Nitawaacha wote wanaotafuta kuuona mwanga tena na kuuona utukufu Niliokuwa nao katika Israeli; Nitawaacha kuona kwamba tayari Nimeshuka chini juu ya wingu jeupe miongoni mwa watu, na kuona mawingu mengi meupe na vishada vya matunda, na zaidi ya hayo, Yehova, Mungu wa Israeli. Nami Nitawaacha waone Mkuu wa Wayahudi, Masihi Aliyengojewa, na kuonekana kamili kwa mimi Niliyeteswa na wafalme katika enzi zote. Nitafanya kazi ya ulimwengu mzima na kufanya kazi kubwa, Nikifichua utukufu Wangu wote na matendo Yangu yote kwa mwanadamu katika siku za mwisho. Nitaonyesha uso Wangu uliojaa utukufu kwa wale wameningoja kwa miaka mingi, kwa wale ambao wametamani kuniona nikija juu ya wingu jeupe, kwa Israeli ambaye amengoja Nionekane kwa mara nyingine tena, na kwa watu wote walionitesa Mimi, ili wote wajue kwamba Mimi kwa muda mrefu uliopita Nimeuchukua utukufu Wangu na kuuleta katika Mashariki. Hauko katika Yudea, kwa maana siku za mwisho tayari zimewadia!
Katika ulimwengu mzima Mimi Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, kutikisa dini zote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo iliyoleta watu katika wakati wa sasa. Nimeiwacha sauti Yangu kuwa inayowashinda wanadamu; wote wanaingia katika mkondo huu na wote wananyenyekea mbele Zangu, kwa maana Mimi kwa muda mrefu uliopita Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote na Nikaupeleka upya Mashariki. Ni nani asiye na hamu ya kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuuona uzuri Wangu? Ni nani asiyetaka kuja kwenye mwanga? Ni nani asiyeona utajiri wa Kanaani? Ni nani asiyengoja kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mkuu Mwenyezi? Sauti Yangu lazima ienee kote duniani; Ningependa kuzungumza zaidi na watu Wangu wateule. Maneno Ninayotamka yanatikisa milima na mito kama radi yenye nguvu; Nasema na ulimwengu wote na kwa watu wote. Hivyo maneno Yangu yanakuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni jinsi kwamba mtu huchukia kuyaacha na pia kuyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote, mwanadamu anayafurahia. Kama watoto wachanga waliozaliwa karibuni, watu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu. Kwa sababu ya sauti Yangu, Nitawaleta watu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia kirasmi kati ya wanadamu ili waje kuniabudu Mimi. Utukufu Ninaotoa na maneno Yangu yatawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki, na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye "Mlima wa Mizeituni" wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari kwa muda mrefu Nimekuwa duniani, si tena Mwana wa Wayahudi lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwa maana ni muda mrefu tangu Nimekwishafufuka, Nimekwenda kutoka miongoni mwa wanadamu, na Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu kwa utukufu. Mimi ndiye Nilichiwa kabla ya enzi, na "mtoto mchanga" aliyeachwa na Israeli kabla ya enzi. Aidha, Mimi ndimi mwenye utukufu wote mtukufu Mwenyezi Mungu wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, kusikia sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vile vile madhumuni ya usimamizi Wangu. Basi kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na kila mtu awe mmoja wa wale walio chini Yangu!
Mwenyezi Mungu| Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kama
mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu
Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya
Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu
kwa jina la Bwana Yesu Kristo - na haya yote sisi hufanya chini ya
utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara
nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote
yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri shahiri
kwamba sisi pia tunajiamini kutembelea njia ya kutii mapenzi ya Baba
aliye mbinguni. Tunatamani kurudi kwake Bwana Yesu, ujaji tukufu wa
Bwana Yesu, kwa mwisho wa maisha yetu hapa duniani, kwa kuonekana kwa
ufalme, na kwa kila kitu kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha
Ufunuo: Bwana anafika, na analeta maafa, na kuwazawadia walio wema na
kuwaadhibu walio waovu, na anawachukua wale wote wanaomfuata na
kukaribisha kurudi Kwake angani kumlaki. Kila wakati tunawaza kuhusu
haya, hatuna budi ila kujawa na hisia. Tunashukuru kwa kuwa
tulizaliwa nyakati za mwisho na tuna bahati ya kutosha ya kushuhudia
kuja kwake Bwana. Ingawa tumepitia mateso, yote ni kwa ajili ya
malipo ya “utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi sana”; hii ni
baraka iliyoje! Hamu hii yote na neema inayopewa na Bwana mara kwa
mara hutufanya kuingia kwenye maombi, na hutuleta pamoja kila mara.
Labda mwaka ujao, labda kesho, au labda hata mapema wakati mwanadamu
hatarajii, Bwana atarejea ghafla, na atatokea kati ya kundi la watu
ambao wamekuwa wakimsubiri kwa umakinifu. Sote tunashindana kati
yetu, hakuna anayetaka kubaki nyuma, ili kuwa kundi la kwanza la
kutazama kuonekana kwa Bwana, na kuwa mmoja ya wale watakaochukuliwa
kwenda mbinguni. Tumetoa kila kitu, bila kujali gharama, kwa ajili ya
kuwadia kwa siku hii. Baadhi yetu wameacha kazi zao, wengine
wameachana na familia zao, wengine kukana ndoa zao, na baadhi yao
hata wamepeana akiba zao zote. Ni upendo usio na ubinafsi wa aina
gani huu! Uaminifu na utiifu kama huu lazima uwe unashinda ule wa
watakatifu wa nyakati za zamani! Kwa kuwa Bwana anavyompa neema
yeyote yule ambaye Yeye anataka, na kumrehemu yeyote ambaye Yeye
anataka, kujitolea kwetu na matumizi yetu, na matumizi yetu,
tunaamini, tayari yametazamika machoni pake. Kwa hivyo, pia, sala
zetu za dhati zimefikia masikio Yake, na tunaamini kuwa Bwana
atatuzawadia kwa ajili ya kujitolea kwetu. Aidha, Mungu aliturehemu
kabla hajauumba ulimwengu, na hakuna atakayenyakua baraka na ahadi
Zake kutoka kwetu. Sote tunapanga kuhusu siku za usoni, na kupuuza
kwamba kujitolea kwetu na kugharamia ni mambo tunayoweza kutumia ili
kuchukuliwa kwenda mbinguni kukutana na Bwana. Pia, bila kusita hata
kidogo, sisi tunajiweka kwenye kiti cha enzi cha siku za baadaye,
tukitawala mataifa na watu wote kwa jumla, ama tunatawala kama
wafalme. Yote haya, sisi huchukulia kama jambo la lazima, kama kitu
kinachotarajiwa.
Tunadharau
wale wote walio kinyume na Bwana Yesu; na mwishowe, wote
wataangamizwa. Nani aliwaambia wasiamini kwamba Bwana Yesu ni
Mwokozi? Bila shaka, kuna wakati tunajifunza kutoka kwa Bwana Yesu na
tunakuwa na huruma kwa dunia, kwa kuwa hawaelewi, na tunapaswa kuwa
wavumilivu na kuwasamehe. Kila kitu tufanyacho ni kwa mujibu wa
mafundisho ya Biblia, kwani kila kitu ambacho hakifuatani na Biblia
ni uzushi, na madhehebu maovu. Imani kama hiyo imehifadhiwa ndani ya
akili zetu. Mola wetu yumo katika Biblia, na tusipoondoka kwenye
Biblia basi hatutaondoka kwa Bwana; tukitii kanuni yake, basi
tutaokolewa. Sisi husaidiana na kuchochea kila mmoja wetu, na kila
wakati tunapokusanyika pamoja ni matumaini yetu kwamba kila kitu
tunachosema na kutenda kinaambatana na matakwa ya Bwana na kuwa
kinaweza kukubaliwa na Bwana. Licha ya uhasama mkubwa ulioko kwenye
mazingira yetu, mioyo yetu imejaa furaha. Tunapowaza kuhusu baraka
hizi tunazoweza kupata kwa urahisi, je, kuna kitu ambacho hatuwezi
kukiacha? Je, kuna kitu ambacho hatuwezi kutengana nacho? Yote haya
ni thabiti, na haya yote yanatazamwa na macho ya Mungu. Sisi, walio
wachache na maskini ambao tumeinuliwa kutoka jaani, ni sawa na
wafuasi wa Bwana Yesu wa kawaida: Tunaota kuhusu kuchukuliwa kwenda
mbinguni, na kubarikiwa, na kutawala mataifa yote. Upotovu wetu
umeanikwa peupe machoni pa Mungu, na tamaa zetu na uchoyo
zinahukumiwa machoni pa Mungu. Bado, yote haya hutokea bila ajabu,
yenye mantiki, na hakuna hata mmoja kati yetu ambaye hushangaa kama
hamu yetu ni ya haki, wala hamna kati yetu ambaye anashuku usahihi wa
yote yale ambayo sisi tunashikilia. Nani anayeweza kujua mapenzi ya
Mungu? Hatujui jinsi ya kutafuta, au kuchunguza, au hata
kujishughulisha na njia ambayo mwanadamu hupitia. Kwa maana sisi
hujali tu kuhusu kama tutaweza kuchukuliwa kwenda mbinguni, kama
tunaweza kubarikiwa, kama kuna pahali tumetengewa kwa ufalme wa
mbinguni, na kama sisi tutaweza kupata mgawo wa maji ya uzima wa mto
wa maisha na matunda ya mti wa uzima. Je, sisi hatumwamini Bwana, na
je, sisi sio wafuasi wake Bwana, kwa ajili ya kupata vitu hivi?
Dhambi zetu zimesamehewa, tumetubu dhambi zetu, tumekunywa kikombe
cha mvinyo ambao ni mchungu, na tumeweka msalaba migongoni mwetu.
Nani anayeweza kusema kuwa gharama ambayo tumelipia haitakubalika na
Bwana? Nani anayeweza kusema kuwa hatujatayarisha mafuta yanayotosha?
Hatutaki kuwa kama wale bikira wapumbavu, ama kama wale ambao
wameachwa. Aidha, tunaomba kila wakati, na kumwomba Bwana atuepushe
kutokana na kudanganywa na Kristo wa uongo, kwa maana imeandikwa
kwenye Biblia kuwa “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazama,
Kristo yupo hapa, au yuko pale; msiamini hili. Kwa maana watatokea
makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na
maajabu; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi.
(Matayo 24: 23-24). Sisi sote tumeweka mistari hii ya biblia kwenye
kumbukumbu, tunazijua aya hizi toka mbele mpaka nyuma, na tunaziona
kama hazina ya thamani, kama maisha, na kama vitambulisho vyetu vya
wokovu wetu na kuchukuliwa kwenda mbinguni kwetu….
Kwa
maelfu za miaka, wanaoishi wamefariki, wakichukua tamaa zao na ndoto
zao, na hakuna anayejua kwa ukweli iwapo wameenda kwa ufalme wa
mbinguni. Wafu wanarudi, na wamesahau hadithi zote zilizotokea wakati
mmoja, na bado wanafuata mafundisho na njia za babu zetu. Kwa hivyo,
miaka inavyopita na siku zinavyosonga, hakuna anayejua iwapo Bwana
Yesu, Mungu wetu, kwa kweli hukubali yote tunayoyafanya. Kwa urahisi,
tunangojea matokeo na kubashiri kuhusu yale yote ambayo yatatokea.
Bado Mungu yu kimya siku zote, na hajawahi kutuonekania, wala kusema
nasi. Na kwa hivyo, kwa hiari yetu tunahukumu mapenzi ya Mungu na
tabia kwa mujibu wa Biblia na ishara. Sisi tumezoea kimya cha Mungu;
tumekuwa na mazoea ya kupima haki na makosa ya tabia zetu kutumia
njia zetu za mawazo: tumekuwa na mazoea ya kutumia elimu yetu, dhana,
na maadili yetu na kuyafanya yachukue nafasi ya matakwa ya Mungu
kwetu sisi; tumekuwa na mazoea ya kufurahia neema ya Mungu; tumekuwa
na mazoea ya Mungu kutoa msaada wakati sisi tunahitaji msaada huo;
tumekuwa na mazoea ya kunyosha mikono yetu kwa Mungu ili tupate mambo
yote, na kumuagiza Mungu; na pia tumekuwa na mazoea ya kufuata
mafundisho ya dini, bila kutilia maanani jinsi Roho Mtakatifu
hutuongoza; zaidi ya hayo, tumekuwa na mazoea ya siku ambazo sisi ni
bwana zetu wenyewe. Tunamwamini Mungu wa namna hii, ambaye hatujawahi
kukutana naye. Maswali kama namna tabia Yake ilivyo, utu wake na mali
yake, mfano wake, kama tutamjua ama hatutamjua wakati atakaporudi, na
kadhalika—haya yote hayana umuhimu. Jambo muhimu ni kuwa Yeye yumo
mioyoni mwetu, na kuwa tunamsubiri, na kuwa tunaweza kufikiria jinsi
Alivyo. Tunathamini imani yetu, na kuthamini hali yetu ya kiroho.
Tunaona kila kitu ni kama samadi, na kukanyaga mambo yote kwa nyayo
zetu. Kwa sababu sisi ni wafuasi wa Bwana mwenye utukufu, bila kujali
jinsi safari yetu ilivyo ndefu na ngumu, bila kujali shida na hatari
inayotukumba, hakuna kitu kitakachosimamisha nyayo tunapomfuata
Bwana. “Mto wa maji safi ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri,
ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo. Na katika
kila upande wa ule mto, ulikuwapo ule mti wa uzima, unaozaa matunda
aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi: Na majani ya
mti huo ni ya kuwaponya mataifa. Wala hapatakuwa na laana tena:
Lakini kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo kitakuwa ndani
yake; na watumwa wake watamtumikia: Nao watauona uso wake; na jina
lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. Na hapatakuwa na usiku
pale; wala hawahitaji mshumaa, wala nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu
huwapa nuru: nao watatawala milele hata na milele (Ufunuo wa Yohana
22:1-5). Kila wakati sisi hukariri maneno hayo, mioyo yetu hujawa na
furaha isiyo na kifani na maridhio pia, na machozi hutiririka kutoka
machoni mwetu. Shukrani ni kwa Bwana kwa kutuchagua, shukrani ni kwa
Bwana kwa neema Yake. Mara mia sasa, yeye ametupa uzima wa milele kwa
ulimwengu ujao, na kama angetuuliza tufe sasa, tungetii amri hiyo
bila kusita hata kidogo. Bwana! Tafadhali njoo hivi karibuni!
Usikawie hata dakika moja tena, kwa kuwa sisi tunakutamani na
tumeacha kila kitu kwa ajili yako.
Mungu
amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake
haijawahi kusimamishwa. Yeye huangalia nchi zote, na huamuru vitu
vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Usimamizi
wake hufanywa hatua kwa hatua na kulingana na mpango wake. Usimamizi
wake huendelea kimya kimya, bila madhara ilhali nyayo zake, daima
hukaribia binadamu, na kiti chake cha hukumu kimeenezwa katika
ulimwengu kwa kasi ya umeme, mara moja kikifuatwa na mshuko wa kiti
chake cha enzi kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, yaani,
tukio hilo ni uwakilishaji wa mandhari kwa makini na wa kuonyesha
Mungu ni mkuu. Kama njiwa na kama simba anayenguruma, Roho anawasili
kati yetu sisi sote. Yeye ni mwenye hekima, Yeye ni mwenye haki na wa
adhimu, Yeye huwasili kati yetu kwa ukimya, na huwasili na mamlaka
akiwa amejazwa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuja
Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo,
hakuna mwanadamu ambaye anajua chote atakachokifanya Yeye. Maisha ya
mwanadamu inabaki ilivyo bila kubadilika; moyo wake hauna tofauti, na
siku zinapita kama kawaida. Mungu anaishi kati yetu kama mtu wa
kawaida, kama mfuasi asiye na maana na pia kama muumini wa kawaida.
Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na vile vile, ana
uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona
kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya
kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila
mipaka au kuogopa, kwa kuwa sisi humwona tu kama muumini wa kawaida
asiye na maana. Yeye huona matukio yetu yote, na fikra na mawazo yetu
yote yanaanikwa wazi mbele Yake. Hakuna mtu ambaye hutilia maanani
uwepo Wake, hamna aliye na mawazo yoyote ya kazi Yake, na zaidi ya
hayo, hakuna mtu ana tuhuma yoyote kuhusu Yeye ni nani. Sisi
huendelea na kazi yetu tu, kana kwamba Yeye hahusiani nasi….
Kwa
bahati, Roho Mtakatifu huonyesha kifungu cha maneno “kupitia”
Kwake, na ingawa inaonekana ni jambo lisilotarajiwa, tunatambua kuwa
huo ni usemi wa Mungu, na tunakubali kwa urahisi kutoka kwa Mungu.
Hii ni kwa sababu, bila kujali ni nani anayeonyesha maneno haya,
ilimradi yanatoka kwa Roho Mtakatifu tunapaswa kuyakubali, na hivyo
hatuwezi kuyakana. Matamshi yajayo yanaweza kuwa kupitia kwangu, au
kwako, ama yanaweza kupitia yeye. Bila kujali ni nani, yote ni neema
ya Mungu. Ilhali bila kujali mtu ni nani, hatufai kumwabudu, kwa kuwa
bila kuzingatia chochote kingine, hawezi kuwa Mungu; hatuwezi kwa
njia yoyote kumchagua mtu wa kawaida kama huyu, kuwa ndiye Mungu
wetu. Mungu wetu ni mkubwa na mwenye kuheshimika; anawezaje
kuwakilishwa na binadamu wa kawaida asiye na umuhimu? Zaidi ya hayo,
sisi wote tunasubiri ujaji wa Mungu kuturudisha kwa ufalme wa
mbinguni, na kwa hivyo mwanadamu asiye na umuhimu mkubwa anawezaje
kuhitimu kufanya kazi ngumu kama hiyo? Bwana akirudi tena, ni lazima
iwe juu ya wingu jeupe, linaloonekana na wote. Huo utakuwa wa adhimu
namna gani! Itakuwaje Awe amejificha kwa ukimya kati ya kundi la watu
wa kawaida?
Na
bado ni huyu mtu wa kawaida aliyefichika kati ya watu ndiye
anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hafafanui chochote kwetu,
wala hatuelezi ni sababu gani Amekuja. Yeye tu, anafanya kazi
anayotarajia kufanya, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na
matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya,
kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu;
kuanzia kutumia sauti ya upole mpaka kutumia maneno makali na ya
adhimu—yote yanatia huruma na hofu kwa mwanadamu. Kila kitu
Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu,
maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha
tukiwa na aibu na wanyonge. Tunaanza kutafakari iwapo Mungu Aliye
katika roho ya huyu mtu kweli anatupenda, na nini hasa Anatarajia
kufanya. Labda tunaweza tu kuchukuliwa kwenda mbinguni baada ya
kuvumilia maumivu kama hayo? Vichwani mwetu tunafanya hesabu…
kuhusu hatima inayokuja na kuhusu majaliwa yetu ya baadaye. Bado
hakuna hata mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu amechukua mwili na
hutenda kazi kati yetu. Japokuwa Amekuwa pamoja nasi kwa muda mrefu,
ingawa tayari Yeye amesema maneno mengi uso kwa uso nasi, bado hatuko
tayari kumkubali mtu aliye wa kawaida kiasi hicho awe Mungu wa
mustakabali wetu, wala hatuna nia ya kumwaminisha mtu asiye na maana
udhibiti wa mustakabali na hatima yetu. Kutoka Kwake, daima
tunafurahia ugavi wa maji ya uhai, na kwa sababu Yake tunaishi uso
kwa uso na Mungu. Sisi tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu aliye
mbinguni, na hatujawahi kamwe kupa umakini hisia za huyu mtu wa
kawaida mwenye kumilikiwa na uungu. Yeye bado, kwa unyenyekevu,
hufanya kazi akiwa amefichwa ndani ya mwili , akielezea sauti ya moyo
wake, bila kuzingatia kukataliwa Kwake na binadamu, inavyoonekana
milele kusamehe utoto na ujinga wa mwanadamu, na milele kuvumilia
mwanadamu kutomheshimu.
Pasipo
sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua baada ya
hatua ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, na hukabiliwa na
kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunajifunza haki ya
Mungu na adhama ya tabia Yake, na kufurahia, upendo na huruma Zake,
tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake,
tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa
mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua asili na
kiini cha Mungu, tunakuja kufahamu mapenzi ya Mungu, tunakuja kujua
asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya
wokovu na ukamilifu. Maneno yake hutufanya sisi tufe, na kutufanya
kuzaliwa upya; maneno yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa
tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno yake hutuletea
furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa. Wakati mwingine sisi ni
kama wanakondoo wa kuchinjwa kwenye mikononi Yake; wakati mwingine
sisi ni kama kipenzi cha roho yake na kufurahia upendo wake na huba
yake; wakati mwingine sisi ni kama adui wake, waliofanywa majivu na
ghadhabu yake katika macho yake. Sisi ni wanadamu waliookolewa Naye,
sisi ni funza machoni pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao
Yeye hufikiria kuhusu kuwapata mchana na usiku. Yeye ni mwenye huruma
kwetu, anatudharau, yeye hutuinua, yeye hutufariji na kutuhimiza,
yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha
nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Yeye hujitia wasiwasi usiku na
mchana kwa ajili yetu, Yeye hutulinda na kututunza usiku na mchana,
na hatuachi kamwe, na Yeye hutoa utunzaji Wake wote kwetu na hulipia
gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa maneno ya mwili huu mdogo
na wa kawaida, tumefurahia ukamilifu wa Mungu, na kuona hatima ambayo
Mungu ametupa. Ila, licha ya haya, majivuno yangali mioyoni mwetu, na
sisi hatuna nia ya kukubali kikamilifu mtu kama huyu kama Mungu wetu.
Ingawa Yeye ametupa mana sana, mengi sana ya kufurahia, hamna kati ya
haya ambayo yanaweza kunyakua nafasi ya mungu katika mioyo yetu.
Tunaheshimu utambulisho maalum wa huyu mwanadamu na hadhi kwa kusita
pekee. Kama Yeye haneni na kutufanya kukiri kwamba Yeye ni Mungu,
basi sisi kamwe hatuwezi kukata kauli wenyewe na kukiri Yeye ni
Mungu, na kuwa Yeye yumo karibu kuja ilhali amekuwa akifanya kazi
kati yetu kwa muda mrefu.
Matamshi
ya mungu yanaendelea, na Yeye hutumia mbinu mbalimbali na mitazamo
kutuonya na kutuelekeza tutakachofanya na kueleza sauti ya moyo Wake.
Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, na hutuonyesha njia tunayopasa
kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na
maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi anavyoongea, na
bila hiari tunaanza kuwa na hamu ya sauti ya moyo wa huyu mwanadamu
asiye wa ajabu. Yeye hufanya juhudi za mchwa kwa ajili yetu,
anapoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa
ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa kwa
ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na
moyo Wake huvuja damu na kulia kwa ajili ya uasi na kufa ganzi kwetu.
Utu kama huu na umiliki Wake haupo kwa upeo wa binadamu wa kawaida,
na hauwezi kumilikiwa na yeyote aliyepotoka. Ana uvumilivu na subira
isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake haumilikiwi na kiumbe
yeyote aliyeumbwa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo
yetu yote, au kufahamu asili yetu ama kiini chetu, ama kuhukumu uasi
wetu na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati
yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu wa mbinguni. Hakuna mtu ila Yeye
anayeweza kumiliki mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya
Mungu na kile Anacho na alicho yametoka, kwa ukamilifu wao, kutoka
Kwake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na
kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia
siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote
isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana utumwa wa shetani ama
upotovu wa tabia yetu potovu Yeye huwakilisha Mungu, na kuonyesha
sauti ya moyo wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya
Mungu, yote ambayo huelekezwa kwa mwanadamu. Ameanza enzi mpya,
nyakati mpya, na akaleta mbingu na nchi mpya, kazi mpya, na
ametuletea matumaini, na akamaliza maisha ambayo si dhahiri, na
akatuwezesha kikamilifu kuona njia ya wokovu. Ameshinda ubinadamu
wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili
zetu zinapata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu
mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na
kwa muda amekuwa akikataliwa na sisi—Je, si Yeye ni Bwana Yesu,
ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, na ambaye tunamtamani usiku na
mchana? Ni Yeye! Ni Yeye Kweli! Yeye ni Mungu wetu. Yeye ndiye kweli,
njia, na uzima! Yeye ameturuhusu kuishi tena, na kuona nuru, na
kusimamisha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu,
tumerejea mbele ya kiti chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na
Yeye, tumeshuhudia uso wake, na tumeona barabara iliyo mbele. Wakati
huo, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye
ni nani tena, wala hatupingi tena kazi na neno lake, na tunasujudu,
kabisa, mbele yake. Hakuna tunachotaka ila kufuata nyayo za Mungu
maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila
yake, na kulipa upendo wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio
yake, na kushirikiana na kazi yake, na kufanya kila kitu tunachoweza
ili kukamilisha kile anachotuaminia.
Kushindwa
na Mungu ni kama mashindano ya kareti.
Kila
neno la Mungu hugonga eneo letu la ubinadamu, na hutuacha tukiwa
tumejawa na huzuni na hofu. Yeye hufichua fikra zetu, hufichua mawazo
yetu, na hufichua tabia zetu potovu. Kupitia kwa yale yote sisi
husema na kuyatenda, na kila wazo na fikra zetu, asili na kiini
zinafunuliwa kwa neno lake, na kutuacha na fedheha, tukitetemeka kwa
hofu. Anatueleza kuhusu matendo yetu yote, malengo yetu na nia, na
hata tabia potovu ambazo hatujawahi kugundua, na kutufanya tuhisi
kwamba tumewekwa hadharani, na hata kuhisi tumeshawishika vikamilifu.
Yeye hutuhukumu kwa ajili ya upinzani wetu Kwake, hutuadibu kwa ajili
ya kufuru kwetu na kumshutumu kwetu, na kutufanya tuhisi kwamba
hatuna thamani machoni pake, na kuwa sisi ni Shetani aishiye.
Matumaini yetu yanakufa, na kamwe hatuwezi kumpa madai yasiyo na
msingi au kumjaribu, na hata ndoto zetu kupotelea mara moja. Huu ni
ukweli ambao hakuna kati yetu anaweza kufikiria, na kwamba hakuna
yeyote kati yetu anayeweza kukubali. Kwa muda, akili zetu hukosa
msimamo, na hatujui tutakavyoendelea na barabara iliyo mbele wala
hatujui jinsi ambavyo tutaendelea katika imani zetu. Inaonekana kama
imani yetu imerudi kama ilivyokuwa mwanzoni, na ya kuwa hatujawahi
kumpata na kumtambua Yesu Kristo.
Kila kitu machoni petu hutushangaza, na kutufanya tuhisi ni kama
tumetupwa mbali. Tunasikitishwa, tunahuzunika, na ndani ya mioyo yetu
kuna ghadhabu ambayo haiwezi kufichika na pia kuna aibu. Tunajaribu
kujieleza, kupata suluhisho, na, hali kadhalika, sisi hujaribu
kuendelea kumsubiri Mwokozi Yesu, na kueleza mioyo yetu mbele yake.
Ingawa kuna wakati mwingine ambao hatuna kiburi wala unyenyekevu kwa
kutazamwa nje, mioyoni mwetu tunateseka na kuwa na hisia ya hasara
kuliko vile tumewahi kuwa nayo. Ingawa wakati mwingine tunaonekana ni
kama tuna utulivu kwa kutazamwa nje, ndani yetu tunavumilia bahari ya
mateso inayopanda na kushuka. Hukumu yake na kuadibu Kwake zimechukua
matumaini na ndoto zetu zote, na kutuacha bila tamaa zetu kuu na
kutokuwa tayari kuamini kuwa Yeye ndiye Mwokozi wetu anayeweza
kutuokoa. Hukumu Yake na kuadibu zimefungua ghuba kubwa kati yetu na
Yeye na hakuna aliye tayari hata kuivuka. Hukumu na kuadibu Kwake ni
mara ya kwanza kwamba sisi tunateseka kwa kupata shida kubwa hivi na
udhalilishaji kiasi kikubwa hivyo. Hukumu na kuadibu Kwake
vimetuwezesha kwa ukweli kuthamini heshima ya Mungu na kutovumilia
kwake kwa makosa ya binadamu, ikilinganishwa na ambavyo sisi ni watu
wa hadhi ya chini na najisi. Hukumu Yake na kuadibu vimetufanya sisi
kutambua kwa mara ya kwanza, jinsi ambavyo tuna kiburi na wenye
majivuno, na jinsi ambavyo mwanadamu kamwe hawezi kulingana na Mungu,
ama kuwa sawa na Mungu. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimetufanya
tutumaini kutoishi katika tabia potovu kama hiyo, na zimetufanya
tutamani kuacha asili kama hiyo na kiini kama hicho haraka
iwezekanavyo, na kamwe tusichukiwe Naye wala tusimchafue moyo. Hukumu
na kuadibu kwake vimetufanya tufurahie kutii neno Lake, na hatumo
tayari kamwe kwenda kinyume na matayarisho na mipangilio yake. Hukumu
na kuadibu Kwake kwa mara nyingine, zimetuwezesha sisi tuwe na tamaa
ya kutafuta uzima, na zimetuwezesha kufurahia kumkubali kama Mwokozi
wetu... Sisi tumetoka nje ya kazi ya ushindi, tumetoka kuzimu,
tumetoka nje ya bonde la uvuli wa mauti.... Mwenyezi Mungu
ametutamalaki, kundi hili la watu! Ameshinda dhidi ya Shetani, na
kuwashinda adui zake!
Sisi
ni kundi la watu wa kawaida waliomilikiwa na tabia potovu ya
kishetani, sisi ndio watu waliochaguliwa na Mungu kabla ya enzi, na
sisi ndio maskini ambao Mungu ameinua kutoka jaani. Kuna wakati
tulipomkataa na kumshutumu Mungu, ila sasa kumeshindwa na Yeye.
Tumepokea maisha na kupokea njia ya uzima wa milele kutoka kwa Mungu.
Bila kujali mahali ambapo tupo hapa duniani, licha ya mateso na
dhiki, hatuwezi kuwa mbali na wokovu wa Mwenyezi
Mungu.
Kwa kuwa Yeye ndiye Muumba wetu, na ukombozi wetu tu!
Upendo
wa Mungu unazidi kuenea kama maji ya chemichemi, na wewe unapewa, na
mimi pia, na kwake, na kwa wale wote ambao wanatafuta ukweli kwa
kweli na kungoja kuonekana kwa Mungu.
Kama
vile daima mwezi hufuata jua, kazi ya Mungu haiishi kamwe, na
inatekelezwa kwako, kwangu, kwake, na kwa wale wote ambao hufuata
nyayo za Mungu na kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu.
Ilielezewa
Machi 23, 2010
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu
Kwa nini unamwamini Mungu ? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa...
-
Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, Mungu ndiye Mwanzo, na tena Mwisho, na tena Mwisho, na tena Mw...
-
Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ...
-
Biblia pia huitwa Agano la Kale na Agano Jipya. Je, wajua “agano” linarejelea nini? “Agano” katika “Agano Jipya” linatokana na makubalia...



