Jumamosi, 19 Agosti 2017

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kusikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje, kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu na dada wanaomfuata Yesu wangependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewaza iwapo utamjua Yesu Atakaporejea? Je, mtaelewa kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya?

Ijumaa, 18 Agosti 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali.

Jumanne, 15 Agosti 2017

Umeme wa Mashariki|Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa thabiti katika kazi Yake, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na harakati ya mambo yote. Kama kila kiumbe, mwanadamu bila kujua anapata lishe ya utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote, mwanadamu bila kujua anaishi chini ya mpango wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yote ya mwanadamu yanatunzwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, vilivyo hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, vitafanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hivi ndivyo Mungu anavyotawala juu ya kila kitu.
Usiku uingiapo kwa utulivu, mwanadamu huwa hafahamu, kwani moyo wa mwanadamu hauwezi kujua jinsi giza linapokaribia au linakotoka. Usiku unapotoweka polepole, mwanadamu anakaribisha mwanga wa mchana, lakini moyo wa mwanadamu haufahamu ilikotoka nuru hii na jinsi gani nuru yenyewe imeliondoa giza la usiku. Mabadiliko kama haya ya kawaida ya mchana na usiku humpitisha mwanadamu katika kipindi kimoja baada ya kingine, kupita katika nyakati, wakati huu wote ikihakikisha kwamba kazi ya Mungu na mpango wake unafanywa wakati wa kila kipindi na katika nyakati zote. Mwanadamu alitembea katika enzi nyingi na Mungu, lakini bado mwanadamu hafahamu kwamba Mungu ndiye kiongozi wa hatima ya mambo yote na viumbe hai na pia hafahamu jinsi Mungu hupanga na kuongoza mambo yote. Hili ni jambo ambalo limekwepa ufahamu wa binadamu tangu enzi za kale mpaka leo. Na juu ya ni kwa sababu ipi, sio kwa sababu njia za Mungu hazifahamiki, au kwa sababu mpango wa Mungu bado haujakamilika, lakini ni kwa sababu moyo na roho ya mwanadamu viko mbali sana na Mungu. Kwa hivyo, hata ingawa mwanadamu Anamfuata Mungu, bila kujua yeye hubaki katika huduma ya Shetani. Hakuna anayetafuta kwa ukamilifu nyayo au nafsi ya Mungu, na hakuna anayetaka kuwepo katika huduma na utunzaji wa Mungu. Badala yake, wao wako tayari kutegemea upotoshaji wa Shetani na yule mwovu ili kubadilishwa na dunia hii na kanuni za maisha ambazo watu waovu hufuata. Katika nafasi hii, moyo na roho za mwanadamu hutolewa kafara kwa shetani na kuwa riziki yake. Aidha, moyo wa binadamu na roho yake huwa mahali ambapo Shetani anaweza kuishi na kuufanya uwanja wake wa kuchezea. Kwa njia hii, mwanadamu kwa kutojua hupoteza ufahamu wake wa kanuni ya kuwa binadamu, na wa thamani na madhumuni ya kuwepo kwa binadamu. Sheria kutoka kwa Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu huangamia hatua kwa hatua kutoka katika moyo wa mwanadamu mpaka mwishowe mwanadamu hawezi tena kuomba au kufuata na kumsikiza Mungu. Wakati upitapo, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba, wala haelewi maneno yanayotoka katika kinywa cha Mungu au kutambua kwamba yote hayo ni kutoka kwa Mungu. Mwanadamu huanza kupinga sheria na amri kutoka kwa Mungu; moyo na roho ya mwanadamu hufishwa. ... Mungu humpoteza mwanadamu Aliyemuumba pale mwanzo, na mwanadamu hupoteza mizizi ya mwanzo wake. Hii ni huzuni ya uanadamu. Kwa uhakika, tangu mwanzo mpaka sasa, Mungu alilifanya janga la wanadamu ambalo mwanadamu ni mhusika mkuu na mwaathiriwa, na hakuna hata mmoja anayeweza kupata jibu kuhusu nani ndiye mwelekezi wa hadithi hii ya janga.
Katika dunia hii kubwa, mabadiliko yasiyo hesabika yamefanyika, tena na tena. Hapana aliye na uwezo wa kuongoza binadamu isipokuwa Yeye ambaye Anatawala juu ya kila kitu katika ulimwengu. Hakuna yeyote hodari kwa kazi au kufanya maandalizi kwa ajili ya binadamu, wala aliye na uwezo wa kuwaongoza wanadamu kurejelea mwanga na ukombozi kutokana na ukosefu wa haki duniani. Mungu Analalamikia wakati ujao wa wanadamu, na Anahuzunishwa na kuanguka kwa mwanadamu. Anahisi huzuni kwa kuangamia kwa mwanadamu polepole na kwenda katika njia isiyo na upande wa kurudi. Mwanadamu ameuvunja moyo wa Mungu, akamkana na kumfuata yule mwovu. Hakuna aliyewahi kuwa na mawazo kuhusu mwelekeo ambao mwanadamu wa aina hii atafuata. Ni kwa sababu hii haswa ndio kwamba hakuna ambaye ameona hasira ya Mungu. Hakuna anayetafuta njia ya kumpendeza Mungu au kujaribu kuwa karibu na Mungu. Kadhalika, hakuna anayetafuta kufahamu huzuni na maumivu ya Mungu. Hata baada ya kusikia sauti ya Mungu, binadamu anaendelea tu kwenye njia yake mbali na Mungu, kukwepa neema na huduma ya Mungu, na kuepuka ukweli wa Mungu, akiona ni afadhali auuze mwili wake kwa Shetani, adui wa Mungu. Na ni nani amewahi kuwa na mawazo yoyote ya jinsi gani Mungu atamtendea mwanadamu asiyetubu na ambaye amempuuza? Hakuna anayejua kwamba ukumbusho wa mara kwa mara na nasaha za Mungu ni kwa sababu Yeye anayo katika mikono yake maafa Aliyowaandalia yasiyokuwa ya kawaida, maafa ambayo yatakuwa magumu kwa mwili na nafsi ya mwanadamu kustahimili. Janga hili sio tu adhabu ya mwili bali ya roho pia. Lazima ujue hili: Mpango wa Mungu unapokataliwa na wakati kuwakumbusha kwake na nasaha hazileti mabadiliko, Atakuwa na hasira ya aina gani? Hii itakuwa kama kitu ambacho hakijawahi kushuhudiwa hapo awali au hata kusikika na viumbe vyovyote. Na hivyo Nasema, janga hili ni kubwa mno na kamwe hayatawahi kurudiwa. Hii ni kwa sababu uumbaji mmoja tu na wokovu mmoja wa mwanadamu ndio ulio ndani ya mpango wa Mungu. Hii ni mara ya kwanza na pia ni ya mwisho. Kwa hivyo, hakuna anayeweza kuelewa nia ya huruma na hamu ya Mungu kwa matarajio yake ya kuwaokoa wanadamu.
Mungu aliumba dunia hii na kuleta mwanadamu, kiumbe hai ambacho alitia uhai ndani yake. Baadaye, mwanadamu akaja kuwa na wazazi na jamaa na hakuwa mpweke tena. Tangu mwanadamu alipotua macho kwa mara ya kwanza katika dunia hii tunayoishi, ilibainika kuwa angeishi ndani ya utaratibu wa Mungu. Ni pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ndiyo hustawisha kila kiumbe hai katika ukuaji wake hadi kinapokomaa. Wakati wa mchakato huu, hakuna hata mmoja anayeamini kwamba mwanadamu huishi na kukua chini ya uangalizi wa Mungu. Badala yake, anashikilia kwamba mwanadamu hukua chini ya upendo na utunzaji wa wazazi wake, na kwamba ukuaji wake unaongozwa na silika ya maisha. Hii ni kwa sababu mwanadamu hajui aliyeleta maisha au kulikotoka maisha hayo, pia hafahamu jinsi silika ya maisha husababisha miujiza. Mwanadamu anajua tu kwamba chakula ndicho msingi wa kuendelea kwa maisha, kwamba uvumilivu ni chanzo cha kuwepo kwa maisha, na kwamba imani iliyomo akilini mwake ni utajiri wa maisha yake. Mwanadamu haihisi neema na riziki itokayo kwa Mungu. Mwanadamu huyatumia kwa uharibifu maisha aliyopewa na Mungu. ... Hapana hata mwanadamu mmoja ambaye Mungu Anamwangazia usiku na mchana amechukua jukumu la kuanza Kumwabudu. Mungu Anaendelea kufanya kazi kama Alivyopanga juu ya mwanadamu Akiwa hana matarajio yoyote kutoka kwa mwanadamu. Anafanya hivyo kwa matumaini kwamba siku moja, mwanadamu ataamka kutoka katika ndoto yake na ghafla kuelewa thamani na madhumuni ya maisha, kuelewa gharama Aliyopitia Mungu ili Ampe mwanadamu kila kitu alicho nacho, na kujua jinsi Mungu anavyotamani kwa ari mwanadamu ageuke na Kumrudia. Hakuna yeyote amewahi kufikiria juu ya siri ya asili na endelezo la maisha ya mwanadamu. Na bila shaka, Mungu tu Ambaye Anaelewa yote haya na kwa kimya huvumilia mapigo na maumivu kutoka kwa binadamu, ambaye alipokea kila kitu kutoka kwa Mungu bila shukurani. Binadamu huchukulia kila kitu kinacholetwa na maisha kimzaha, na tena kama "kama jambo lisilo na shaka," Mungu amesalitiwa, amesahaulika, na kukataliwa na binadamu. Je, mpango wa Mungu ni wa maana namna hii? Je mwanadamu, kiumbe hai ambaye alitoka katika mkono wa Mungu, ni wa maana namna hiyo? Mpango wa Mungu ni wa umuhimu kabisa; hata hivyo, maisha ya viumbe vya mkono wa Mungu vipo kwa ajili ya mpango Wake. Kwa hivyo, Mungu hawezi kuuharibu mpango wake kwa sababu ya chuki Yake kwa mwanadamu. Ni kwa ajili ya mpango Wake na pumzi aliyotoa ndiyo maana Mungu Hustahimili mateso yote, siyo kwa ajili ya mwili wa mwanadamu ila ni kwa sababu ya uhai wa mwanadamu. Mungu ana hamu ya kuchukua pumzi aliyopuliza ndani mwa mwanadamu, wala sio nyama za mwili. Huu ndio mpango wake.
Wote wanaokuja duniani lazima wapitie maisha na kifo, na wengi wamepitia mzunguko wa kifo na kuzaliwa upya. Wale wanaoishi watakufa hivi karibuni na wafu watarejea karibuni. Yote haya ni mwendo wa maisha uliopangwa na Mungu kwa kila kiumbe hai. Hata hivyo, njia hii na mzunguko huu ni ukweli ambao Mungu Anataka binadamu aone, kwamba maisha aliyopewa na Mungu hayana kikomo na hayazuiliwi na mwili, wakati, au nafasi. Hii ni siri ya maisha aliyopewa binadamu na Mungu na dhihirisho kwamba maisha yalikuja kutoka Kwake. Ingawa watu wengi wanaweza kosa kuamini kwamba maisha yalitoka kwa Mungu, binadamu bila ya kufahamu wanafurahia yote yatokayo kwa Mungu, iwe wanaamini au wanakana uwepo Wake. Iwapo siku moja Mungu kwa ghafla Atabadili moyo na Atake kurudisha yote yaliyomo duniani na kuchukua maisha Aliyotoa, basi yote duniani yataisha. Mungu Hutumia maisha Yake kukimu vitu vyote vilivyo hai na visivyo na uhai, na kuleta yote kwa utaratibu mzuri kwa mujibu wa madaraka na mamlaka Yake. Huu ni ukweli ambao hakuna anayeweza kuufahamu au kuuelewa kwa urahisi, na kweli hizi zisizoeleweka kwa fikira zetu ni dhihirisho halisi na ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha. Sasa hebu nikupe siri: Ukuu na nguvu ya uhai wa Mungu hauwezi kueleweka na kiumbe chochote. Hii ilikuwa hivyo awali, iko hivyo wakati huu, na itakuwa hivyo wakati ujao. Siri ya pili Nitakayotoa ni hii: chanzo cha uhai hutoka kwa Mungu, kwa viumbe vyote, haijalishi tofauti katika maumbile au muundo. Hata uwe kiumbe hai cha aina gani, huwezi kwenda kinyume na njia ya maisha ambayo Mungu ameweka. Katika hali yoyote, kile Napenda ni kuwa mwanadamu aelewe kwamba bila huduma, utunzaji, na utoaji wa Mungu, mwanadamu hawezi kupokea yote aliyokusudiwa kupokea, haijalishi juhudi au mapambano yake. Bila ruzuku ya uhai kutoka kwa Mungu, mwanadamu hupoteza maana ya thamani katika maisha na kupoteza madhumuni ya kusudi katika maisha. Mungu angewezaje kuruhusu mwanadamu anayepoteza thamani ya uhai wake kuishi hivyo bila ya kujali? Kisha tena, usisahau kwamba Mungu Ndiye chanzo cha maisha yako. Iwapo mwanadamu atashindwa kuthamini yote ambayo Mungu Amemfanyia, Mungu Hatachukua kile Alichotoa pekee, lakini zaidi ya hayo, mwanadamu atalipa mara mbili kufanya fidia kwa yote ambayo Mungu Ametumia.
Mei 26, 2003
      Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu ndiye ujio wa pili wa Bwana Yesu. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi usome maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana! Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli kuja hapa na kutazama.

Jumatatu, 14 Agosti 2017

Umeme wa Mashariki|Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wetu wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya haki ya mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo kwa Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu.
Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa msanifu wa utamaduni na ustaarabu wa binadamu wa zamani wa mataifa mengine. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana. Ukuaji wa mwanadamu na maendeleo ya binadamu hayatengani na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu haziwezi kuondolewa kwa miundo ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na mwisho wa safari ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga.
Angalia nyuma wakati wa safina ya Nuhu: Mwanadamu alikuwa mpotovu sana, alikuwa amepotea kutoka katika baraka za Mungu, hakuwa anatunzwa na Mungu tena, na alipoteza ahadi za Mungu. Waliishi gizani, bila mwangaza wa Mungu. Hivyo wakawa kinyume na maadili kwa asili, wakajiachilia katika mkengeuko. Watu kama hao hawangeweza tena kupokea ahadi za Mungu; hawakufaa kushuhudia uso wa Mungu, wala kusikia sauti ya Mungu, kwani walikuwa wamemwacha Mungu, kuweka kando yote Aliyowapa, na kusahau mafunzo ya Mungu. Mioyo yao ilipotea mbali zaidi na zaidi na Mungu, na ilivyofanya hivyo, wakawa wapotovu zaidi ya mantiki na ubinadamu wote na wakazidi kuwa waovu. Hivyo walikaribia kifo, na kukabiliwa na ghadhabu na adhabu ya Mungu. Ni Nuhu tu aliyemwabudu Mungu na kuepukana na uovu, na hivyo aliweza kusikia sauti ya Mungu, na kusikia maelekezo ya Mungu. Alijenga safina kulingana na maelekezo ya neno la Mungu, na kukusanya aina yote ya viumbe hai. Na kwa njia hii, wakati kila kitu kilikuwa kimetayarishwa, Mungu aliangamiza dunia. Nuhu tu na wanachama saba wa familia yake walinusurika maangamizi, kwani Nuhu alimwabudu Yehova na kuepukana na uovu.
Kisha angalia enzi ya sasa: Hawa watu wenye haki kama Nuhu, wanaoweza kumwabudu Mungu na kuepuka uovu, wamekoma kuwepo. Lakini bado Mungu ana fadhili kwa mwanadamu huyu, na Anamsamehe mwanadamu wakati huu wa enzi ya mwisho. Mungu anawatafuta wanaomtaka Yeye ajitokeze. Anawatafuta wale wanaoweza kuyasikia maneno Yake, na wale ambao hawajasahau agizo Lake na kutoa mioyo na miili yao Kwake. Anawatafuta wale walio watiifu kama watoto wachanga mbele Yake, na hawampingi. Kama hujazuiliwa na nguvu zozote katika ibada yako Kwake, basi Mungu atakutazama na neema, na kukupea baraka Zake Kama wewe ni wa daraja la juu, wa sifa ya heshima, aliyemiliki maarifa mengi, mmiliki wa mali nyingi, na kuungwa mkono na watu wengi, lakini mambo haya hayakuzuii kuja mbele za Mungu kuukubali wito Wake na agizo Lake, kufanya kile Mungu anachokuambia ufanye, basi yote unayoyafanya yatakuwa na umuhimu zaidi duniani na yenye haki zaidi duniani. Ukiukataa wito wa Mungu kwa sababu ya hadhi yako na malengo yako mwenyewe, yote utakayoyafanya yatalaaniwa na pia kudharauliwa na Mungu. Labda wewe ni rais, ama mwanasayansi, ama mchungaji, ama mzee, lakini bila kujali ukuu wa ofisi yako, ukitegemea maarifa yako na uwezo wa shughuli zako, basi daima utakuwa wa kushindwa na kamwe utanyimwa baraka za Mungu, kwa sababu Mungu hakubali chochote unachofanya, na Hakubali kwamba kazi yako ni yenye haki, wala kukubali kwamba unafanya kazi kwa msaada wa mwanadamu. Atasema yote unayofanya, ni ya kutumia maarifa na nguvu za mwanadamu kumnyima mwanadamu ulinzi wa Mungu na kumnyima baraka za Mungu. Atasema kuwa unamwongoza mwanadamu kuelekea gizani, kuelekea kifo, na kuelekea mwanzo wa kuwepo bila mipaka ambapo mwanadamu amempoteza Mungu na baraka Zake.
Kutoka wakati mwanadamu kwanza alikuwa na sayansi ya jamii, akili yake ilikuwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa vikawa vyombo vya kutawala mwanadamu, na hapakutosha tena nafasi ya kumwabudu Mungu, na hapakuwa tena na mazingira mazuri ya kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu ilikuwa ndogo zaidi moyoni mwa mwanadamu. Dunia moyoni mwa mwanadamu bila nafasi ya Mungu ni giza, tupu bila matumaini. Na hivyo kukatokea wanasayansi wa jamii, wataalamu wa historia na wanasiasa wengi kueleza nadharia ya sayansi ya jamii, nadharia ya mageuko ya binadamu, na nadharia zingine zinazoenda kinyume na ukweli kwamba Mungu alimuumba mwanadamu, kujaza moyo na akili ya mwanadamu. Na kwa njia hii, wanaoamini kwamba Mungu aliumba kila kitu wakawa wachache zaidi, na wale wanaoamini nadharia ya mageuko wakawa hata wengi kwa nambari. Watu zaidi wanachukulia rekodi za kazi ya Mungu na maneno Yake wakati wa Agano la Kale kuwa hadithi na simulizi. Kwa mioyo yao, watu wanakuwa wasiojali heshima na ukubwa wa Mungu, kwa kanuni kwamba Mungu yupo na anatawala kila kitu. Kusalimika kwa mwanadamu na majaliwa ya nchi na mataifa si muhimu kwao tena. Mwanadamu anaishi katika dunia tupu akijishughulisha tu na kula, kunywa, na ufuatiliaji wa furaha….Watu wachache wanashughulika kutafuta Afanyapo Mungu kazi Yake leo, ama kutafuta jinsi Anavyoongoza na kupanga majaliwa ya mwanadamu. Na kwa njia hii, ustaarabu wa ubinadamu bila fahamu ukawa huwezi kukutana na matakwa ya mwanadamu, na kuna watu zaidi wanaohisi kwamba, kuishi kwa dunia kama hii, wanayo furaha ya chini kuliko watu walioenda. Hata watu wa nchi zilizokuwa na ustaarabu wa juu wanaeleza malalamiko haya. Kwani bila mwongozo wa Mungu, bila kujali idadi ya viongozi na wanasosholojia wanaotafakari kuhifadhi ustaarabu wa binadamu, haina mafanikio. Hakuna anayeweza kujaza utupu kwa moyo wa mwanadamu, kwani hakuna anayeweza kuwa uhai wa mwanadamu, na hakuna nadharia ya kijamii inayoweza kumwokoa kutokana na utupu unaomtesa. Sayansi, maarifa, uhuru, demokrasia, wasaa wa mapumziko, faraja, haya yote ni mapumziko ya muda, Hata na mambo haya, mwanadamu hataepuka kufanya dhambi na kuomboleza ukosefu wa haki wa jamii. Mambo haya hayawezi kupunguza tamaa ya mwanadamu na hamu ya kuchunguza. Kwa sababu mwanadamu aliumbwa na Mungu na kafara kipumbavu na uchunguzi wa mwanadamu vitamwongoza tu kwa dhiki zaidi, Mwanadamu atakuwa na hofu isiyoisha, hatajua jinsi ya kuukabili mustakabali wa wanadamu, ama jinsi ya kuikabili njia iliyo mbele. Mwanadamu atakuja hata kuogopa sayansi na elimu, na kuhofia utupu ulio ndani yake sana. Duniani humu, bila kujali kama unaishi katika nchi huru ama isiyo na haki za binadamu, huwezi kabisa kuponyoka majaliwa ya mwanadamu. Kama wewe ni kiongozi ama anayeongozwa, huwezi kabisa kuponyoka hamu ya kuchunguza majaliwa, siri na majaliwa ya mwanadamu. Chini ya hayo, huna uwezo wa kutoroka hisia ya utupu inayohangaisha. Matukio kama haya, yaliyo kawaida kwa wanadamu wote, yanaitwa matukio ya kijamii na wanasoshiolojia, lakini hakuna mtu mkubwa anayeweza kuja mbele kutatua shida kama hizi. Mwanadamu, hata hivyo, ni mwanadamu. Nafasi na maisha ya Mungu hayawezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Mwanadamu hahitaji tu jamii iliyo na haki, ambayo kila mtu analishwa vyema na ana uhuru na usawa, lakini wokovu wa Mungu na Yeye kuwapa uhai. Wakati tu mwanadamu atapokea wokovu wa Mungu na kupatiwa kwake uhai na Yeye ndipo mahitaji, hamu ya kuchunguza, na utupu wa kiroho wa mwanadamu unaweza kutatuliwa. Iwapo watu wa nchi ama taifa hawawezi kupokea wokovu na utunzaji wa Mungu, basi nchi ama taifa kama hilo litatembelea njia inayoelekea uharibifuni, inayoelekea gizani, na litaangamizwa na Mungu.
Labda nchi yako inafanikiwa sasa, lakini ukiruhusu watu wako kumpoteza Mungu, basi nchi yako itazidi kujipata bila baraka za Mungu. Ustaarabu wa nchi yako utazidi kukanyagiwa chini, na kabla ya muda mrefu watu watamshambulia Mungu na kulaani Mbingu. Na hivyo majaliwa ya nchi italetwa kwa uharibifu. Mungu ataziinua nchi zenye nguvu ili kukabiliana na nchi hizo zilizolaaniwa na Mungu, na anaweza kuzifuta kutoka uso wa dunia. Kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa kunategemea kama viongozi wao wanamwabudu Mungu, na kama wanawaongoza watu wao karibu na Mungu na kumwabudu. Lakini, kwa hii enzi ya mwisho, kwa sababu wale wanaomtafuta Mungu kwa kweli na kumwabudu wanazidi kuwa wachache, Mungu ataweka fadhili ya pekee juu ya nchi ambayo Ukristo ni dini ya serikali. Anawakusanya pamoja kuunda kambi ya haki kiasi ya dunia, wakati nchi zikanazo Mungu ama zile zisizomwabudu Mungu wa kweli zinakuwa wapinzani wa kambi ya haki. Kwa njia hii, Mungu hana tu mahali miongoni mwa wanadamu pa kufanyia kazi Yake, lakini pia Anapata nchi zinazoweza kutumia mamlaka ya haki, ili kulazimisha adhabu na vikwazo kwa nchi hizo zinazompinga Mungu. Lakini licha ya hayo, bado hakuna watu zaidi wanaokuja mbele kumwabudu Mungu, kwa sababu mwanadamu amepotea mbali sana kutoka Kwake, na Mungu hajakuwa kwa mawazo ya mwanadamu kwa muda mrefu. Kunabakia tu duniani nchi zinazotumia haki na kupinga udhalimu. Lakini hii ni mbali na matakwa ya Mungu, kwani hakuna kiongozi wa nchi yoyote atamruhusu Mungu kuongoza watu wake, na hakuna chama cha kisiasa kitakachokusanya pamoja watu wake kumwabudu Mungu; Mungu amepoteza mahala Pake halali kwa mioyo ya nchi zote, taifa, chama tawala, na hata kwa moyo wa kila mtu. Ingawa nguvu za haki ziko kwa dunia hii, utawala ambao Mungu hana mahali kwa moyo wa mwanadamu ni dhaifu. Bila baraka ya Mungu, uwanja wa kisiasa utaanguka katika vurugu na kuathirika na mashambulizi. Kwa mwanadamu, kuwa bila baraka ya Mungu ni kama kukosa mwanga wa jua. Bila kujali jinsi viongozi wanafanya mchango kwa watu wao kwa uangalifu, bila kujali idadi ya mikutano ya haki mwanadamu anashikilia, hakuna kati ya hii itakayorejesha maneno ama kubadilisha majaliwa ya mwanadamu. Mwanadamu anaamini kuwa nchi ambayo watu wanalishwa na kuvalishwa nguo, ambayo watu wanaishi kwa amani, ni nchi nzuri, na iliyo na uongozi mzuri. Lakini Mungu hafikirii hivyo. Anaamini kuwa nchi ambayo hakuna mtu anayemwabudu ndiyo Atakayoiangamiza. Njia ya mwanadamu ya kufikiria haiambatani na ya Mungu. Kama mkuu wa nchi hamwabudu Mungu, basi majaliwa ya nchi hii itakuwa ya kutisha, na nchi haitakuwa na majaliwa.
Mungu hashughuliki na siasa za mwanadamu, lakini majaliwa ya nchi ama taifa inadhibitiwa na Mungu, Mungu anadhibiti dunia hii na ulimwengu mzima. Majaliwa ya mwanadamu na mpango wa Mungu yanashikamana kwa undani, na hakuna mwanadamu, nchi ama taifa imetolewa kwa mamlaka ya Mungu. Iwapo mwanadamu anatamani kujua majaliwa yake, basi lazima aje mbele ya Mungu. Mungu atawafanya wanaomfuata na kumwabudu kufanikiwa, na Atashusha na kuwaangamiza wale wanaompinga na kumkataa.
Kumbuka tukio katika Biblia ambapo Mungu aliangamiza Sodoma, na fikiria pia jinsi mke wa Loti alivyokuwa nguzo ya chumvi. Fikiria nyuma jinsi watu wa Ninawi walitubu dhambi zao kwa gunia na majivu, na kumbuka kilichofuata baada ya Wayahudi kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita. Wayahudi walitolewa Israeli na kukimbilia nchi duniani kote. Wengi waliuwawa, na taifa lote la Wayahudi lilikabiliwa na uharibifu. Walimsulubisha Mungu—wakafanya uhalifu wa kutisha—na kuchochea tabia ya Mungu. Walifanywa kulipa walichofanya, walifanywa kubeba matokeo ya vitendo vyao. Walimlaani Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na majaliwa moja: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo matokeo machungu na maafa ambayo viongozi wao waliletea nchi na taifa lao.
Leo, Mungu amerudi duniani kufanya kazi Yake. Atasimama kwanza kwa mkutano mkubwa wa viongozi madikteta: Uchina, ngome kali ya ukanaji Mungu. Mungu amepata kundi la watu kwa hekima na nguvu Zake. Wakati huu, Anawindwa na chama tawala cha Uchina kwa kila namna na kukabiliwa na mateso makubwa, bila mahala pa kupumzisha kichwa Chake na kutoweza kupata makazi. Licha ya haya, Mungu anaendelea kufanya kazi Aliyonuia kufanya: Anatamka sauti Yake na kueneza injili. Hakuna anayeweza kuelewa uweza wa Mungu. Uchina, nchi inayomchukulia Mungu kama adui, Mungu hajawahi kukoma kazi Yake. Badala yake, watu wengi wamekubali kazi na neno Lake, kwani Mungu anafanya yote Awezayo kuokoa kila mshiriki wa ubinadamu. Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kusimama kwa njia ya anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga kazi ya Mungu, kuvuruga na kutatiza mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayekataa kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayokataa kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka usoni pa dunia, na litakoma kuwepo. Nahimiza watu wa mataifa, nchi na hata viwanda vyote kusikiza sauti ya Mungu, kutazama kazi ya Mungu, kuzingatia kwa makini majaliwa ya mwanadamu, hivyo kumfanya Mungu kuwa mtakatifu zaidi, wa heshima zaidi, wa juu zaidi na chombo cha pekee cha kuabudu miongoni mwa wanadamu, na kuruhusu wanadamu wote kuishi chini ya baraka za Mungu, kama ukoo wa Ibrahimu ulivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama Adamu na Hawa, walioumbwa awali na Mungu, walivyoishi kwa Bustani ya Edeni.
Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayofurika kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na kumtafuta na kuwa na kiu Naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na wanastahili adhabu.

Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu ndiye ujio wa pili wa Bwana Yesu. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi usome maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana! Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli kuja hapa na kutazama.

Jumapili, 13 Agosti 2017

Umeme wa Mashariki|Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa. Mungu kamwe hajawahi kosa kwa moyo wa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa binadamu wakati wote. Amekuwa nguvu ya kuendesha maisha ya mwanadamu, chanzo cha kuwepo kwa binadamu, na amana ya fahari ya kuwepo kwa binadamu baada ya kuzaliwa. Husababisha binadamu kuzaliwa upya, na kumwezesha kwa ushupavu kuishi kwa kila jukumu lake. Kwa sababu ya uwezo Wake, na nguvu ya maisha Yake yasiyopungua, binadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, ambapo nguvu ya uhai wa Mungu umekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa binadamu, na ambayo Mungu amelipa gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha si rahisi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung'aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Maisha ya Mungu, huishi milele bila kubadilika katika kusumbuka kwa mbingu na nchi. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao. Asili ya maisha ya mwanadamu hutoka kwa Mungu, kuwepo kwa mbingu ni kwa sababu ya Mungu, na kuwepo kwa ardhi kunatokana na nguvu ya uhai wa Mungu. Hakuna kitu kinachomiliki nguvu kinachoweza kuzidi ukuu wa Mungu, na hakuna kitu chenye nguvu kinachoweza kuvunja mipaka ya mamlaka ya Mungu. Kwa njia hii, bila kujali wao ni nani, kila mtu lazima ajiwasilishe kwa utawala wa Mungu, kila mtu lazima aishi chini ya amri za Mungu, na hakuna mtu anayeweza kutoroka kutoka katika utawala Wake.
Pengine, sasa, unataka kupokea maisha, au labda unataka kupata ukweli. Vyovyote vilivyo, unataka kumpata Mungu, kumpata Mungu unayeweza kutegemea, na ambaye anaweza kukupa uzima wa milele. Ukitaka kupata uzima wa milele, lazima kwanza uelewe chanzo cha uzima wa milele, na lazima kwanza ujue Mungu yuko wapi. Tayari nilishasema Mungu pekee ndiye maisha yasiyobadilika, na Mungu tu ndiye aliye na njia ya maisha. Kwa kuwa maisha Yake ni imara, hivyo ni ya milele; kwa kuwa Mungu tu ndiye njia ya maisha, basi Mungu Mwenyewe ni njia ya uzima wa milele. Kwa hivyo, lazima kwanza uelewe aliko Mungu, na jinsi ya kupata njia hii ya uzima wa milele. Hebu sasa tushiriki kwa masuala haya mawili tofauti.
Kama kweli unataka kupata njia ya uzima wa milele, na kama wewe unayo tamaa katika utafutaji wako kwa ajili yake, basi kwanza ulijibu swali hili: Mungu yuko wapi leo? Labda utajibu kwamba Mungu anaishi mbinguni, bila shaka—Hangeishi katika nyumba yako? Labda unaweza kusema, kawaida Mungu anaishi kati ya mambo yote. Au unaweza kusema kwamba Mungu anaishi katika moyo wa kila mtu, au kwamba Mungu yuko katika ulimwengu wa kiroho. Mimi sipingi lolote kati ya haya, lakini lazima nifafanue suala hilo. Sio sahihi kabisa kusema kwamba Mungu anaishi katika moyo wa mwanadamu, wala si makosa kabisa. Hiyo ni kwa sababu, miongoni mwa waumini katika Mungu, kuna wale ambao imani yao ni ya kweli na wale ambao imani yao ni uongo, kuna wale ambao Mungu anawakubali na wale ambao hawakubali, kuna wale ambao humfurahisha na wale ambao ni chukizo, na kuna wale ambao Yeye huwafanya kamili na wale ambao hupunguza. Na hivyo mimi Nasema kwamba Mungu Anaishi tu katika nyoyo za watu wachache, na watu hawa bila shaka ni wale ambao kweli wanaamini katika Mungu, wale ambao Mungu anawakubali, wale ambao humpendeza, na wale ambao Yeye huwafanya kamili. Wao ni wale wanaoongozwa na Mungu. Kwa kuwa wanaongozwa na Mungu, kwa hivyo ni watu ambao tayari wamesikia na kuona njia ya Mungu ya uzima wa milele. Wale ambao imani yao kwa Mungu ni ya uongo, wale ambao hawajaidhinishwa na Mungu, wale ambao wanadharauliwa na Mungu, wale ambao wamechujwa na Mungu—wamefungwa katika kukataliwa na Mungu, wamefungwa kubaki bila njia ya maisha, na wamefungwa kubaki wajinga wa kujua aliko Mungu. Kwa upande mwingine, wale ambao Mungu anaishi katika nyoyo zao wanajua aliko Mungu. Wao ni watu wale ambao Mungu huwapa njia ya uzima wa milele, na ni wale wanaomfuata Mungu. Je, unajua, sasa, aliko Mungu? Mungu yupo katika moyo wa mtu na upande wa mtu. Hayupo tu katika ulimwengu wa kiroho, na juu ya mambo yote, lakini hata zaidi Yupo duniani ambapo mwanadamu huishi. Na hivyo kufika kwa siku za mwisho kumechukua hatua ya kazi ya Mungu katika sehemu mpya. Mungu ana ukuu juu ya mambo yote katika ulimwengu, na Yeye ni uti wa mgongo wa mwanadamu katika moyo wake, na zaidi ya hayo, Yeye yuko miongoni mwa wanadamu. Ni kwa njia hii pekee Anaweza kuleta njia ya maisha kwa binadamu, na kumleta mwanadamu katika njia ya maisha. Mungu amekuja duniani, na Anaishi kati ya wanadamu, ili wanadamu wanaweza kupata njia ya maisha, na hivyo binadamu anaweza kuwepo. Wakati huo huo, Mungu pia huamuru mambo yote katika ulimwengu, ili wapate kushirikiana na usimamizi Wake miongoni mwa wanadamu. Na hivyo, kama wewe unakiri tu kwamba Mungu yuko mbinguni na katika moyo wa mwanadamu, lakini usikiri ukweli wa kuwepo kwa Mungu miongoni mwa watu, basi kamwe hutapata uzima, na kamwe hutapata njia ya kweli.
Mungu Mwenyewe ni maisha, na kweli, na uzima Wake na ukweli hutawala. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli kamwe hawatapata uzima. Bila mwongozo, msaada, na utoaji wa kweli, nanyi tu mtapata barua, mafundisho, na zaidi sana, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachodhihirishwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na hali Yake halisi ya kazi. Kama wewe utatumia rekodi ya maneno yaliyosemwa na Mungu wakati wa enzi zilizopita leo, basi wewe ni mtafutaji wa mambo ya kale, na njia bora ya kukueleza wewe ni mtaalamu wa urithi wa kihistoria. Kwa sababu wewe daima unaamini katika athari ya kazi ambayo Mungu alifanya katika nyakati zilizopita, amini tu katika kivuli cha Mungu alichowacha awali Alipokuwa Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, na kuamini tu kwa njia ambayo Mungu aliwapa wafuasi wake katika nyakati za zamani. Huamini katika mwelekeo wa kazi ya Mungu leo, huamini katika uso wa utukufu wa Mungu leo, na huamini katika njia ya sasa ya kweli iliyotolewa na Mungu. Na hivyo wewe ni mwotaji wa mchana ambaye hana ufahamu kamwe na hali ya mambo ya sasa. Kama sasa bado wewe unafuata maneno yasiyokuwa na uwezo wa kuleta maisha kwa binadamu, basi wewe ni kipande cha ukuni uliokauka kisicho na matumaini[a], kwa maana wewe ni mwenye kushikilia ukale mno, asiyeweza kutiishwa kwa urahisi, huwezi kusikiza wosia!
Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, Kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, badala yake, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale Kristo bandia wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe. Kwa njia hii, kama kweli unataka kutafuta njia ya maisha, lazima kwanza ukiri kuwa ni kwa kuja duniani ndipo Anazirejesha njia za maisha kwa binadamu, na lazima kukiri ni katika siku za mwisho Yeye anakuja duniani kuhifadhia njia ya maisha kwa mwanadamu. Haya sio ya wakati wa nyuma; yanatendeka leo.
Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atajua Mungu na kuidhinishwa na Mungu. Kama hutatafuta njia ya maisha inayotolewa na Kristo wa siku za mwisho, basi kamwe hutapata kibali cha Yesu, na kamwe hutahitimu kuingia lango la ufalme wa mbinguni, kwa ajili nyote ni makaragosi na wafungwa wa historia. Wale ambao wanadhibitiwa na kanuni, na barua, na waliofungwa na historia kamwe hawataweza kupata maisha, na kamwe hawataweza kupata njia ya daima ya maisha. Hayo ni kwa sababu walio nayo ni maji machafu yaliyolala palepale kwa maelfu ya miaka, badala ya maji ya uzima yanayotiririka kutoka kiti cha enzi. Wale ambao hawajasambaziwa na maji ya uzima daima watabakia maiti, vitu vya mchezo wa Shetani, na wana wa Jehanamu. Je, basi jinsi gani wanaweza kumtazama Mungu? Kama wewe kamwe hujaribu kushikilia kwenye siku zilizopita, jaribu tu kuweka mambo kama yalivyo kwa kusimama kwa utulivu, na wala hujaribu kubadili hali kama ilivyo na kuacha historia, basi wewe hutakuwa daima dhidi ya Mungu? Hatua za kazi ya Mungu ni kubwa na zenye nguvu, kama kufurika kwa mawimbi na mngurumo wa radi—ilhali wewe unakaa na kwa uvivu ukisubiri uharibifu, na kujikita katika upumbavu wako na kutofanya chochote. Kwa njia hii, jinsi gani unaweza kuchukuliwa kama mtu anayefuata nyayo za kondoo? Jinsi gani unaweza kuhalalisha Mungu unayeshikilia kama Mungu ambaye ni daima mpya na si kamwe wa zamani? Na jinsi gani maneno ya vitabu vyako vya manjano yanaweza kukubeba hadi enzi mpya? Yanawezaje kukuongoza katika kutafuta hatua za kazi ya Mungu? Na jinsi gani yanaweza kukuchukua wewe kwenda mbinguni? Unayoshikilia mikononi ni barua ambayo isiyoweza kukuondolea kitu ila furaha ya muda mfupi, sio ukweli unaoweza kukupa maisha. Maandiko unayosoma ni yale tu ambayo yanaweza kuimarisha ulimi wako, sio maneno ya hekima ambayo yanaweza kukusaidia kujua maisha ya binadamu, wala njia inayoweza kukuongoza kwa ukamilifu. Je, si tofauti hii hukupa sababu kwa ajili ya kutafakari? Je, si inakuruhusu kuelewa siri zilizomo ndani? Je, una uwezo wa kujiwasilisha mwenyewe mbinguni kukutana na Mungu? Bila kuja kwa Mungu, je, unaweza kujichukua mwenyewe kwenda mbinguni kufurahia pamoja na familia ya Mungu? Je, wewe bado unaota sasa? Basi, Napendekeza sasa uwache kuota, na kuangalia Anayefanya kazi sasa, na Anayefanya kazi ya kuwaokoa binadamu siku za mwisho. Kama huwezi, wewe kamwe hutapata ukweli, na kamwe hutapata uzima.
Wale ambao wanataka kupata uzima bila kutegemea ukweli wa neno la Kristo ni watu wafidhuli mno duniani, na wale ambao hawawezi kukubali njia ya maisha inayoletwa na Kristo wamepotea ndotoni. Na hivyo nasema kwamba watu ambao hawakubali Kristo wa siku za mwisho watadharauliwa milele na Mungu. Kristo ni lango la binadamu kwa ufalme katika siku za mwisho, ambayo hakuna anayeweza kupita bila Yeye. Hakuna anayeweza kukamilishwa na Mungu ila kwa njia ya Kristo. Unaamini katika Mungu, na basi ni lazima ukubali neno Lake na kutii njia Yake. Lazima usifikiri juu ya kupata baraka tu bila kupokea ukweli, au kukubali utoaji wa maisha. Kristo Anakuja katika siku za mwisho ili wale wote ambao kweli wanaamini katika Yeye waweze kupata maisha. Kazi Yake ni kwa ajili ya kuhitimisha enzi ya zamani na kuingia enzi mpya, na ni njia ambayo lazima ichukuliwe na wale wote ambao wataingia enzi mpya. Kama huna uwezo wa kumtambua Yeye, na badala yake kumhukumu, kulikufuru jina Lake au hata kumtesa Yeye, basi wewe umefungwa kuchomwa milele, na kamwe hutaingia katika ufalme wa Mungu. Kwa maana Kristo Mwenyewe ni dhihirisho la Roho Mtakatifu, udhihirisho wa Mungu, Yule ambaye Mungu amemkabidhi kufanya kazi Yake hapa duniani. Na hivyo nasema kwamba kama huwezi kukubali yote yanayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, basi unakufuru Roho Mtakatifu. Adhabu ambayo lazima ishuhudiwe na wale ambao wanakufuru Roho Mtakatifu ni hasa dhahiri kwa wote. Nawaambia tena kwamba kama mtampinga Kristo wa siku za mwisho, na kumkanusha, basi hakuna mtu ambaye anaweza kubeba matokeo ya hilo kwa niaba yako. Aidha, tangu siku hii na kuendelea huwezi kuwa na nafasi nyingine ya kupata kibali cha Mungu; hata kama utajaribu kujikomboa mwenyewe, kamwe tena hutautazama uso wa Mungu. Kwa kuwa unachopinga si binadamu, unachokataa si jambo dogo, bali ni Kristo. Je, unafahamu ghadhabu ya matokeo haya? Wewe hujafanya makosa madogo, bali umetenda uhalifu wa kutisha. Na hivyo Nashauri kila mtu kutoweka wazi meno yenu mbele ya ukweli, au kufanya shutuma bila ya kujali, kwa kuwa ni ukweli tu unaoweza kukuletea maisha, na hakuna kitu isipokuwa ukweli kinachoweza kukuruhusu kuzaliwa upya na kutazama uso wa Mungu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuja kuwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu—Bwana Yesu aliyerudi—Kristo wa siku za mwisho, na pia chini ya hukumu Yake ya haki na kuadibu. Kanisa limejumuisha wale wote ambao wanaikubali kwa kweli kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na wameshindwa na kuokolewa na neno la Mungu. Liliasisiwa kabisa na Mwenyezi Mungu mwenyewe, na linaongozwa na kuchungwa binafsi na Yeye, na kamwe halikuanzishwa na mtu yeyote. Huu ni ukweli unaokubaliwa na watu wote waliochaguliwa katika Kanisa la Mwenyezi Mungu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Kwa nini unamwamini Mungu ? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa...