
Kama
mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu
Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya
Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu
kwa jina la Bwana Yesu Kristo - na haya yote sisi hufanya chini ya
utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara
nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote
yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri shahiri
kwamba sisi pia tunajiamini kutembelea njia ya kutii mapenzi ya Baba
aliye mbinguni. Tunatamani kurudi kwake Bwana Yesu, ujaji tukufu wa
Bwana Yesu, kwa mwisho wa maisha yetu hapa duniani, kwa kuonekana kwa
ufalme, na kwa kila kitu kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha
Ufunuo: Bwana anafika, na analeta maafa, na kuwazawadia walio wema na
kuwaadhibu walio waovu, na anawachukua wale wote wanaomfuata na
kukaribisha kurudi Kwake angani kumlaki. Kila wakati tunawaza kuhusu
haya, hatuna budi ila kujawa na hisia. Tunashukuru kwa kuwa
tulizaliwa nyakati za mwisho na tuna bahati ya kutosha ya kushuhudia
kuja kwake Bwana. Ingawa tumepitia mateso, yote ni kwa ajili ya
malipo ya “utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi sana”; hii ni
baraka iliyoje! Hamu hii yote na neema inayopewa na Bwana mara kwa
mara hutufanya kuingia kwenye maombi, na hutuleta pamoja kila mara.
Labda mwaka ujao, labda kesho, au labda hata mapema wakati mwanadamu
hatarajii, Bwana atarejea ghafla, na atatokea kati ya kundi la watu
ambao wamekuwa wakimsubiri kwa umakinifu. Sote tunashindana kati
yetu, hakuna anayetaka kubaki nyuma, ili kuwa kundi la kwanza la
kutazama kuonekana kwa Bwana, na kuwa mmoja ya wale watakaochukuliwa
kwenda mbinguni. Tumetoa kila kitu, bila kujali gharama, kwa ajili ya
kuwadia kwa siku hii. Baadhi yetu wameacha kazi zao, wengine
wameachana na familia zao, wengine kukana ndoa zao, na baadhi yao
hata wamepeana akiba zao zote. Ni upendo usio na ubinafsi wa aina
gani huu! Uaminifu na utiifu kama huu lazima uwe unashinda ule wa
watakatifu wa nyakati za zamani! Kwa kuwa Bwana anavyompa neema
yeyote yule ambaye Yeye anataka, na kumrehemu yeyote ambaye Yeye
anataka, kujitolea kwetu na matumizi yetu, na matumizi yetu,
tunaamini, tayari yametazamika machoni pake. Kwa hivyo, pia, sala
zetu za dhati zimefikia masikio Yake, na tunaamini kuwa Bwana
atatuzawadia kwa ajili ya kujitolea kwetu. Aidha, Mungu aliturehemu
kabla hajauumba ulimwengu, na hakuna atakayenyakua baraka na ahadi
Zake kutoka kwetu. Sote tunapanga kuhusu siku za usoni, na kupuuza
kwamba kujitolea kwetu na kugharamia ni mambo tunayoweza kutumia ili
kuchukuliwa kwenda mbinguni kukutana na Bwana. Pia, bila kusita hata
kidogo, sisi tunajiweka kwenye kiti cha enzi cha siku za baadaye,
tukitawala mataifa na watu wote kwa jumla, ama tunatawala kama
wafalme. Yote haya, sisi huchukulia kama jambo la lazima, kama kitu
kinachotarajiwa.
Tunadharau
wale wote walio kinyume na Bwana Yesu; na mwishowe, wote
wataangamizwa. Nani aliwaambia wasiamini kwamba Bwana Yesu ni
Mwokozi? Bila shaka, kuna wakati tunajifunza kutoka kwa Bwana Yesu na
tunakuwa na huruma kwa dunia, kwa kuwa hawaelewi, na tunapaswa kuwa
wavumilivu na kuwasamehe. Kila kitu tufanyacho ni kwa mujibu wa
mafundisho ya Biblia, kwani kila kitu ambacho hakifuatani na Biblia
ni uzushi, na madhehebu maovu. Imani kama hiyo imehifadhiwa ndani ya
akili zetu. Mola wetu yumo katika Biblia, na tusipoondoka kwenye
Biblia basi hatutaondoka kwa Bwana; tukitii kanuni yake, basi
tutaokolewa. Sisi husaidiana na kuchochea kila mmoja wetu, na kila
wakati tunapokusanyika pamoja ni matumaini yetu kwamba kila kitu
tunachosema na kutenda kinaambatana na matakwa ya Bwana na kuwa
kinaweza kukubaliwa na Bwana. Licha ya uhasama mkubwa ulioko kwenye
mazingira yetu, mioyo yetu imejaa furaha. Tunapowaza kuhusu baraka
hizi tunazoweza kupata kwa urahisi, je, kuna kitu ambacho hatuwezi
kukiacha? Je, kuna kitu ambacho hatuwezi kutengana nacho? Yote haya
ni thabiti, na haya yote yanatazamwa na macho ya Mungu. Sisi, walio
wachache na maskini ambao tumeinuliwa kutoka jaani, ni sawa na
wafuasi wa Bwana Yesu wa kawaida: Tunaota kuhusu kuchukuliwa kwenda
mbinguni, na kubarikiwa, na kutawala mataifa yote. Upotovu wetu
umeanikwa peupe machoni pa Mungu, na tamaa zetu na uchoyo
zinahukumiwa machoni pa Mungu. Bado, yote haya hutokea bila ajabu,
yenye mantiki, na hakuna hata mmoja kati yetu ambaye hushangaa kama
hamu yetu ni ya haki, wala hamna kati yetu ambaye anashuku usahihi wa
yote yale ambayo sisi tunashikilia. Nani anayeweza kujua mapenzi ya
Mungu? Hatujui jinsi ya kutafuta, au kuchunguza, au hata
kujishughulisha na njia ambayo mwanadamu hupitia. Kwa maana sisi
hujali tu kuhusu kama tutaweza kuchukuliwa kwenda mbinguni, kama
tunaweza kubarikiwa, kama kuna pahali tumetengewa kwa ufalme wa
mbinguni, na kama sisi tutaweza kupata mgawo wa maji ya uzima wa mto
wa maisha na matunda ya mti wa uzima. Je, sisi hatumwamini Bwana, na
je, sisi sio wafuasi wake Bwana, kwa ajili ya kupata vitu hivi?
Dhambi zetu zimesamehewa, tumetubu dhambi zetu, tumekunywa kikombe
cha mvinyo ambao ni mchungu, na tumeweka msalaba migongoni mwetu.
Nani anayeweza kusema kuwa gharama ambayo tumelipia haitakubalika na
Bwana? Nani anayeweza kusema kuwa hatujatayarisha mafuta yanayotosha?
Hatutaki kuwa kama wale bikira wapumbavu, ama kama wale ambao
wameachwa. Aidha, tunaomba kila wakati, na kumwomba Bwana atuepushe
kutokana na kudanganywa na Kristo wa uongo, kwa maana imeandikwa
kwenye Biblia kuwa “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazama,
Kristo yupo hapa, au yuko pale; msiamini hili. Kwa maana watatokea
makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na
maajabu; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi.
(Matayo 24: 23-24). Sisi sote tumeweka mistari hii ya biblia kwenye
kumbukumbu, tunazijua aya hizi toka mbele mpaka nyuma, na tunaziona
kama hazina ya thamani, kama maisha, na kama vitambulisho vyetu vya
wokovu wetu na kuchukuliwa kwenda mbinguni kwetu….
Kwa
maelfu za miaka, wanaoishi wamefariki, wakichukua tamaa zao na ndoto
zao, na hakuna anayejua kwa ukweli iwapo wameenda kwa ufalme wa
mbinguni. Wafu wanarudi, na wamesahau hadithi zote zilizotokea wakati
mmoja, na bado wanafuata mafundisho na njia za babu zetu. Kwa hivyo,
miaka inavyopita na siku zinavyosonga, hakuna anayejua iwapo Bwana
Yesu, Mungu wetu, kwa kweli hukubali yote tunayoyafanya. Kwa urahisi,
tunangojea matokeo na kubashiri kuhusu yale yote ambayo yatatokea.
Bado Mungu yu kimya siku zote, na hajawahi kutuonekania, wala kusema
nasi. Na kwa hivyo, kwa hiari yetu tunahukumu mapenzi ya Mungu na
tabia kwa mujibu wa Biblia na ishara. Sisi tumezoea kimya cha Mungu;
tumekuwa na mazoea ya kupima haki na makosa ya tabia zetu kutumia
njia zetu za mawazo: tumekuwa na mazoea ya kutumia elimu yetu, dhana,
na maadili yetu na kuyafanya yachukue nafasi ya matakwa ya Mungu
kwetu sisi; tumekuwa na mazoea ya kufurahia neema ya Mungu; tumekuwa
na mazoea ya Mungu kutoa msaada wakati sisi tunahitaji msaada huo;
tumekuwa na mazoea ya kunyosha mikono yetu kwa Mungu ili tupate mambo
yote, na kumuagiza Mungu; na pia tumekuwa na mazoea ya kufuata
mafundisho ya dini, bila kutilia maanani jinsi Roho Mtakatifu
hutuongoza; zaidi ya hayo, tumekuwa na mazoea ya siku ambazo sisi ni
bwana zetu wenyewe. Tunamwamini Mungu wa namna hii, ambaye hatujawahi
kukutana naye. Maswali kama namna tabia Yake ilivyo, utu wake na mali
yake, mfano wake, kama tutamjua ama hatutamjua wakati atakaporudi, na
kadhalika—haya yote hayana umuhimu. Jambo muhimu ni kuwa Yeye yumo
mioyoni mwetu, na kuwa tunamsubiri, na kuwa tunaweza kufikiria jinsi
Alivyo. Tunathamini imani yetu, na kuthamini hali yetu ya kiroho.
Tunaona kila kitu ni kama samadi, na kukanyaga mambo yote kwa nyayo
zetu. Kwa sababu sisi ni wafuasi wa Bwana mwenye utukufu, bila kujali
jinsi safari yetu ilivyo ndefu na ngumu, bila kujali shida na hatari
inayotukumba, hakuna kitu kitakachosimamisha nyayo tunapomfuata
Bwana. “Mto wa maji safi ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri,
ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo. Na katika
kila upande wa ule mto, ulikuwapo ule mti wa uzima, unaozaa matunda
aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi: Na majani ya
mti huo ni ya kuwaponya mataifa. Wala hapatakuwa na laana tena:
Lakini kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo kitakuwa ndani
yake; na watumwa wake watamtumikia: Nao watauona uso wake; na jina
lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. Na hapatakuwa na usiku
pale; wala hawahitaji mshumaa, wala nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu
huwapa nuru: nao watatawala milele hata na milele (Ufunuo wa Yohana
22:1-5). Kila wakati sisi hukariri maneno hayo, mioyo yetu hujawa na
furaha isiyo na kifani na maridhio pia, na machozi hutiririka kutoka
machoni mwetu. Shukrani ni kwa Bwana kwa kutuchagua, shukrani ni kwa
Bwana kwa neema Yake. Mara mia sasa, yeye ametupa uzima wa milele kwa
ulimwengu ujao, na kama angetuuliza tufe sasa, tungetii amri hiyo
bila kusita hata kidogo. Bwana! Tafadhali njoo hivi karibuni!
Usikawie hata dakika moja tena, kwa kuwa sisi tunakutamani na
tumeacha kila kitu kwa ajili yako.
Mungu
amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake
haijawahi kusimamishwa. Yeye huangalia nchi zote, na huamuru vitu
vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Usimamizi
wake hufanywa hatua kwa hatua na kulingana na mpango wake. Usimamizi
wake huendelea kimya kimya, bila madhara ilhali nyayo zake, daima
hukaribia binadamu, na kiti chake cha hukumu kimeenezwa katika
ulimwengu kwa kasi ya umeme, mara moja kikifuatwa na mshuko wa kiti
chake cha enzi kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, yaani,
tukio hilo ni uwakilishaji wa mandhari kwa makini na wa kuonyesha
Mungu ni mkuu. Kama njiwa na kama simba anayenguruma, Roho anawasili
kati yetu sisi sote. Yeye ni mwenye hekima, Yeye ni mwenye haki na wa
adhimu, Yeye huwasili kati yetu kwa ukimya, na huwasili na mamlaka
akiwa amejazwa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuja
Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo,
hakuna mwanadamu ambaye anajua chote atakachokifanya Yeye. Maisha ya
mwanadamu inabaki ilivyo bila kubadilika; moyo wake hauna tofauti, na
siku zinapita kama kawaida. Mungu anaishi kati yetu kama mtu wa
kawaida, kama mfuasi asiye na maana na pia kama muumini wa kawaida.
Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na vile vile, ana
uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona
kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya
kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila
mipaka au kuogopa, kwa kuwa sisi humwona tu kama muumini wa kawaida
asiye na maana. Yeye huona matukio yetu yote, na fikra na mawazo yetu
yote yanaanikwa wazi mbele Yake. Hakuna mtu ambaye hutilia maanani
uwepo Wake, hamna aliye na mawazo yoyote ya kazi Yake, na zaidi ya
hayo, hakuna mtu ana tuhuma yoyote kuhusu Yeye ni nani. Sisi
huendelea na kazi yetu tu, kana kwamba Yeye hahusiani nasi….
Kwa
bahati, Roho Mtakatifu huonyesha kifungu cha maneno “kupitia”
Kwake, na ingawa inaonekana ni jambo lisilotarajiwa, tunatambua kuwa
huo ni usemi wa Mungu, na tunakubali kwa urahisi kutoka kwa Mungu.
Hii ni kwa sababu, bila kujali ni nani anayeonyesha maneno haya,
ilimradi yanatoka kwa Roho Mtakatifu tunapaswa kuyakubali, na hivyo
hatuwezi kuyakana. Matamshi yajayo yanaweza kuwa kupitia kwangu, au
kwako, ama yanaweza kupitia yeye. Bila kujali ni nani, yote ni neema
ya Mungu. Ilhali bila kujali mtu ni nani, hatufai kumwabudu, kwa kuwa
bila kuzingatia chochote kingine, hawezi kuwa Mungu; hatuwezi kwa
njia yoyote kumchagua mtu wa kawaida kama huyu, kuwa ndiye Mungu
wetu. Mungu wetu ni mkubwa na mwenye kuheshimika; anawezaje
kuwakilishwa na binadamu wa kawaida asiye na umuhimu? Zaidi ya hayo,
sisi wote tunasubiri ujaji wa Mungu kuturudisha kwa ufalme wa
mbinguni, na kwa hivyo mwanadamu asiye na umuhimu mkubwa anawezaje
kuhitimu kufanya kazi ngumu kama hiyo? Bwana akirudi tena, ni lazima
iwe juu ya wingu jeupe, linaloonekana na wote. Huo utakuwa wa adhimu
namna gani! Itakuwaje Awe amejificha kwa ukimya kati ya kundi la watu
wa kawaida?
Na
bado ni huyu mtu wa kawaida aliyefichika kati ya watu ndiye
anayefanya kazi hii mpya ya kutuokoa. Yeye hafafanui chochote kwetu,
wala hatuelezi ni sababu gani Amekuja. Yeye tu, anafanya kazi
anayotarajia kufanya, na kwa mujibu wa mpango Wake. Maneno Yake na
matamshi Yake yanazidi kuja kwa wingi. Kuanzia kufariji, kuonya,
kukumbusha, na kupeana onyo mpaka kukaripia na kufundisha nidhamu;
kuanzia kutumia sauti ya upole mpaka kutumia maneno makali na ya
adhimu—yote yanatia huruma na hofu kwa mwanadamu. Kila kitu
Anachosema kinatufikia kwetu na kulenga siri zilizofichwa ndani yetu,
maneno Yake huchoma mioyo yetu, huchoma nafsi zetu, na hutuacha
tukiwa na aibu na wanyonge. Tunaanza kutafakari iwapo Mungu Aliye
katika roho ya huyu mtu kweli anatupenda, na nini hasa Anatarajia
kufanya. Labda tunaweza tu kuchukuliwa kwenda mbinguni baada ya
kuvumilia maumivu kama hayo? Vichwani mwetu tunafanya hesabu…
kuhusu hatima inayokuja na kuhusu majaliwa yetu ya baadaye. Bado
hakuna hata mmoja wetu anayeamini kwamba Mungu amechukua mwili na
hutenda kazi kati yetu. Japokuwa Amekuwa pamoja nasi kwa muda mrefu,
ingawa tayari Yeye amesema maneno mengi uso kwa uso nasi, bado hatuko
tayari kumkubali mtu aliye wa kawaida kiasi hicho awe Mungu wa
mustakabali wetu, wala hatuna nia ya kumwaminisha mtu asiye na maana
udhibiti wa mustakabali na hatima yetu. Kutoka Kwake, daima
tunafurahia ugavi wa maji ya uhai, na kwa sababu Yake tunaishi uso
kwa uso na Mungu. Sisi tunashukuru tu kwa neema ya Bwana Yesu aliye
mbinguni, na hatujawahi kamwe kupa umakini hisia za huyu mtu wa
kawaida mwenye kumilikiwa na uungu. Yeye bado, kwa unyenyekevu,
hufanya kazi akiwa amefichwa ndani ya mwili , akielezea sauti ya moyo
wake, bila kuzingatia kukataliwa Kwake na binadamu, inavyoonekana
milele kusamehe utoto na ujinga wa mwanadamu, na milele kuvumilia
mwanadamu kutomheshimu.
Pasipo
sisi kujua, huyu mtu asiye muhimu ametuelekeza katika hatua baada ya
hatua ya kazi ya Mungu. Sisi hupitia majaribu tele, na hukabiliwa na
kurudi kusikohesabika, na tunajaribiwa na kifo. Tunajifunza haki ya
Mungu na adhama ya tabia Yake, na kufurahia, upendo na huruma Zake,
tunakuja kufahamu nguvu za Mungu ambazo ni kubwa na hekima Yake,
tunashuhudia uzuri wa Mungu, na kutazama hamu Yake ya kumwokoa
mwanadamu. Kwa maneno ya huyu mtu wa kawaida, tunakuja kujua asili na
kiini cha Mungu, tunakuja kufahamu mapenzi ya Mungu, tunakuja kujua
asili ya mwanadamu na kiini cha mwanadamu, na tunapata kuona njia ya
wokovu na ukamilifu. Maneno yake hutufanya sisi tufe, na kutufanya
kuzaliwa upya; maneno yake hutufariji, na ilhali pia hutuacha tukiwa
tumejawa na hatia na hisia ya kuwa wadeni; maneno yake hutuletea
furaha na amani, lakini pia maumivu makubwa. Wakati mwingine sisi ni
kama wanakondoo wa kuchinjwa kwenye mikononi Yake; wakati mwingine
sisi ni kama kipenzi cha roho yake na kufurahia upendo wake na huba
yake; wakati mwingine sisi ni kama adui wake, waliofanywa majivu na
ghadhabu yake katika macho yake. Sisi ni wanadamu waliookolewa Naye,
sisi ni funza machoni pake, na sisi ni wanakondoo waliopotea ambao
Yeye hufikiria kuhusu kuwapata mchana na usiku. Yeye ni mwenye huruma
kwetu, anatudharau, yeye hutuinua, yeye hutufariji na kutuhimiza,
yeye hutuongoza, yeye hututia nuru, yeye huturudi na kutufundisha
nidhamu, na Yeye hata hutulaani. Yeye hujitia wasiwasi usiku na
mchana kwa ajili yetu, Yeye hutulinda na kututunza usiku na mchana,
na hatuachi kamwe, na Yeye hutoa utunzaji Wake wote kwetu na hulipia
gharama yoyote kwa ajili yetu. Miongoni mwa maneno ya mwili huu mdogo
na wa kawaida, tumefurahia ukamilifu wa Mungu, na kuona hatima ambayo
Mungu ametupa. Ila, licha ya haya, majivuno yangali mioyoni mwetu, na
sisi hatuna nia ya kukubali kikamilifu mtu kama huyu kama Mungu wetu.
Ingawa Yeye ametupa mana sana, mengi sana ya kufurahia, hamna kati ya
haya ambayo yanaweza kunyakua nafasi ya mungu katika mioyo yetu.
Tunaheshimu utambulisho maalum wa huyu mwanadamu na hadhi kwa kusita
pekee. Kama Yeye haneni na kutufanya kukiri kwamba Yeye ni Mungu,
basi sisi kamwe hatuwezi kukata kauli wenyewe na kukiri Yeye ni
Mungu, na kuwa Yeye yumo karibu kuja ilhali amekuwa akifanya kazi
kati yetu kwa muda mrefu.
Matamshi
ya mungu yanaendelea, na Yeye hutumia mbinu mbalimbali na mitazamo
kutuonya na kutuelekeza tutakachofanya na kueleza sauti ya moyo Wake.
Maneno Yake hubeba nguvu ya maisha, na hutuonyesha njia tunayopasa
kutembea, na yanatuwezesha kujua ukweli ni nini. Tunaanza kuvutiwa na
maneno Yake, tunaanza kuzingatia sauti Yake na jinsi anavyoongea, na
bila hiari tunaanza kuwa na hamu ya sauti ya moyo wa huyu mwanadamu
asiye wa ajabu. Yeye hufanya juhudi za mchwa kwa ajili yetu,
anapoteza usingizi na hamu ya chakula kwa ajili yetu, analia kwa
ajili yetu, anashusha pumzi kwa ajili yetu, anaugua magonjwa kwa
ajili yetu, anadhalilishwa kwa ajili ya wokovu na hatima yetu, na
moyo Wake huvuja damu na kulia kwa ajili ya uasi na kufa ganzi kwetu.
Utu kama huu na umiliki Wake haupo kwa upeo wa binadamu wa kawaida,
na hauwezi kumilikiwa na yeyote aliyepotoka. Ana uvumilivu na subira
isiyomilikiwa na mtu wa kawaida, na upendo Wake haumilikiwi na kiumbe
yeyote aliyeumbwa. Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo
yetu yote, au kufahamu asili yetu ama kiini chetu, ama kuhukumu uasi
wetu na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati
yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu wa mbinguni. Hakuna mtu ila Yeye
anayeweza kumiliki mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya
Mungu na kile Anacho na alicho yametoka, kwa ukamilifu wao, kutoka
Kwake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na
kutuletea mwangaza. Hakuna yeyote ila Yeye anayeweza kutufichulia
siri ambazo Mungu hajatufunulia tangu uumbaji hadi leo. Hamna yeyote
isipokuwa Yeye ambaye anaweza kutuokoa kutokana utumwa wa shetani ama
upotovu wa tabia yetu potovu Yeye huwakilisha Mungu, na kuonyesha
sauti ya moyo wa Mungu, ushawishi wa Mungu, na maneno ya hukumu ya
Mungu, yote ambayo huelekezwa kwa mwanadamu. Ameanza enzi mpya,
nyakati mpya, na akaleta mbingu na nchi mpya, kazi mpya, na
ametuletea matumaini, na akamaliza maisha ambayo si dhahiri, na
akatuwezesha kikamilifu kuona njia ya wokovu. Ameshinda ubinadamu
wetu wote, na kupata mioyo yetu. Tangu wakati huo na kuendelea, akili
zetu zinapata ufahamu, na nafsi zetu huonekana kufufuka: Huyu
mwanadamu wa kawaida asiyekuwa na umuhimu, ambaye huishi kati yetu na
kwa muda amekuwa akikataliwa na sisi—Je, si Yeye ni Bwana Yesu,
ambaye daima huwa kwa mawazo yetu, na ambaye tunamtamani usiku na
mchana? Ni Yeye! Ni Yeye Kweli! Yeye ni Mungu wetu. Yeye ndiye kweli,
njia, na uzima! Yeye ameturuhusu kuishi tena, na kuona nuru, na
kusimamisha mioyo yetu kuhangaika. Tumerudi nyumbani mwa Mungu,
tumerejea mbele ya kiti chake cha enzi, tuko uso kwa uso pamoja na
Yeye, tumeshuhudia uso wake, na tumeona barabara iliyo mbele. Wakati
huo, mioyo yetu imeshindwa kabisa na Yeye; hatuna shaka kuhusu Yeye
ni nani tena, wala hatupingi tena kazi na neno lake, na tunasujudu,
kabisa, mbele yake. Hakuna tunachotaka ila kufuata nyayo za Mungu
maishani mwetu mwote, na kufanywa wakamilifu naye, na kulipa fadhila
yake, na kulipa upendo wake kwetu, na kutii matayarisho na mipangilio
yake, na kushirikiana na kazi yake, na kufanya kila kitu tunachoweza
ili kukamilisha kile anachotuaminia.
Kushindwa
na Mungu ni kama mashindano ya kareti.
Kila
neno la Mungu hugonga eneo letu la ubinadamu, na hutuacha tukiwa
tumejawa na huzuni na hofu. Yeye hufichua fikra zetu, hufichua mawazo
yetu, na hufichua tabia zetu potovu. Kupitia kwa yale yote sisi
husema na kuyatenda, na kila wazo na fikra zetu, asili na kiini
zinafunuliwa kwa neno lake, na kutuacha na fedheha, tukitetemeka kwa
hofu. Anatueleza kuhusu matendo yetu yote, malengo yetu na nia, na
hata tabia potovu ambazo hatujawahi kugundua, na kutufanya tuhisi
kwamba tumewekwa hadharani, na hata kuhisi tumeshawishika vikamilifu.
Yeye hutuhukumu kwa ajili ya upinzani wetu Kwake, hutuadibu kwa ajili
ya kufuru kwetu na kumshutumu kwetu, na kutufanya tuhisi kwamba
hatuna thamani machoni pake, na kuwa sisi ni Shetani aishiye.
Matumaini yetu yanakufa, na kamwe hatuwezi kumpa madai yasiyo na
msingi au kumjaribu, na hata ndoto zetu kupotelea mara moja. Huu ni
ukweli ambao hakuna kati yetu anaweza kufikiria, na kwamba hakuna
yeyote kati yetu anayeweza kukubali. Kwa muda, akili zetu hukosa
msimamo, na hatujui tutakavyoendelea na barabara iliyo mbele wala
hatujui jinsi ambavyo tutaendelea katika imani zetu. Inaonekana kama
imani yetu imerudi kama ilivyokuwa mwanzoni, na ya kuwa hatujawahi
kumpata na kumtambua Yesu Kristo.
Kila kitu machoni petu hutushangaza, na kutufanya tuhisi ni kama
tumetupwa mbali. Tunasikitishwa, tunahuzunika, na ndani ya mioyo yetu
kuna ghadhabu ambayo haiwezi kufichika na pia kuna aibu. Tunajaribu
kujieleza, kupata suluhisho, na, hali kadhalika, sisi hujaribu
kuendelea kumsubiri Mwokozi Yesu, na kueleza mioyo yetu mbele yake.
Ingawa kuna wakati mwingine ambao hatuna kiburi wala unyenyekevu kwa
kutazamwa nje, mioyoni mwetu tunateseka na kuwa na hisia ya hasara
kuliko vile tumewahi kuwa nayo. Ingawa wakati mwingine tunaonekana ni
kama tuna utulivu kwa kutazamwa nje, ndani yetu tunavumilia bahari ya
mateso inayopanda na kushuka. Hukumu yake na kuadibu Kwake zimechukua
matumaini na ndoto zetu zote, na kutuacha bila tamaa zetu kuu na
kutokuwa tayari kuamini kuwa Yeye ndiye Mwokozi wetu anayeweza
kutuokoa. Hukumu Yake na kuadibu zimefungua ghuba kubwa kati yetu na
Yeye na hakuna aliye tayari hata kuivuka. Hukumu na kuadibu Kwake ni
mara ya kwanza kwamba sisi tunateseka kwa kupata shida kubwa hivi na
udhalilishaji kiasi kikubwa hivyo. Hukumu na kuadibu Kwake
vimetuwezesha kwa ukweli kuthamini heshima ya Mungu na kutovumilia
kwake kwa makosa ya binadamu, ikilinganishwa na ambavyo sisi ni watu
wa hadhi ya chini na najisi. Hukumu Yake na kuadibu vimetufanya sisi
kutambua kwa mara ya kwanza, jinsi ambavyo tuna kiburi na wenye
majivuno, na jinsi ambavyo mwanadamu kamwe hawezi kulingana na Mungu,
ama kuwa sawa na Mungu. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimetufanya
tutumaini kutoishi katika tabia potovu kama hiyo, na zimetufanya
tutamani kuacha asili kama hiyo na kiini kama hicho haraka
iwezekanavyo, na kamwe tusichukiwe Naye wala tusimchafue moyo. Hukumu
na kuadibu kwake vimetufanya tufurahie kutii neno Lake, na hatumo
tayari kamwe kwenda kinyume na matayarisho na mipangilio yake. Hukumu
na kuadibu Kwake kwa mara nyingine, zimetuwezesha sisi tuwe na tamaa
ya kutafuta uzima, na zimetuwezesha kufurahia kumkubali kama Mwokozi
wetu... Sisi tumetoka nje ya kazi ya ushindi, tumetoka kuzimu,
tumetoka nje ya bonde la uvuli wa mauti.... Mwenyezi Mungu
ametutamalaki, kundi hili la watu! Ameshinda dhidi ya Shetani, na
kuwashinda adui zake!
Sisi
ni kundi la watu wa kawaida waliomilikiwa na tabia potovu ya
kishetani, sisi ndio watu waliochaguliwa na Mungu kabla ya enzi, na
sisi ndio maskini ambao Mungu ameinua kutoka jaani. Kuna wakati
tulipomkataa na kumshutumu Mungu, ila sasa kumeshindwa na Yeye.
Tumepokea maisha na kupokea njia ya uzima wa milele kutoka kwa Mungu.
Bila kujali mahali ambapo tupo hapa duniani, licha ya mateso na
dhiki, hatuwezi kuwa mbali na wokovu wa Mwenyezi
Mungu.
Kwa kuwa Yeye ndiye Muumba wetu, na ukombozi wetu tu!
Upendo
wa Mungu unazidi kuenea kama maji ya chemichemi, na wewe unapewa, na
mimi pia, na kwake, na kwa wale wote ambao wanatafuta ukweli kwa
kweli na kungoja kuonekana kwa Mungu.
Kama
vile daima mwezi hufuata jua, kazi ya Mungu haiishi kamwe, na
inatekelezwa kwako, kwangu, kwake, na kwa wale wote ambao hufuata
nyayo za Mungu na kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu.
Ilielezewa
Machi 23, 2010
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni